Unaumizwa na mambo yaliyopita? Fanya yafuatayo (Sehemu 1)

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
474
1,000
IMG_20210427_142454_744.jpg


Jifunze kusamehe na kusahau, kutokuwa tayari kusamehe kutakufanya uendelee kuumizwa na mambo yaliyopita na kushindwa kuendelea na maisha yako

Jiruhusu kusikia maumivu, linapokukuta jambo la kuumiza kama kufiwa ni vyema ukaruhusu maumivu kwa wakati ule ili yaishe kutofanya hivyo kutasababisha uumie kwa muda mrefu zaidi
 
Upvote 0

hellefay

Member
May 16, 2018
61
125
Mimi ni mhanga wa hili..nilifiwa na mtu wangu wa karibu sana yapita miaka sita,lakini haipiti wik bila kumkumbuka,na pia kila ikifika tarehe ya siku aliyotwaliwa hua naumia hata kazin nakua moodless . NATAMAN HII HALI YA KUUMIA INITOKE KABISA.
 

Kapyepye Mfyambuzi

JF-Expert Member
Jun 18, 2020
398
500
Mimi ni mhanga wa hili..nilifiwa na mtu wangu wa karibu sana yapita miaka sita,lakini haipiti wik bila kumkumbuka,na pia kila ikifika tarehe ya siku aliyotwaliwa hua naumia hata kazin nakua moodless . NATAMAN HII HALI YA KUUMIA INITOKE KABISA.
Pole Sana
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,231
2,000
Jiruhusu kusikia maumivu, linapokukuta jambo la kuumiza kama kufiwa ni vyema ukaruhusu maumivu kwa wakati ule ili yaishe kutofanya hivyo kutasababisha uumie kwa muda mrefu zaidi
ndiyo maana watu huhakikisha wamekwenda kuzika. Unapotupa udongo kaburini kumfukia mpendwa wako, wala hutajua machozi yametoka wapi - hapo ndipo maumivu yanafanya kazi yake, na ndiyo mwanzo wa kuanza kusahau.
Niliwahi kumuona mama mmoja akiwambia watu msibani - mwacheni alie tu, msimzuie!
 

commentor

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
526
500
Jambo lingine katika masuala ya kufiwa ni lazima mtu afahamu kwamba yapo nje ya uwezo wetu. Kila nafsi hai ipo huru na ina muunganiko na muumba wake. Tufurahie uwepo wake ikingalipo, na tujifunze kukubaliana na uhalisia wa maisha kwamba ipo siku tutatengana tu. Iwe ni mtoto, mke, mume, mzazi, rafiki kipenzi, ndugu wa damu n.k.

Sikitika kwa kiasi, tafuta namna ya kuenzi mazuri yake, maisha yaendelee.
 

commentor

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
526
500
Kwa masuala ya kupoteza vitu vya thamani, kudhulumiwa, kuonewa kwa kiwango cha juu na mengine yanayofanana na hayo; fahamu kwamba huo sio mwisho wa maisha. Pia usijisumbue kulipa kisasi kwa vile ulimwengu wenyewe hulipa kwa kiwango kile kile au hata kuzidi ulichofanyiwa na mtu. Ukiwa na bahati hakika utashuhudia namna ulimwengu (universe) umekulipia madhira uliyofanyiwa. Piga moyo konde, ongea na watu unaowaamini, kama una imani - omba Mungu, maisha yaendelee.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom