Unataka kuwa tajiri?(Desa hili hapa)

Hongera Mkuu.
Chukua kanuni hizo zikusaidie kakaako hapa naendelea kuzitumia japo mwingine atasema inakutosha...sijazileta kumaanisha wasomaji ni maskini natamani tufikie lengo kubwa zaidi kila mmoja wetu
 
Sawa Bwana mdogo ,,nimeuchukua nachambua yanayo nifaa.
Chukua kanuni hizo zikusaidie kakaako hapa naendelea kuzitumia japo mwingine atasema inakutosha...sijazileta kumaanisha wasomaji ni maskini natamani tufikie lengo kubwa zaidi kila mmoja wetu
 
Watu wanayafahamu yote hayo na bado ni masikini
Ni ubishi wetu tu kuyaishi haya...tukithubutu hakika kufanikiwa hapa nchini inawezekana sana...na tuna kila linalohitajika.

1. Ardhi ya kutosha na yenye kuzaa

2. Idadi kubwa ya watu (masoko)

3. Upungufu wa taasisi za kijamii ambazo ni fursa kibiashara e.g. shule za kulipia,hospitali za kulipia,huduma binafsi za kuuza maji maeneo kame,

4. Idadi kubwa ya wanyama-mfugo fursa ya nyama,ngozi,kwato,pembe nk

5. Fursa ya misitu ya kupanda inayokua haraka eg. Pines

6. Tuna mito,maziwa,mabwawa na bahari hapa nasemea fursa ya biashara kv za samaki na mazao ya majini kv shells mwani mangrove logs nk

7. Tuna soko la ukanda wa EAC na Kati linatuzunguka hawa hatujawauzia ipasavyo vitu ambavyo hawana hasa tunavyovipata kirahisi ndani ya nchi ambavyo wao hawana na vile vipitavyo bandarini.

8. Tuna uhitaji mkubwa wa nguo nzuri na za bei nafuu hapa tuanzishe 'viwanda' au tailoring marts kusapply nguo za viwango muhimu kuwekeza kwenye kupata maarifa na material nafuu...ni aibu bado watu wetu wanategemea mtumba ilhali viwanda vya ndani vipo ila soko la ndani hawatoshelezi...kwa mfano kiwanda gani Tanzania kinatengeneza chupi za kike au boksa...hata Jean's nasikia tunauza nje au zinaenda nje ndo zirudi...

9. Tuna fursa ya kutumia TEHAMA kujiajiri mfano vijana kuunda kitu kinachofanana na UBER/TAXIFY kwenye sekta ya kilimo.

10. Tuna fursa ya mazao ya porini ambayo mtu anahitaji kibali tu kibali kutumia mfano kukusanya ubuyu na kutengeneza mafuta ya ubuyu na ubuyu wa kula,juisi nk aidha huko mwituni kuna fursa za kufuga vipepeo nk
11. Utalii ktk maeneo ya kitalii ambayo hayajafikiwa sana hasa utalii wa kitamaduni k.v Tukuyu,Uheheni,kule Dodoma kwa akina nyungu ya mawe.

12. Kuna fursa za kuuza souvenirs/vipusa kupitia minada ya kimataifa mtandaoni
13. Kuna fursa ya kukuza muziki pendwa bongo flava ukaimbwa kwa lugha zote pendwa ili tupenye kwenye masoko ya kimataifa kama ilivyo Nigeria nk

14. Fursa za kuuza tofali nyepesi nje ya nchi na ndani baada ya kuzifyatua na kuzipaki kwa viwango vya kimataifa(tofali nyekundu za udongo wa kichuguu zinapatikana kwa wingi sana Tanzania kuliko popote EAC na zinahitajiwa kwenye corporate real estate industry huko Ulaya na Asia)

15. Sekta ya ujenzi inakua kwa kasi...ni nani atakuja na nyumba nafuu sana na zenye ubora ili ateke soko? Mfano milioni 30 ifyatue 3bdrm kali tena self?

16. Je tunaweza kuanzisha huduma za ufundi makanika hasa wa magari ule smart nikaja popote ulipo nika diagnose gari lako na kulipa tiba haraka? 'Mechanic at a go? Au tunaendelea na huu ufundi wa kuloa maoili

# Fursa zipo nyingi sana FOCUS iwe tu FANYA kwa HARAKA na UFANISI kwa sababu hiki ni Kizazi cha 'Papo kwa Papo'
An instant generation....wazee wa instant coffee,instant call,instant internet,instant customer care,instant voting,instant insurance etc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom