Unatumia memory card ya aina gani? je ni sahihi kwako?

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,703
39,776
leo nimeona tuzungumzie kuhusu hizi memory card. mtu anapotaka kununua memory card huulizia brand name tu ipi nzuri wengine watajibu sandisk wengine watajibu kingstone ila kila mtu atajibu lake. lakini tujiulize kitu kimoja kama laptop au simu tunachagua kwa perfomance na matumizi yetu je hizi memory card hazina specs kama vifaa vyengine?

jibu ni kwamba ndio memory card zina specs kama vifaa vyengine na ni vizuri kuchagua inayokidhi mahitaji yako. kuna wakati unaweza ukaona simu ipo slow au haichukui vizuri video pamoja na kucheza game tatizo hili linaweza kuchangiwa na memory card.

kwenye kuchagua memory card mambo mawili ni muhimu kuangalia.

1. ukubwa wa memory.
hapa nafkiri kila mtu anajua na wala nisipaelezee kirefu kila mtu anajua gb ngapi zinamtosha kuhifadhi mambo yake.

2. speed ya memory card.
hapa ndio dhumuni la hii thread watu wengi hawafahamu kuwa memory card zinatofautiana speed unaweza nunua memory card ikawa kimeo na kufanya kifaa kiwe slow.

memory card zimeekwa class kutokana na speed zake kuna class hizi hapa.

-class 2
-class 4
-class 6
-class 8
-class 10

zipo class za juu zaidi ila hizi zinatosha kumuelewesha mtu. class 2 inamaana speed yake ni 2MB/ps ikiwa class 6 ina maana 6MB/ps na class 10 ni 10MB/ps

hivyo ina maana jinsi inavyopanda ndio jinsi memory card inavyokua na speed.

tuchukulie mfano huu una simu inayorekodi hd utakapokua unachukua video za hd na memory card class 2 hio video haitatoka vizuri sababu video ni kubwa na speed ya kuandika memory card ni ndogo. same kwenye activities nyengine itakua slow.

je utatambuaje class ya memory card?
hii utaiangalia kwa juu kabisa ya memory card wanaandika class yake. ukiona hawajaandika ujue hio memory card ina walakin.

pnreggd.jpg

hitimisho
ni vizuri ukanunua memory card class 10 yenye brandname nzuri ili kupata perfomance nzur
 
Nilikuwa sijui hii kitu. Lakini mimi sijawahi kukutana na memory card hata moja ambayo ina label ya class yake. Na unaweza ukapima vipi kama kweli hiyo ni class yake kwa kuangalia tu label???

ukishaona label ni rahisi kuhakikisha kwa computer ukiieka kwenye modem au card reader ikihamisha file pale inaonesha speed. kama ni class 10 speed haitakiwi kushuka 10MB/ps kama ikishuka ina maana mwenye duka amekudanganya na hata ukiirudisha anatakiwa akurudishie hela au aibadilishe hio memory card
 
Memory nyingi mjini nifake kuwa mwangalifu sana. Nyingi class 10 huwa ni class 4. Hakikisha kama ni sandisk class 10 anakupa na warantee. Na huwa hizo ni mara 2 ya bei au zaidi ya za kawaida

Sent from my Samsung Note III using Tapatalk
 
leo nimeona tuzungumzie kuhusu hizi memory card. mtu anapotaka kununua memory card huulizia brand name tu ipi nzuri wengine watajibu sandisk wengine watajibu kingstone ila kila mtu atajibu lake. lakini tujiulize kitu kimoja kama laptop au simu tunachagua kwa perfomance na matumizi yetu je hizi memory card hazina specs kama vifaa vyengine?

jibu ni kwamba ndio memory card zina specs kama vifaa vyengine na ni vizuri kuchagua inayokidhi mahitaji yako. kuna wakati unaweza ukaona simu ipo slow au haichukui vizuri video pamoja na kucheza game tatizo hili linaweza kuchangiwa na memory card.

kwenye kuchagua memory card mambo mawili ni muhimu kuangalia.

1. ukubwa wa memory.
hapa nafkiri kila mtu anajua na wala nisipaelezee kirefu kila mtu anajua gb ngapi zinamtosha kuhifadhi mambo yake.

2. speed ya memory card.
hapa ndio dhumuni la hii thread watu wengi hawafahamu kuwa memory card zinatofautiana speed unaweza nunua memory card ikawa kimeo na kufanya kifaa kiwe slow.

memory card zimeekwa class kutokana na speed zake kuna class hizi hapa.

-class 2
-class 4
-class 6
-class 8
-class 10

zipo class za juu zaidi ila hizi zinatosha kumuelewesha mtu. class 2 inamaana speed yake ni 2MB/ps ikiwa class 6 ina maana 6MB/ps na class 10 ni 10MB/ps

hivyo ina maana jinsi inavyopanda ndio jinsi memory card inavyokua na speed.

tuchukulie mfano huu una simu inayorekodi hd utakapokua unachukua video za hd na memory card class 2 hio video haitatoka vizuri sababu video ni kubwa na speed ya kuandika memory card ni ndogo. same kwenye activities nyengine itakua slow.

je utatambuaje class ya memory card?
hii utaiangalia kwa juu kabisa ya memory card wanaandika class yake. ukiona hawajaandika ujue hio memory card ina walakin.

pnreggd.jpg

hitimisho
ni vizuri ukanunua memory card class 10 yenye brandname nzuri ili kupata perfomance nzur

wee jamaa Mkali sana, big up. kuna siku nilizungumzia speed ya storage devices humu jukwaani kuna jamaa akaniambia hapo nimewadanganya . ila huo ndio ukweli 100% 100%
 
thanks mkuu chief-mkwawa, sijajua bado yangu ni class gani ila natumia sony sd nlonunua kwenye workshop yao. naogopa kuichomoa hapa maana 90% ya apps zangu zpo kwa memory
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo hilo neno class huwezi kuliona kwa kutumia sim mpaka kwenye omputer? make mi natumia cm. nisaidie jibu mkuu

kaka angalia hio picha niliyoeka nimezungusha duara jekundu hio ni class 6. njia ya kuijua hutumii computer unaangalia tu nyuma ya memory card ila utatumia computer kuprove speed.
 
thanks mkuu chief-mkwawa, sijajua bado yangu ni class gani ila natumia sony sd nlonunua kwenye workshop yao. naogopa kuichomoa hapa maana 90% ya apps zangu zpo kwa memory

sony wana memory card hadi za laki mbili za 4gb. hua kwa quality hawa jamaa hawana wasiwasi tatizo tu ni bei. na sd zao mara nyingi ni uhs ambazo speed ni 45MB/ps kupanda sikuzieka hapa sababu sidhani kama kuna watu wanatoa hela nyingi kuzinunua.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom