Unavaa saa mkono gani?

Mimi navaa kushoto, lakin baada ya kuvaa sana saa mkono wa kushoto sasa hiv mkono una kama alama hiv, yaani ile sehem ya mkono imekua white tofauti na sehem nyingine ya ngozi.

Hii inakaaje wakuu inaweza kuniletea shida yeyote kiafya ?
 
Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.

Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.

#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.
Hii nimeipenda imewai kunitokea.
 
Nilikuwa navaa saa mkono wa kushoto nilibadilisha baada ya kuona wanawake wengi wanavaa mkono huo niliamua kuvaa mkono wa kulia mpaka sasa.

Sababu kubwa iliyonifanya nibadilike ni mpenzi wangu pia anavaa mkono wa kushoto na anaigeuza sehemu ya kuangalia mda inakuwa kiganjani, huangalia muda kila baada ya masaa kadhaa ya kazi kupita sasa jinsi anavyoangalia anavutia sana, niliona huu kumbe ni mkono wa kike nilivua saa yangu na kuivaa mkono wa kulia.

Ni mtazamo wangu tu, wenzangu sijui kwanini wanavaa mkono wa kulia au kushoto!
Ilikuwa ni uoga wako tuu

Suala la kuvaa au kutokuvaa saa mkono wakushoto halikuondolei au kukushushia hadhi yako kama mwanamume
Heshima na unadhifu wako kama mwanamume unaanzia kwanza kwenye akili yako
Wanaume wote maarufu ninaowafahamu wanavaa saa mkono wa kushoto ..na haijawaondolea sifa ya kuwa wanaume wenye heshima
Mfano

Magufuli,
Biden
Obama
Ronaldo
Majaliwa
Kikwete
Lewandowski
Lebron James

Na wengine weengi ,

Na pia watu wengi wanatumia mkono wa kulia kwa mambo mengi mfano unapokula chakula....kama ni saa ya mkanda wa chuma basi ni kash kash zisizo maana

unaweza kuta mtu ni fundi carpenter kwa hiyo mkono waa kulia kuanzia asubuhi hadi jioni ni nenda rudi ,Panda shuka..kwa hiyo ni rahisi saa kuharibika....

Kazi nyingi ngumu zinafanyika kwa mkono wa kulia, japokuwa siyo wote wanatumia mkono wa kulia kwa hiyo uwezekano wa Saa kuharibika ikivaliwa mkono wa kulia ni mkubwa zaidi

Hoja ya kusema kwamba unaacha kifanya jambo kwa sababu tu eti mwanamke au msichana anafanya hivyo hivyo ni ushamba

Kwa hiyo wanaume waache kucheza na kushabikia mpira wa miguu kwa sababau eti siku hizi kuna wanawake nao wanacheza mpira wa miguu kama wanaume?

Sent from my TA-1032 using JamiiForums mobile app
 
Navaa mkono wa kulia, ila SAA inakua upande wa kiganja hivyo huwa rahis kwangu kutazama muda.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom