SoC01 Unataka kusafiri nje kikazi au kufanya biashara? Zingatia yafuatayo;

Stories of Change - 2021 Competition

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Maisha ya ajira nchini yamekuwa magumu lakini tambua Dunia ni kijiji. Ukiwaza kufanya kazi popote Duniani Ni tofauti na mtu anayewaza kufanya kazi popote Tanzania. Wapo watu wamehitimu shahada ya kwanza lakini awajui wanawezaje kuvuka vipi mpaka. Wapo wenye masters lakini ukiwauliza kuhusu kuvuka mpaka awawezi kukupa taratibu za kufuata. Lakini pia wote humu tunamiliki smartphone lakini atujawahi kujielimisha Nini tufanye tuweze kulifikia soko la Dunia.

Naleta kwenu mambo kumi yakuwaongoza kufikia lengo la safari nje hata kwa matembezi tu;
1. Tumia simu yako kuisoma Dunia, jipe muda wa angalau lisaa limoja kusoma nini kimetokea Dunia kiuchumi,kisiasa,kijamii au kimichezo. Kufanya hivi utaulisha ubongo mambo chanya na utagundua Dunia inahitaji Nini.

2. Kwa mwaka weka malengo yakutembea japo nchi moja ya karibu hata kwa kwenda leo na kurudi au kukaa kwa muda flani ukijifunza lakini pia kutembea Mataifa jirani itakujengea nguvu kuhusu mawasiliano, mbadilishano wa fedha, mahitaji ya kijamii na fursa ikiwemo hata mfumo wa biashara.

3. Ili ufanikishe kutembea Taifa jirani tambua lazima uwe na pasipoti yakusafiria ya muda mfupi au muda mrefu. Kwa Sasa pasipoti ni hati ya lazima kuwa nayo na Ni haki ya kikatiba. Kumiliki pasipoti ujenga hari na amasa yakutafuta fursa nje. Fanya ufanyavyo fika ofisi zinazotoa pasipoti ujipatie pasipoti yako utagundua nguvu yake katika kuisabahi Dunia.

4. Tafuta marafiki raia wa kigeni, jiwekee utaratibu wa kuwa na marafiki raia wa kigeni. Waulize kuhusu maisha ya kwao, gharama za kuishi, gharama za hiteli nk. Kupitia njia hii utabaini zipo nchi gharama Ni ndogo kuliko Tanzania.

5. Usiwashirikishe marafiki zako wa kigeni mambo yako ya ndani mfano lengo lako lakutaka kutembea nchini kwao, hoteli uliyofikia au uwezo wako kiuchumi. Aidha, marafiki wa kigeni ambao huna ufahamu zaidi juu yako wasifahamu kwako wala biashara zako maana ni rahisi kukuzunguka na kukupa jeraha la moyo,uchumi,afya nk Kisha wakarejea kwao. Ishi nao kwa kujifunza siyo kuwaruhusu wakufahamu kiundani vinginevyo wewe umemfaham vyakutosha.

6. Uwapo ugenini usijifanya mwenyeji na usijifanye mgeni. Usiwe mwepesi kuuliza njia, usiwe mwepesi kuhoji ilipo hoteli nzuri nk jifunze kutumia Google kupata majibu ya maswali yako. Uliza pale tu unapotaka ufafanuzi wa Jambo ambalo tayari unauelewa flani. Hii itakusaidia kutoangukia mikononi mwa watu wabaya kirahisi.

7. Ukiwa ugenini jitahidi kufahamu ulipo Ubalozi wa nchi yako na Kama nchi hiyo hakuna Ubalozi basi tafuta ubalozi unaosaidia Watanzania. Mfano Sasa hivi Balozi za nchi za afrika mashariki zinasaidia watu bila kubagua taifa. Lakini pia jitahidi kutumia tovuti ya Wizara ya mambo ya nje ukihitaji msaada.

8. Linda Sana pasipoti yako na tembea nayo au nakala yake (Kama nchi husika inaruhusu nakala) popote unapokwenda. Hati yako ya kusafiri Ni mlinzi wako mkubwa na usimwachie mtu akae nayo.

9. Epuka kuzidisha muda uliopewa au kufanya shughuli ambayo haujarusiwa na mamlaka za nchi husika. Ukipuuza utaishia jela au kufukuzwa kwa fedhea na ukirejea bongo wanakunyanganya pasipoti usisafiri Tena. Ila pia inaweza pelekea ukazuiwa kuingia nchi hiyo kwa kipindi flani

10. Endapo umepata fursa hakikisha unawekeza nyumbani, maisha ya ugenini utia aibu usipojipanga. Eneo zuri la kuwekeza Ni kwenye Ardhi,wape ndugu wakununulie ardhi na uipime uwe na hata.

NB: HATA KAMA UTANOGEWA KIASI GANI, USIRUHUSU NAFSI YAKO IKAKUSHAWISHI UPATE URAIA WA NJE......UTATESEKA BAADAYE MAANA WABONGO WENGI MICHONGO YETU NJE NIKUUTAFUTA URAIA WA NJE.

Haya Ni baadhi kwa uzoefu wangu, Mwenye nyongeza karibu
 
Back
Top Bottom