Unaupimaje utendaji wa Waziri wa uchukuzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaupimaje utendaji wa Waziri wa uchukuzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Aug 11, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Unaupimaje utendaji wa Waziri wa uchukuzi?

  Katika ITV ya usiku wa leo nimemwona Mkuu wa uchukuzi akitia for a kwa vioja na kuonyesha hana taaluma ya utawala kwenye Nyanja zifuatazo:-

  1) Sina zogo na Mkuu kufanya "surprise checks" kwenye maeneo yake ya kikazi tatizo ni kuropoka juu ya hatma ya ajira wa kibosile wa TAZARA mbele ya wadogo zake huyo njemba………….wadogo tajwa hawana uhimili wa ajira ya bosi wao na wala uhusiano wa moja kwa moja na tija haupo sasa hizi purukshani za nini?


  2) Mkuu amekuwa akizibeza Bodi na menejimenti kwenye maeneo yake ya kikazi na hivyo kuzidhoofisha na kuzivunja moyo wa kutekeleza majukumu yake…………

  3) Zima moto za mkuu zinaficha ukweli wa ya kuwa matatizo makubwa ya kimfumo hayawezi kudhibitiwa na ukulele wa Mkuu tu…………….jambo ambalo linatia majonzi kuelewa ya kuwa domo la Mkuu siyo tiba ya uzembe na ubadhirifu ndani ya TAZARA.

  4) Ahadi ya kumtimua kibosile wa TAZARA hata kama Mkuu ataifanikisha na kuijaza nafasi tajwa na swahiba wake bado siyo ufumbuzi wa matatizo ya malipo duni ndani ya TAZARA na maamuzi dhoofisha ya awali yanaweza kutatuliwa na jitihada za mkuu peke yake jambo ambalo linatia shaka juu ya uwezo wa Mkuu katika kutakari hatma ya kitaifa iko wapi……………Ikumbukwe kibosile wa TAZARA lazima awe mzambia na Mwakyembe hana mamlaka ya kumteua, sasa haya majigambo ya kuwa ana uwezo wa kumfukuza kazi kibosile tajwa Mwakyembe ameyatoa wapi kama siyo kuleta usanii wa kisiasa tu?

  5) Bila ya Mkuu kutumia nyenzo zote alizonazo zikiwemo Bodi na menejimenti zake katika kufanikisha shughuli za umma kunaongeza mashaka kuwa kama jitihada hizi siyo za kugombea Uraisi mwaka 2015 na hazina uhusiano na kazi ya kuibua changamoto ndani ya wizara yake…….basi jinamizi lake ni siri kubwa........
   
 2. m

  mosagane Senior Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara anakagua daladala stand ya mwenge,mara anafukuza daladala stand ya mwenge eti ziende makumbusho,mara anakagua leseni za madereva ubungo Hivi yeye hana watendaji wa ngazi ya chini?au matataizo yote ya wizara yake atayamaliza yeye mwenyewe?anaboa bwana kwa kujifanya kufanya kila kitu na kutomwamini mtendaji hata mmomja ktk wizara yake.sijui ndo kuutaka urais?ngoja tusubiri
   
 3. k

  kajembe JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Sasa toa ushauri afanye nini? akae ofisini tu ili asiboe? Watanzania sijui tukoje jamani mtu akijaribu kufanya kazi tunamlaumu kwanini? kama wengine ni wazembe basi aangalie tu!kila kitu kibaya tu,Mtu akijaribu kujituma basi anatafuta Urais,akikaa kimya mtaema hafai kabisa amefanya nini nchi hii!Wengine ndiyo maana wamekata tamaa wameamua kushibisha matumbo yao maana sisi ni kulaumu kila kitu.Nchi hii inakatisha tamaa sana, kila mtu ana ajenda ya siri! Wapeni moyo watu wanao jitahidi kwa mazuri wanayofanya na mabaya wakosoeni lakini siyo kila kitu kibaya tu! sasa unataka waziri akae tu basi aangalie madudu napo utapiga kelele hawezi huyu mnafiki tu,basi onesha njia basi wewe!
   
