Unatumiaje kipato chako, kuboresha mazingira ya kijiji ulipotoka?

Watu wengi ni wabinafsi sana; na hii inaathiri hata uhusiano kwa jamii inayomzunguka. Una miaka mingi uko mjini unapambana kutafuta kipato; na wapo waliofanikiwa kwa kuwa na kipato kingi cha ziada.

Matokeo yake, kipindi cha mapumziko (likizo), unaenda kuwatembelea kijijini ulikozaliwa, na kuwatimulia vumbi zito; huku hujawahi kuchangia maendeleo yoyote katika kijiji chako.

Swali: Unatumiaje kipato chako, kuboresha mazingira ya kijiji ulipotoka?
Nalipa kodi
 
Jana kumetokea taarifa za Tanzia toka Songea -Mfaranyaki,Daktari mmoja bingwa wa neva toka Muhimbili alipeleka msiba wa mdogo wake.Walipokuwa wakiaga naye akadondoka ghafla na kufariki wakati alikuwa mzima hana shida yoyote.Mambo kama haya yanaogopesha kwa baadhi ya maeneo.
Waafrika kila familia ina mijichawi yenye chuki isiyopenda wenzao wafanikiwe na kuendelea
 
Ujamaa na kujitegemea??

Kila mtu apambane na familia yake mkuu, saidia kulingana na uwezo wako unapofikia uwijitese kubeba misalaba ya watu wengine..

saidia sana kwa kile kilicho ndani ya uwezo wako tena bila kujali shukrani, lakini kama huna uwezo acha usijitese kufurahisha mtu ili jamii ikuone mtu mwema utajuta!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom