Unatatua vipi changamoto ya housegirl mwenye mtoto?

Mahondaw

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
61,972
156,266
Nawasalimu katika jina la aliye juu wapendwa! As the topic is concerned, how do you handle changamoto za housemaid mwenye mtoto nawe una watoto?

Ni wiki mbili sasa niko na dada wa kazi mwenye mtoto tena mtoto mdogo guys mdogo sana. Ni baada ya connections zote kufeli so sikuwa na namna majukumu yalinibana aliyepatikana ana mtoto wa 6 months wapendwa ningefanyaje sasa?!

Watoto wa kuwaangalia ni watatu, wawili wana umri wa miaka 5 wapo chekechea mwingine ana miaka miwili na miezi 7. Sasa huyu wangu mdogo anaumwa. Kama mnavyojua mtoto mdogo akiumwa analialia kukosa raha na lile deko seriously anahitaji care ya kimataifa na huyu wake analia hatari si usiku si mchana. Haya wake analia wangu analia na kutaka kubebwa guys mnahandle vipi hili??

Unaweza kuta ni asubuhi muda wa kuamka kuandaa na kuhudumia hawa wanaoenda chekechea mtoto wake amekesha analiaa stili analia na anatakiwa kuamka kuendelea na kazi au ameamka asubuhi mwanae analia njaa sana huku wanangu nao ni muda wa kuandaliwa chai kwani hawapendi uji kabisa so ni kunywa maziwa; afanye kipi na katoto kake kanalia mnoo!!

Yaani kwa asilimia 200 mtoto anaathiri utendaji kazi wa mamake wiki 2 nilienda kazini na huyu mdogo wale wakitoka shule nao walikua wananifata kazini yani ofisi ilikuwa kama daycare aisee mara wapande dirishani makelele sasa niliongea mpaka hapo nilikua nikirudi nyumbani kila kitu kinaniangalia nalala hooi, mgongo sasa hizi shughuli za kuinamaima muda mwingi lol mgongo unaumaa
 
Kuwa na housegirl mwenye mtoto ni mtihani sana. Hasa pale anapotakiwa kutimiza majukumu yake alafu mtoto wake aanze kulia. Nilikuwa nae kipindi flani, ila yeye alikuwa akimuacha mtoto analia ili afanye kazi na tatizo lilikuwa mwanae alikuwa anakataa watu isipokuwa mama yake tu.

Ilisababisha kumuondoa na ilipelekea akahisi labda sipendi watoto. Ila kwa upande wangu nilione yeye kumlea mwanae ni muhimu sana kuliko hizi kazi ninazompa. Nakushauri endelea kutafuta housegirl mwingine na utakapompata muondoe huyu aliyekuepo maana hiyo hali kubadilika ni ngumu sana na kufanya hivyo inahitaji moyo mgumu sana.
 
Kiukweli hapo ni mtihani.

Na watoto watakuwa affected whether you like it or not.

Do this, tafuta msichana asiekuwa na mtoto and I assure you wapo wengi mimi nawachukua almost 10 years now kutoka kwa Agents hapa hapa Dar es Salaam. It's pricy lakini siumizi kichwa na background check wanakuwa wameshafanyiwa.

Then huyo ulie nae let her go lakini help her to find her own path in this life. Kama upo vizuri hata mtaji wa kuanza ka biashara kadogo dogo so she can survive because mpaka anafanya Kazi na mtoto ni muhitaji.

All the best.
 
Kuwa na housegirl mwenye mtoto ni mtihani sana. Hasa pale anapotakiwa kutimiza majukumu yake alafu mtoto wake aanze kulia. Nilikuwa nae kipindi flani, ila yeye alikuwa akimuacha mtoto analia ili afanye kazi na tatizo lilikuwa mwanae alikuwa anakataa watu isipokuwa mama yake tu. Ilisababisha kumuondoa na ilipelekea akahisi labda sipendi watoto. Ila kwa upande wangu nilione yeye kumlea mwanae ni muhimu sana kuliko hizi kazi ninazompa. Nakushauri endelea kutafuta housegirl mwingine na utakapompata muondoe huyu aliyekuepo maana hiyo hali kubadilika ni ngumu sana na kufanya hivyo inahitaji moyo mgumu sana.
Asante mkuu no way inanibidi nifanye hivo tu
 
Ilikuwa 2015 kwetu wakaleta house maid ana watoto wawili. Kwanza alikuja mwenyewe akakaa mwezi hivi kisha akaenda kuwafata watoto wake, mwanzoni hatukujua ana watoto, wana kama miaka minne na miwili.

Ilitokea msiba kwa jirani na mmoja wa waombolezaji akamtambua yule dada kumbe alimtoroka mume wake aliyekuwa anamtesa. Mumewe kujua vile akauza nguruwe kuja kukuchukua familia yake. Siku anafika tuko sebuleni tunaona madogo wanamkimbilia baba, alitoroka na mmoja mwingine mama yake tukampa nauli arudi mkoani kwao alisema harudi tena kwa mumewe anateseka.

