Unauaga mwaka 2021 ukiwa ni mwaka wa aina gani kwako?

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,008
68,154
Habari zenu wakuu, herini kwa sikukuu pendwa za mwisho wa mwaka. Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2021 kwanza tumshukuru Mungu kwa zawadi ya huu mwaka na uhai hadi sasa tukiwa na imani ya kuuona mwaka mpya 2022.

2021 umekuwa na mambo mengi mazuri na mabaya, inawezekana kwa wengine ni mwaka wenye nuru, furaha, amani na mafanikio tofauti kabisa na miaka mingine iliyopita.

2021 kwangu ni tofauti kabisa ni mwaka ambao umekuwa mgumu sana kwangu sijapiga hatua kurudi nyuma lakini nmekutana na ya kuniumiza, kunikatisha tamaa lakini yote yameniachia somo kwenye maisha.

Nilipata ajali nkatumia akiba yote kujiuguza namshukuru Mungu kwa sasa nipo vyema japo ilikuwa ni mateso(nilipotea hadi humu jf for months) Ndani ya hiki kipindi niliachwa na mpenzi wangu baada ya kujua nimepata ajali alinitafuta na kunijulia hali na kuniahid atakuja jioni kunijulia hali lakini ndio mpaka kesho hakuwahi kuja wala kuulizia hali yangu na sijawahi kumtafuta tena. Sasa nipo singo nainjoiii

Rafiki wa kweli yupo? Ni nani? Rafiki wa kweli ni pesa huyu ndie anaekujali kwa kukutimizia mahitaji yako on time. Marafiki wanafki sana nmegundua hili ndani ya mwaka huu. Ndugu ndio kabisa kikubwa ni kuwafumbia macho na kuziba masikio ili usiyape mda wako.

Mambo ya familia ndani ya huu mwaka ndio pasua kichwa sipendi kabisa kuyaongelea nayo yamechangia kwa % kubwa mwaka kuwa mgumu kwangu. Kuna mda nawaza nisijali chochote lakini nna moyo wa kujali najikuta tu najali bila kujua madhara yake, hii kitu inamaliza furaha wakuu. Migogoro+misiba.

Kiuchumi kila nachokifanya ili kujiweka vizuri kinasua sua mambo yakianza kuwa sawa yanatokea matatzo yanafyeka akiba yote na mambo yanaanza kuvurugika.

Huu mwaka na uishe tu hapa imenipiga homa ya december ndio nafungia nayo mwaka, natumaini 2022 utakuwa mwaka wenye uafadhali kwenye mengi.
Pole kwa wale waliokutana na magumu ndani ya huu mwaka ni sehemu ya maisha kikubwa ni kutokukata tamaa kamwe.

Karibu sana mwaka 2022, ukawe mwaka wenye baraka na mafanikio kwa kila mmoja wetu.
 
1.ni mwaka mzuri kwani kwa Mara ya Kwanza nimepata ajira
2.nasikitika Sana kumpoteza mtu ambaye hotuba zake zilikuwa zinanivutia kuliko watu wote duniani RIP JOHN POMBE
3.Ni mwaka wa mwisho kunywa pombe,kuvuta bangi,sigara,kupiga pull.kwangu mimi nimefanikiwa kukaa kwa muda mrefu bila kutumia au kufanya vitu ambavyo kiukweli nilikuwa na mazoea navyo Sana...
 
Huu mwaka ¼ ya mwanzo ilikuw tamu sana, ila baada mzee kututoka kiukweli kwangu mambo yamekuw yote ya kinijia kiume

Hadi sasa nimeshindw kutekezeleza malengo yangu kwa 64%

Nazn hata sera za Taifa letu zmepelekea mambo mengi kuwepo au kuja bila yakutabilika

R. I. P. Magu.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu nafasi ya kufanya mambo bado ipo kikubwa uzima na afya njema.
 
Habari zenu wakuu, herini kwa sikukuu pendwa za mwisho wa mwaka. Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2021 kwanza tumshukuru Mungu kwa zawadi ya huu mwaka na uhai hadi sasa tukiwa na imani ya kuuona mwaka mpya 2022.

2021 umekuwa na mambo mengi mazuri na mabaya, inawezekana kwa wengine ni mwaka wenye nuru, furaha, amani na mafanikio tofauti kabisa na miaka mingine iliyopita.

