Unataka wanasiasa wasikunyan'ganye shamba lako eti hujaendeleza? Usilipime ukapata hati

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Baada ya utafiti mdogo nilioufanya,nimegundua njia pekee itakayokufanya ukwepe makucha ya wanasiasa hasa pale unaponunua/unapomiliki shamba,ni kuacha kulipima na kupata hati miliki

Nina sababu zifuatazo.

MOJA:
Ukipimisha shamba ukapata hati,unajiweka chini ya kamishna wa Ardhi na Rais ambao watakuwa na mamlaka ya kutengua umiliki wako.

Angalia wale wazee wetu wa vijijini,wanamiliki mapori na mapori lakini umiliki wao hautenguliwi japo hawayaendelezi,kwa sababu hawana hati miliki,wangekuwa na hati miliki tayari wanasiasa wangewachongea,hati zao zikafutwa

MBILI

Ukipima shamba lako na kupata hati miliki,wanakupangia muda wa kumiliki,eti miaka 33,66,99.

Lakini ukiwa huna hati miliki ya shamba lako,umiliki wako ni wa milele,hupangiwi miaka,ni vizazi na vizazi

TATU

Usipopima shamba lako,unakuwa huna adha ya kulipishwa kodi ya shamba kila mwaka.
Ambaye kapima anahenyeshwa na mzigo wa kodi mpaka anakoma

NNE:

Kama shamba lako halijapimwa na mwingine limepimwa,kama serikali ikitaka kuyachukua,wote mnalipwa fidia sawa.

TANO.
Ukipima shamba lako na kupata hati unakuwa na hatari zaidi ya kunyanganywa kuliko ambaye hajapima

SITA

Wachache mno,karibu asilimia sifuri ndio hukopeshwa na mabenki kwa kutumia hati za mashamba

Ukisikia Fulani kafutiwa umiliki wa shamba,ujue iliyofutwa ni hati,ili uwe salama dhidi ya wanasiasa,epuka kupimisha shamba lako,weka mipaka ya asili tu kama miti,katani........
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
iparamasa

Juzijuzi Bakhressa kapewa ma eka kibao, unafikiri yametoka wapi?

Ni hayo hayo ya "wazee wetu" wasio na hati miliki.

Kuna maeneo makubwa yamehodhiwa sehemu kubwa za makazi na hayo ndiyo yenye utata zaidi, watu wanataka kuishi mtu anazuwia eneo kubwa na haliendelezi. Maeneo ya maporini (mbali na makazi ya watu hayana matizo sana).

Na njia rahisi sana ya kuhodhi hata pori liwe kubwa vipi ni kueneza mizinga ya nyuki na kulifanya sehemu ya kufugia nyuki, kuwa na "documents" rasmi zinazoonesha kuwa ni mfugaji wa nyuki na kuwashirikisha mali asili. Hapo hutaguswa.
 
Santi

JF-Expert Member
Oct 30, 2016
529
1,000
Juzijuzi Bakhressa kapewa ma eka kibao, unafikiri yametoka wapi?

Ni hayo hayo ya "wazee wetu" wasio na hati miliki.

Kuna maeneo makubwa yamehodhiwa sehemu kubwa za makazi na hayo ndiyo yenye utata zaidi, watu wanataka kuishi mtu anazuwia eneo kubwa na haliendelezi. Maeneo ya maporini (mbali na makazi ya watu hayana atizo sana).

Na njia rahisi sana ya kuhodhi hata pori liwe kubwa vipi ni kueneza mizinga ya nyuki na kulifanya sehemu ya kufugia nyuki, kuwa na "documents" rasmi zinazoonesha kuwa ni mfugaji wa nyuki na kuwashirikisha mali asili. Hapo hutaguswa.
Ahsante, trick nzuri.
 
esitena tetena

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
1,750
2,000
mkuu,ni kweli unayosema lakini ukiacha shamba lako bila kuliendeleza halafu halijapimwa akija mwekezaji uchwara "anapewa" na uongozi wa kijiji kwa maelezo kuwa ardhi ni mali ya kijiji.
yaani kwa sera ya ardhi iliyopo sasa hivi hakuna pa kukwepea.
kulikuwa na zoezi la hatimiliki za vijiji sijui liliishia wapi.
 