Wana visa hao hasa baba mtoto akiingilia kati. Ila huwa wanakaa sana kama mtoto kakua kidogo. Aunt yangu mwaka wa tano huu ana maid aliyekuja mjamzito na mwanae kashamuandikisha nursery. Ila kama huna uwezo wanasumbua
 
Kiukweli hapo ni mtihani.

Na watoto watakuwa affected whether you like it or not.

Do this, tafuta msichana asiekuwa na mtoto and I assure you wapo wengi mimi nawachukua almost 10 years now kutoka kwa Agents hapa hapa Dar es Salaam. It's pricy lakini siumizi kichwa na background check wanakuwa wameshafanyiwa.

Then huyo ulie nae let her go lakini help her to find her own path in this life. Kama upo vizuri hata mtaji wa kuanza ka biashara kadogo dogo so she can survive because mpaka anafanya Kazi na mtoto ni muhitaji.

All the best.
Thanks dear yeah ni muhitaji sana
 
Ilikuwa 2015 kwetu wakaleta house maid ana watoto wawili. Kwanza alikuja mwenyewe akakaa mwezi hivi kisha akaenda kuwafata watoto wake, mwanzoni hatukujua ana watoto, wana kama miaka minne na miwili.

Ilitokea msiba kwa jirani na mmoja wa waombolezaji akamtambua yule dada kumbe alimtoroka mume wake aliyekuwa anamtesa. Mumewe kujua vile akauza nguruwe kuja kukuchukua familia yake. Siku anafika tuko sebuleni tunaona madogo wanamkimbilia baba, alitoroka na mmoja mwingine mama yake tukampa nauli arudi mkoani kwao alisema harudi tena kwa mumewe anateseka.

Wana visa hao hasa baba mtoto akiingilia kati. Ila huwa wanakaa sana kama mtoto kakua kidogo. Aunt yangu mwaka wa tano huu ana maid aliyekuja mjamzito na mwanae kashamuandikisha nursery. Ila kama huna uwezo wanasumbua
Hilo la kuwahudumia yeye na mtoto si tatizo tatizo ni management ya majukumu na mtoto mdogo ambae si kwamba anaenda kucheza no ni mdogo, binti ana 15 alibebeshwa na denti form 3
 
Ninaye mwenye mtoto tangu September mwaka jana alikuja na mtoto akiwa na mwaka mmoja na miezi kadhaa ana mudu majukumu yake vizuri kwa sababu mtoto wake hasumbui na mwanangu mdogo ana miaka 5

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
Yeah mtoto akiwa mkubwa hakuna tatizo kwaku anakua anacheza mama anafanya kazi huyu ni mdogo ambapo muda mwingi anahitaji kuwa na mamake
 
Aisee kuwa na msichana wa kazi mwenye mtoto wakati na wewe una watoto tena watatu mbona ngumu sana, bora huyo wake angekuwa mkubwa mkubwa sasa na wake bado mdogo na mbaya zaid ni wakulia, kazi zinafanyika kweli hapo nyumbani? watoto wako hasa huyo mdogo anaangaliwa inavyotakiwa hasa unapokuwa haupo?

Wewe unaweza usione lakini kwa watoto wako haijakaa vizuri, hapana kwa kweli tafuta msichana asie na mtoto bwana hata kama anae basi awe radhi kumuacha huko kwao, wapo ma agent wanakuletea msichana mpaka kwako 0762 529857 mpigie huyo kaka ana wadada wazuri kabisa
 
Hilo la kuwahudumia yeye na mtoto si tatizo tatizo ni management ya majukumu na mtoto mdogo ambae si kwamba anaenda kucheza no ni mdogo, binti ana 15 alibebeshwa na denti form 3
Pole....

Hapa ndio mtihani zaidi binti ni mdogo anajifunza kulea mwanae na ukitegemea miezi 6 bado anahitaji titi zaidi.

Kama utaweza mvumilia miezi mitatu basi hakika mtoto akiwa na miezi 9 changamoto zitapungua....

Ukishindwa tafuta mwingine au kama unaweza tafuta msichana ambaye atakua anakuja na kuondoka akimsaidiaa huyo wakati mtoto anakua....

Anyway mambo ya malezi wamama ndio mnaelewa struggle zake.
 
Mimi sikushauri kabisa kuwa na housegirl mwenye mtoto.
Hataweza kabisa kufanya kazi kwa ufasaha,japo ukiongea naye mwenyewe kabla hajaanza kazi atakwambia anaweza.
Yaani mtu akishakuwa na mtoto, hata awe mchapakazi vipi! lazima tu Mtoto atamkwamisha.

Tafuta housegirl mwingine ambaye hana mtoto..mabinti wa kazi ni wengi sana aisee.
 
Back
Top Bottom