Unatumia mswaki gani?

Colgate Max fresh
Dawa ya meno safi sana
IMG_20210731_120058_mfnr.jpg
 
Me hata sijui jina lake..nachojua naukutaga kwenye box la whitedent Basi.
 
Miswaki ya siku hizi haina ubora kiukweli.

Mi ni mtu nazingatia sana usafi wa kinywa ila naangushwa na miswaki ya siku hizi, Whitedent ndo ilikuaga miswaki yangu bora ila naona nao wameanza kuregeza.

Nataka mswaki ukipita kinywani jino na fizi viitikie.

Nyie mnatumia miswaki gani uko?
Miswaki ni mingi, mimi ninatumia colget na mingine haina jina ya kichinachina.Inauzwa kwenye maduka yanaitwa Litle more.

Kuwa makini: Nimeona unasema unataka ukipiga mswaki meno na fizi viitikie. Japo sijajua unamaanisha nini hasa,lakini, nakutahadharisha kuepuka miswaki yenye brashi ngumu kupitiliza. Hakikisha brashi zinaweza kulala unapotumia. Kuna miswaki hata ile ya gharama,migumuu utasema ya kusugulia sakafu. Hiyo haifai. Shida kubwa ya brashi ngumu na kutumia nguvu ni kwisha kwa tabaka la juu la meno(enamel, sijui kama nimepatia).

Enamel ikiisha, utaanza kupata tatizo la sensitivity. Hapo utasahau ukoko wa ubwabwa, kitumbua kilichokauka, nyama iliyokauka na usilogwe utafune kamfupa ama jiwe.Hata mtu akikikwangua ama kukereza kitu ,mfano, msumari juu ya sakafu ,kraaaaaaaaaah! utakoma. Mimi ni victim wa tatizo hili,hivyo, sasa nimekuwa mpole,ninatafuta miswaki bora na laini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom