Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Kila mtu anaweza kuwa na uelewa (knowledge) mkubwa, na sio lazima awe msomi wa kiwango cha juu. Kuzingatia tabia hizi 10 kunaweza kumfanya mtu yeyote kuwa mwenye uelewa mkubwa
1. Kusoma kila nafasi inaporuhusu - iwe ni gazeti, vitabu au yaliyomo mtandaoni. Epuka kusoma "vitu visivyo na maana" na badala yake zingatia vitu vya kukuelimisha, kukuhabarisha au hata kukuburudisha. Usipitishe siku bila kusoma kitu cha maana.
2. Kiu ya kufahamu kuhusu watu. Si kufahamu kwa minajili ya umbeya bali kwa mfano "flani aliwezaje kufikia mafanikio aliyonayo?"
3. Kufundisha watu wengine. Kadri unavyofundisha watu wengine ndivyo kadri unavyojiimarisha katika mada unayofundisha.
4. Kushiriki mijadala ya maana
5. Kufanya chemshabongo (zipo nyingi tu mtandaoni) lakini pia waweza kufanya na mtu mwingine, anakuuliza maswali/mafumbo
6. Kuangalia vipindi vya runinga vinavyoeleza matukio/vitu muhimu vilivyoifikisha dunia ilipo leo
7. Kutengeneza mtandao wa marafiki wenye ujuzi/utaalam katika mambo mbalimbali (networking)
8. Kujifunza kuhusu vitu vya kumfanya mtu kuwa bora zaidi (self-development)
9. Kutobweteka na uelewa uliopo kichwani hata kama ni mwingi. Uelewa ni chakula cha ubongo. Hakikisha huunyimi ubongo wako mlo wake
10. Kujiamini.
Evarist Chalali Istagram