 4. k

  kajembe JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Sasa wewe rutashiba sijui kitu gani! unasema anataka kuweka rafiki yake du wabongo tunachekesha sana,wewe aliyopo ndugu yako nini unaona atakosa ulaji! wapeni moyo watu wanaojitahidi kufanya kazi acheni majungu! mnakatisha tamaa watu wengine wanaamua kuangalia tu!kila kitu kukosoa tu du nchi hii ina laana ya aina yake sijawhi kuona.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Alisema anamfukuza wa TRC au TAZARA? mimi kama niliposikia alikuwa karakana za TAZARA. Tuwekane sawa, which is which?
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  mosagane Kichekesho ni kuwa juzi nilipanda basi Ubungo bado nikatozwa elfu tanoi zaidi ya nauli sasa mizunguko yake hapo kituo cha Ubungo ina tija gani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  zomba ninashukuru kwa masahihisho nimerekebisha...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  kajembe usichojua bosi kulingana na sheria lazima awe mzambia na Mwakyembe hana ubavu wa kumwondoa.....sijui tangia lini wazambia wakawa ni ndugu zangu.................la muhimu hapa ni kuwa tutaendelea kukosoa hadi majambozi yatakapowekwa sawa ni haki yetu ya kikatiba...................aache kuingilia watendaji ambao wamewekwa kisheria na hata katibu mkuu wake hamshirikishi kama ni kasi ya kwenda Ikulu hatafika........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  kajembe tumesema atumie vyombo atakuwa na ufanisi mkubwa kulikoni hii zima moto ya kuwanyang'anya wenzie majukumu yao. Hawezi kutatua lolote kwani hata bei za ubungo hazikubadilika kwa vile yeye alienda pale bali zinaendelea kupanda kinyemela.................nafikiri Mkuu anafanya haya ili kujijenga kwa mbio za uraisi za 2015 lakini hatafanikiwa............we are not that stupid..................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu mtu hafai kabisa anapenda sana cheap popularity.......ni mnafiki sana
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Sio hafai hajui anachokifanya anabwatabwata tu..eti mwambie ntamfukuza..hivi huyu ni waziri annayetoa maneno as if atafikuza mchunga mbuzi wake nyumbani..mwakyembe are u serious?
   
 12. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,487
  Likes Received: 2,146
  Trophy Points: 280
  Ruta,

  Kitu kikubwa kinachotakiwa ni kutendea kazi kile ambacho umeona Mwakyembe anapigia kelele. Wewe ndo umekosea. Fuata sheria siku nyingine hawataendelea. Umetozwa elfu 5 halafu ulichukuwa hatua gani? Sio kazi yake kukuangalia wewe umetendewa nini bali kukusaidia kujua haki yako.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  mlallilaN[/MENTION] nimekuelewa wewe na wengineo ambao kutokana na kuzidiwa na kero mwaona kheri njia za mkato hata kama hazitufikishi tutakakokwenda......................kuhusu nilifanya nini msafiri kafiri......................lengo langu ni kufika A-Town na sina muda wa kuingia gharama kubwa zaidi za kutatua matatizo ambayo Waziri mhusika alivalia njuga na sasa yamemshinda yako palepale........................hata hili la kuripoti hapa jamvini ni hatua ya kuelimisha umma ya kuwa tatizo bado lipo palepale.........................na kuendeleza mjadala wa kutafuta majibu yake............
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Yaya Toure[/MENTION] mimi sioni "future" ya Mwakyembe kwenye ulingo wa siasa hapa nchini.....................he is too ambitious but he lacks the political talent............
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Boflo ninaafiki hoja zako zote.......................huyu Mkuu anafikiri nchi yaendeshwa kwa vitisho na kudhalilishana hadharani..............................kama yeye kweli ni kibosile kwani atoe matambo kwa wadogo wa bosi kwa nini asimfuate ofisini na kumtambia kule kama siyo uabbaishaji na kutafuta umaarufu kwenye dirisha la vyombo vya khabari?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Inaelekea Mheshimiwa Mwakyembe yuko overexcited na madaraka yake hayo, na kushindwa kujua matumizi yake. Kufuatilia dala dalaau kukagua leseni siyo kazi ya waziri.. Tanzania ina miji mingi sana yenye daladala; hwezi kwenda sehemu zote hizo na kukagua madaladala hayo. Akiwa mchapa kazi, anatakiwa awape malendo subordinates wakke, halafu awasimamia kuhakikisha wanaleta results sahihi na zinazoendana na malengo.

  Ninajua kuwa iwapo katika kupitia mafaili ya ateule walioko chini yake akagundua makosa ,basi ana uhuru wa kuwachukulia hatua ya papo kwa papo, lakini siyo kukagua leseni za madereva au eti kukagua vituo vya daladala kwa kushtukiza.
   
 17. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  siku yake itafika tu huyu mnafiki...... hata akiumwa homa au akijikwaa huwa anaanza kutangaza kuwa wabaya wake ndio

  wamesababisha......na anafanya hivyo akijua kuwa watz wengi ni vilaza
   
 18. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Mwacheni afanye kazi kama hao walio chini yake hawawajibiki mnataka akae kimya!ili baadaye mje kumlaumu?watz bhana
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  [mention]
  masikitiko[/mention] tatizo ni kuwa anavunja sheria zilizopo kwa kuwaingilia wasaidizi wake wakati sheria hiyohiyo inampa madaraka ya kuiondoa bodi kama anaona imeshinwa kazi.....................swali kwanini haiondoi bodi anabakia kuingilia majukumu yake kama siyo kuleta vurugu kazini na kutamba mbele ya wapagasi anafikiri ndiyo uwaziri ulivyo?
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata sisi watz hatuamini watendaji wake wa chini kwa sababu wangekua wanafanya kazi zao kikamilifu kusingekua na matatizo tuliyonayo saivi so ni bora afuatilie mwenyewe hao watendaji wa chini watapewa rushwa afu watasema kila kitu kiko sawa
   
Loading...