Ndani ya kijiji kuna milk I binafsi za ardhi,mzee fulani ana shamba lake,huwezi kusema ni mali ya kijiji,mama Fulani ana shamba lake,huwezi kusema anamiliki kwa hisani ya kijiji

Ni lake peke yake

Kijiji kama serikali,kinatakiwa kiwe na maeneo yake pekee kwa ajili ya mipango yake ya baadae
 
pandagichiza

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
3,532

Hata kama una hati mwekezaji akitaka shamba lako anapewa we unalipwa fidia tena kwa kupangiwa bei
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Hata kama una hati mwekezaji akitaka shamba lako anapewa we unalipwa fidia tena kwa kupangiwa bei
Lakini huwezi kufutiwa tuu hati jumla jumla,kama alivyofanyiwa sumaye,na shamba likarudishwa serikalini.

Unafidiwa,tatizo fidia wanapanga wenyewe!!
 
esitena tetena

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
1,750
2,000
Ndani ya kijiji kuna milk I binafsi za ardhi,mzee fulani ana shamba lake,huwezi kusema ni mali ya kijiji,mama Fulani ana shamba lake,huwezi kusema anamiliki kwa hisani ya kijiji

Ni lake peke yake

Kijiji kama serikali,kinatakiwa kiwe na maeneo yake pekee kwa ajili ya mipango yake ya baadae
kuna viongozi wengi wa vijiji hawajitambui wala hawaelewi mwisho wa mamlaka yao kuhusu ardhi.ndio maana migogoro ya ardhi ni mingi sana.
 
G.Jacob

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
3,540
2,000
Wanasiasa ni watu wakuwakwepa sana la sivyo wanakuumiz japo haki ni yako
 
Panapet

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
749
500
Baada ya utafiti mdogo nilioufanya,nimegundua njia pekee itakayokufanya ukwepe makucha ya wanasiasa hasa pale unaponunua/unapomiliki shamba,ni kuacha kulipima na kupata hati miliki

Nina sababu zifuatazo.

MOJA:
Ukipimisha shamba ukapata hati,unajiweka chini ya kamishna wa Ardhi na Rais ambao watakuwa na mamlaka ya kutengua umiliki wako.

Angalia wale wazee wetu wa vijijini,wanamiliki mapori na mapori lakini umiliki wao hautenguliwi japo hawayaendelezi,kwa sababu hawana hati miliki,wangekuwa na hati miliki tayari wanasiasa wangewachongea,hati zao zikafutwa

MBILI

Ukipima shamba lako na kupata hati miliki,wanakupangia muda wa kumiliki,eti miaka 33,66,99.

Lakini ukiwa huna hati miliki ya shamba lako,umiliki wako ni wa milele,hupangiwi miaka,ni vizazi na vizazi

TATU

Usipopima shamba lako,unakuwa huna adha ya kulipishwa kodi ya shamba kila mwaka.
Ambaye kapima anahenyeshwa na mzigo wa kodi mpaka anakoma

NNE:

Kama shamba lako halijapimwa na mwingine limepimwa,kama serikali ikitaka kuyachukua,wote mnalipwa fidia sawa.

TANO.
Ukipima shamba lako na kupata hati unakuwa na hatari zaidi ya kunyanganywa kuliko ambaye hajapima

SITA

Wachache mno,karibu asilimia sifuri ndio hukopeshwa na mabenki kwa kutumia hati za mashamba

Ukisikia Fulani kafutiwa umiliki wa shamba,ujue iliyofutwa ni hati,ili uwe salama dhidi ya wanasiasa,epuka kupimisha shamba lako,weka mipaka ya asili tu kama miti,katani........

Hahaha! Tuelekeza shamba lilipo tuje tuluchukue tuliendeleze .
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Hahaha! Tuelekeza shamba lilipo tuje tuluchukue tuliendeleze .
Nimetoa angalizo tu mkuu.

Ukiwa na shamba halina hati lazima wahangaike kujua liko wapi

Kama lina hati,wanavuta droo yenye hati zote za nchi nzima wanakupata na wanajua liko wapi

Au kama wame computerise,wanaingiza jina lako kwenye computer wanalisoma mpaka lilipo

Ni vyema kubaki na kamkataba ka manunuzi tu,shahidi mzee chakubanga
 
Panapet

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
749
500
Nimetoa angalizo tu mkuu.

Ukiwa na shamba halina hati lazima wahangaike kujua liko wapi

Kama lina hati,wanavuta droo yenye hati zote za nchi nzima wanakupata na wanajua liko wapi

Au kama wame computerise,wanaingiza jina lako kwenye computer wanalisoma mpaka lilipo

Ni vyema kubaki na kamkataba ka manunuzi tu,shahidi mzee chakubanga

Unajua ukiliendeleza huna tatizo,lakini likibaki kichaka ndo tabu .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom