Unatumiaje kipato chako, kuboresha mazingira ya kijiji ulipotoka?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,323
40,172
Watu wengi ni wabinafsi sana; na hii inaathiri hata uhusiano kwa jamii inayomzunguka. Una miaka mingi uko mjini unapambana kutafuta kipato; na wapo waliofanikiwa kwa kuwa na kipato kingi cha ziada.

Matokeo yake, kipindi cha mapumziko (likizo), unaenda kuwatembelea kijijini ulikozaliwa, na kuwatimulia vumbi zito; huku hujawahi kuchangia maendeleo yoyote katika kijiji chako.

Swali: Unatumiaje kipato chako, kuboresha mazingira ya kijiji ulipotoka?
 
Huwa tunafanya Harambe Mara Kwa Mara.. Kulingana na changamoto tunayotaka kutatua huko uchagoo.. Ni utaratibu tuliukuta.. Na tunauendeleza.
 
Inategemea na uhitaji na swala linaloglhitajika kutatuliwa. Sometimes tunaweza vusha mwaka bila kuitishwa michango. Au angalau mara Moja Kwa mwaka. Mambo mengi yametatuliwa.. Yamebaki machache.
Utaratibu wenu uko vizuri
 
Utaratibu wenu uko vizuri
Yap, ni utaratibu mzuri.. Ambao umegeuka kuwa sehemu ya maisha. Imekuwa lazima kuchanga, either fedha taslimu au nguvu kazi Marika kufanikisha hitaji husika. Kila mmoja lazima ajitolee kijijini pale. Imekuwa kawaida Sasa.
 
Nimepambana sana kuwapatia umeme lakini nguvu yangu inapungua, naamini siku moja nitafanikiwa, napenda sana kijijini kwetu, naenda mara kwa mara,makazi yangu ya kudumu pia nayafanya huko, watoto wangu wataanzia huko, utoto wao(makuzi ya awali) watakuwa huko, hata mwisho wa uhai wangu nintatamani ukome nikiwa huko. Asante kwa uzi mzuri.
 
Watu wengi ni wabinafsi sana; na hii inaathiri hata uhusiano kwa jamii inayomzunguka. Una miaka mingi uko mjini unapambana kutafuta kipato; na wapo waliofanikiwa kwa kuwa na kipato kingi cha ziada. Matokeo yake, kipindi cha mapumziko (likizo), unaenda kuwatembelea kijijini ulikozaliwa, na kuwatimulia vumbi zito; huku hujawahi kuchangia maendeleo yoyote katika kijiji chako.

Swali: Unatumiaje kipato chako, kuboresha mazingira ya kijiji ulipotoka?
Ngoja Kwanza ma NGULI wa elimu chafu ya kutesana wapungue kidogo.

Kila anayejarubu kusomesha ndugu, jamaa au rafiki na hata jirani hadumu. Wanamtuliza kwenye jeneza
 
Ngoja Kwanza ma NGULI wa elimu chafu ya kutesana wapungue kidogo.

Kila anayejarubu kusomesha ndugu, jamaa au rafiki na hata jirani hadumu. Wanamtuliza kwenye jeneza
Jana kumetokea taarifa za Tanzia toka Songea -Mfaranyaki,Daktari mmoja bingwa wa neva toka Muhimbili alipeleka msiba wa mdogo wake.Walipokuwa wakiaga naye akadondoka ghafla na kufariki wakati alikuwa mzima hana shida yoyote.Mambo kama haya yanaogopesha kwa baadhi ya maeneo.
 
Inahuzunisha
 
Ni kweli wengi ni wabinafsi wanataka wakienda kijijini wakatambe tu. Wengi hawana moyo wa kujitolea kusaidia mazingira ya jamii walizotoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom