Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kuwa tajiri? - Mwongozo kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by GAZETI, Feb 26, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 2,906
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

  Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao. Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!

  Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasa kuwa makini zaidi.

  Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 .

  Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

  Ndugu mwanajamvi, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana.

  Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo.

  ==============

  MAELEZO ZAIDI:

  UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI  SEHEMU YA KWANZA

  UTANGULIZI

  Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu wana JF ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo.

  A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI?

  1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
  2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
  3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
  4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
  5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.

  B.FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.

  Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
  - Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
  - Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
  - Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
  Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
  Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
  Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
  Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
  Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
  Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
  Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku

  C:MAPUNGUFU

  Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.


  D: KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI

  Kuna maelezo ya kusisimua sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
  a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
  b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
  c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
  d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
  Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
  Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

  (i) KUCHI

  Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

  (ii) CHING'WEKWE

  Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
  Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.

  (iii)UMBO LA KATI

  Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
  Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.

  (iv) SINGAMAGAZI

  Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.

  (iiv) MBEYA

  Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49

  (iiiv)PEMBA

  Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42

  (xi) UNGUJA.

  Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.


  SEHEMU YA PILI

  1. MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

  A. MFUMO HURIA
  Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

  FAIDA.
  Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

  HASARA
  Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
  Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
  Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
  Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
  Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
  Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

  UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
  Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
  Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
  Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
  Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.


  B.MFUMO NUSU HURIA
  Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

  FAIDA
  Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.


  C. MFUMO WA NDANI
  Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

  FAIDA
  Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

  HASARA
  Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

  UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
  1. Matandiko yageuzwe kila siku
  2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
  4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.  UTATUZI WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
  Mambo ya kuzingatia:

  Mabanda bora - Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
  Sifa za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
  Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi
  Kuwa makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi bora.


  UTAGAJI WA MAYAI
  Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

  Hakikisha ya fuatayo.
  Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
  Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
  Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

  UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
  Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
  Uatamiaji na uanguaji wa asili

  KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
  Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
  Yasiwe na uchafu yawe masafi
  Yasiwe na nyufa
  Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
  Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
  Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
  Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
  Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

  KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
  Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
  Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
  Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
  Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
  Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

  Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

  PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
  Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.
  Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
  Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

  UTEKELEZAJI WAKE
  Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga
  Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
  Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
  Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
  Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

  MUHIMU
  Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

  JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
  Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

  TAMBUA VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.

  JIFUNZE MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
  Zoezi hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
  Taz.
  Hesabu ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu.
  Mpaka mwisho wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya vifaranga 2520.

  Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo ili ufundishwe zaidi kuhusu mbinu hiyo ya kuzalisha kuku wengi.

  ULEAJI WA VIFARANGA
  NJIA YA KUBUNI
  NJIA YA ASILI
  Njia zote mbili zinafahamika kama huzifahamu tafadhali fuatilia kwa mtaalamu aliye karibu nawe.


  MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.

  A. MAGONJWA.
  Ugonjwa hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi (Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata vijijini.

  Pamoja na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini

  Ndui ya kuku(Fowl pox)
  Mafua ya kuku(Infectious coryza)
  Homa ya matumbo (Cocciodiosis)
  Minyoo na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.

  DALILI ZA KUKU MGONJWA.

  Huzubaa
  Hali chakula/maji vizuri
  Hujitenga na wenzake
  Hujikunyata au kuinama
  Hutetemeka
  Hutembea kwa shida
  Utagaji wa mayai hupungua au hukoma kabisa


  MAGONJWA YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
  Yako mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.

  ATHARI ZA MAGONJWA.
  Hili liko wazi

  Maelezo haya ya magonjwa ni mengi hivyo tuwe wafuatiliaji kwa wataalam.  MATIBABU

  KIDERI - Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa chanjo.
  Ugonjwa huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.

  KUMBUKA
  Mdondo au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
  Mdondo ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine huzunguka na huzungusha vichwa.
  Mdondo unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3

  NDUI YA KUKU
  HOMA YA MATUMBO (Fowly typhoid)
  MAFUA YA KUKU(Infectious coryzya)
  KUHARISHA DAMU(Coccidiosis)
  Minyoo na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k

  Kwa magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini watatusaidia.

  TIBA ZA ASILI
  Kuna madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.

  BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.

  MWAROBAINI - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
  ALOEVERA - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana zaidi namna ya kuandaa dawa hii.

  Hapa nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na kukinga kuku.
  Mwarobaini, Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge, Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili kichaa.

  NAWASHUKURU PIA NAOMBA MWENYE MCHANGO ZAIDI AENDELEE KUONGEZEA TUSIWE WACHOYO WA MAARIFA KIDOGO GAWANA NA MWENZIO
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,225
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa ushauri wako. Umetoa makadrio ya juu sana ambayo katika halisi yasiweze kuwa applicable. I stand 2b corrected.
   
 3. E

  Exav Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13

  Asante sana!
   
 4. markach

  markach Senior Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Gazeti. Nashukuru sana kwa msaada wako.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,558
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  big up mkuu umetoa mchango mzuri sana na hilo wazo ninalo mda mrefu na ss naanza kulifanyia kazi mkuu
   
 6. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,203
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  naona umeignore gharama za kutengeneza banda la hao kuku (250,000 haitoshi)
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,741
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Ahsante. Nahisi nahitaji maelezo zaidi.
  Nitakupm.
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,369
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Asante sana na shukurani kwa muongozo ila kama jamaa alivyogusia kuhusu gharama za banda la hao kuku nalo ni muhimu
   
 9. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kufafanua zaidi initial na recurrent costs ingetusaidia sana.
   
