iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,438
- 14,916
Baada ya utafiti mdogo nilioufanya,nimegundua njia pekee itakayokufanya ukwepe makucha ya wanasiasa hasa pale unaponunua/unapomiliki shamba,ni kuacha kulipima na kupata hati miliki
Nina sababu zifuatazo.
MOJA:
Ukipimisha shamba ukapata hati,unajiweka chini ya kamishna wa Ardhi na Rais ambao watakuwa na mamlaka ya kutengua umiliki wako.
Angalia wale wazee wetu wa vijijini,wanamiliki mapori na mapori lakini umiliki wao hautenguliwi japo hawayaendelezi,kwa sababu hawana hati miliki,wangekuwa na hati miliki tayari wanasiasa wangewachongea,hati zao zikafutwa
MBILI
Ukipima shamba lako na kupata hati miliki,wanakupangia muda wa kumiliki,eti miaka 33,66,99.
Lakini ukiwa huna hati miliki ya shamba lako,umiliki wako ni wa milele,hupangiwi miaka,ni vizazi na vizazi
TATU
Usipopima shamba lako,unakuwa huna adha ya kulipishwa kodi ya shamba kila mwaka.
Ambaye kapima anahenyeshwa na mzigo wa kodi mpaka anakoma
NNE:
Kama shamba lako halijapimwa na mwingine limepimwa,kama serikali ikitaka kuyachukua,wote mnalipwa fidia sawa.
TANO.
Ukipima shamba lako na kupata hati unakuwa na hatari zaidi ya kunyanganywa kuliko ambaye hajapima
SITA
Wachache mno,karibu asilimia sifuri ndio hukopeshwa na mabenki kwa kutumia hati za mashamba
Ukisikia Fulani kafutiwa umiliki wa shamba,ujue iliyofutwa ni hati,ili uwe salama dhidi ya wanasiasa,epuka kupimisha shamba lako,weka mipaka ya asili tu kama miti,katani........