2021 kwangu ni tofauti kabisa ni mwaka ambao umekuwa mgumu sana kwangu sijapiga hatua kurudi nyuma lakini nmekutana na ya kuniumiza, kunikatisha tamaa lakini yote yameniachia somo kwenye maisha.

Nilipata ajali nkatumia akiba yote kujiuguza namshukuru Mungu kwa sasa nipo vyema japo ilikuwa ni mateso(nilipotea hadi humu jf for months) Ndani ya hiki kipindi niliachwa na mpenzi wangu baada ya kujua nimepata ajali alinitafuta na kunijulia hali na kuniahid atakuja jioni kunijulia hali lakini ndio mpaka kesho hakuwahi kuja wala kuulizia hali yangu na sijawahi kumtafuta tena. Sasa nipo singo nainjoiii

Rafiki wa kweli yupo? Ni nani? Rafiki wa kweli ni pesa huyu ndie anaekujali kwa kukutimizia mahitaji yako on time. Marafiki wanafki sana nmegundua hili ndani ya mwaka huu. Ndugu ndio kabisa kikubwa ni kuwafumbia macho na kuziba masikio ili usiyape mda wako.

Mambo ya familia ndani ya huu mwaka ndio pasua kichwa sipendi kabisa kuyaongelea nayo yamechangia kwa % kubwa mwaka kuwa mgumu kwangu. Kuna mda nawaza nisijali chochote lakini nna moyo wa kujali najikuta tu najali bila kujua madhara yake, hii kitu inamaliza furaha wakuu. Migogoro+misiba.

Kiuchumi kila nachokifanya ili kujiweka vizuri kinasua sua mambo yakianza kuwa sawa yanatokea matatzo yanafyeka akiba yote na mambo yanaanza kuvurugika.

Huu mwaka na uishe tu hapa imenipiga homa ya december ndio nafungia nayo mwaka, natumaini 2022 utakuwa mwaka wenye uafadhali kwenye mengi.
Pole kwa wale waliokutana na magumu ndani ya huu mwaka ni sehemu ya maisha kikubwa ni kutokukata tamaa kamwe.

Karibu sana mwaka 2022, ukawe mwaka wenye baraka na mafanikio kwa kila mmoja wetu.
Mwaka wa kindezi tu no serious achievement,nimepoteza ndugu muhimu sana huu mwaka yani it should just leave.

Im hoping for the best next year.
 
1.ni mwaka mzuri kwani kwa Mara ya Kwanza nimepata ajira
2.nasikitika Sana kumpoteza mtu ambaye hotuba zake zilikuwa zinanivutia kuliko watu wote duniani RIP JOHN POMBE
3.Ni mwaka wa mwisho kunywa pombe,kuvuta bangi,sigara,kupiga pull.kwangu mimi nimefanikiwa kukaa kwa muda mrefu bila kutumia au kufanya vitu ambavyo kiukweli nilikuwa na mazoea navyo Sana...
Hongera mkuu kwa mafanikio hayo ila pole kwa kumpoteza JPM
 
Ulikuwa mwaka poa sana kwangu, sema vile Mie ndo sikujiandaa kwenda nao maana mkwanja niliopata uwekezaji nimefanya kidogo mno Hadi najiona bwege

Kimahusiano nimeachwa pia na mpz wangu kisa dini na hapa ni baada ya kumpa mtaji ila sijawah lalamika maana miezi mi 2 mbele alirudi kuomba msamaha nikamkazia

Kiafya pia nafunga kwa homa, Hadi dr. Kadata ile kukuta nba joto 39 kataka anichome sindano kushusha joto nkagoma

Mwaka 2022 ukiwa kama 2021 ntafurahi sana.
 
Kama fungu bado lipo wekeza. Mapenzi ni janga mi nishayapa kisogo kwa muda.
 
Duuh, kwa mwaka huu kama ngekuwa nna remote ngefoward tu mpaka mwisho wa awamu hii ya sita,, maana sio kwa kupoa huku. Nchi haina mchaka mchaka, tofaut na awam ya tano, , mara uku fulani katumbuliwa mara pale usafi nchi nzima, mara kule raisi kampandsha cheo fulani kwa kchapa kaz yaan had raha

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Hii awamu ya mwenye msemo wake wa MIMI NI MAMA utadhani aliambiwa yeye ni baba.
 
Back
Top Bottom