 10. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  asante kwa mchango wako mkuu
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,491
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kumbe watu wengi tunapenda kuwa matajiri kama nanihino wa igunga
   
 12. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu kwa mchanganuo huu, Je wewe umeshaanza kufuga au unaelezea nadharia? Katika uwekezaji au biashara yeyote kuna changamoto zake, kwa hiyo usijekuingia katika uwekezaji au biashara kwa mahesabu haya; mambo yakienda tofauti unaweza kukata tamaa. Unaweza kuona ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi, lakini siyo rahisi kama wengi wamavyofikiria (kwa uzoefu wangu). Nami nilikuwa na mahesabu kama haya nikanunua kuku zaidi ya 35, lakini zilianza changamoto za magonjwa na walibaki wachache sana. Unaweza kusema tumia dawa. Kwa sasa kuku wa kienyeji nimeweka kwa ajili ya matumizi binafsi lakini kwa biashara niliamua kufuga kuku wa nyama (broiler). Nimetoa comment kutokana na uzoefu niliopata lakini wengine wanaweza kuwa na uzoefu wa tofauti na michango zaidi inaweza kutolewa.
   
 13. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 2,906
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Ni kweli unachozungumza lakini nilichokua natoa hapo ni kama dira tu jinsi kuku wanavyoweza kuwa mtaji muhimu. Ujenzi wa banda na mahitaji mengine yanategemea na mahali ulipo, Mtu aliye kijijini au mwenye shamba ana nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.jambo muhimu kuhusu gharama za kujenga banda linategemea zaidi na changamoto za mahali ulipo. Mfano Mtu wa Dar atatakiwa kujenga banda ambalo licha ya kuwaweka kuku katika hali nzuri pia atatakiwa aangalie jinsi ya kuwalinda kuku hao na wezi. Wako ambao watakabiliwa na changamoto za mwewe na kadhalika. Mwisho nimetoa ushauri watu wafanye utafiti zaidi kwani mimi naweza kueleza lakini nikawapoteza kulingana na utofauti wa jiografia ya mahali niliko.
   
 14. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 341
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri mkuu, but naona kama 1m inaweza kuwa ndogo kama utainclude operating costs kwa hiyo project!
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 2,906
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu kwa sasa mimi sio mfugaji lakini nimeshawahi kufuga na kupata faida kubwa sana kutokana na kuku. Ni kweli kuna changamoto za magonjwa lakini kama utapata ushauri kwa mtaalamu wa mifugo aliyeko karibu nawe utagundua wazi kuwa si kitu cha kuogopa. Kwa upande wangu kipindi hicho nilichokuwa mfugaji nilikuwa natumia dawa ya asili, kuna majani ambayo nilikuwa naletewa na mtaalamu mmoja wa tiba za asili ambayo yanatwangwa na kuchanganywa kwenye maji ya kuku amini wanakuwa hawasumbuliwi na magonjwa. Si nia yangu kukuelekeza dawa hiyo kwa ni siku nyingi kidogo zimepita ila ninachokushauri onana na mtaalamu wa Mifugo. Napenda kukufahamisha kuwa mimi nilianza na kuku watano tu lakini ndani ya miaka mitatu nilikuwa mbali sana.
   
 16. freethinker

  freethinker Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mada nzuri,ila hujazungumzia masoko. Kuzalisha ni kitu kimoja mauzo na gharama za uzalishaji ni vitu vya msingi pia kujua.
   
 17. A

  Atukuzwe Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio tatizo la watanzania vitu vya msingi tunaleta utani mwingi, ametoa dira not necessarily ufuge unaweza umuulize other activity, cost analysis, market na mambo mengine, lets be positive once in atime, nashukuru mimi ni mfugaji wa kuku wa mayai ya kizungu ila wa kienyeji nilikuw nao pia wakafa sana nikakata tamaa, labda kama kuna mtu anafahamu dawa za kuwastustain mbali na zile chanjo zao.
   
 18. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 2,906
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Swali zuri na rahisi. Bado tunarudi kulekule kwa waliotangulia inabidi ufanye utafiti wa soko kulingana na eneo ulilopo kwani sina uhakika sana kama kuna maeneo hawapendi nyama ya kuku wa kienyeji katika nchi hii. Nasema sina uhakika kwani nilishawahi kusikia watu fulani hawapendi samaki lakini kuku bado!
   
 19. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 2,906
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Kitu kimoja inabidi ufahamu ndugu yangu, utafika wakati ambao huo mradi itabidi ujiendeshe wenyewe. Usiogope haihitaji sana elimu ya darasani kujua kwamba lazima kuna kiasi fulani cha kuku utalazimika kuwauza ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji. Kama uko Mjini haraka sana rudi kijijini ukaanzishe hako kamradi katakutoa kwani yawezekana ugumu ukatokana na uwepo wako wa Mini. "MWANAFUNZI anatakiwa asikilize,atafakari, achunguze na kudadisi na atoe maoni yake na sababu za maoni hayo.Kisomo ambacho kinamfanya mtu aone tabu kurudi vijijini si kisomo bali ni mapambo. Kupata shahada ni matokeo tu na si msingi wa elimu ya chuo kikuu " Julai 4 1977 Ibrahim Kaduma,Aliyekuwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho mwaka huo. Kaduma pia aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania wakati wa mwalimu nyerere. Chanzo RAIA MWEMA Febr. 2 - 8
   
 20. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,640
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Thanks mkuu umesomeka.
   
Loading...