Unataka kupata “job offer” kwa haraka UpWork au Freelancer.com? Here is the secret

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
Peace everybody!

Kama kawaida nipo hapa tena siku ya leo nikikupatia darasa muhimu kabisa litakalokusaidia kupata kazi UpWork au Freelancer.com kwa haraka.

Nafahamu wapo feelancers wengi wamemefungua Account kwenye haya majukwaa lakini kwa kipindi kirefu hawajapata kazi hata moja. Sasa leo nataka nikuonyeshe mambo matano unayoweza kufanya ili kuongeza nafasi yako yakupata kazi.

Kwa kuanza niseme tu.

Kupata kazi kama freelancer si kazi ngumu kama wengi wanavyodhani. Sababu kuu inayofanya Freelancers hawa kushindwa kupata kazi ni uwezo wao wakufahamu nini clients wanataka lakini pia kuwa na Skills zinazohitajika kwa wingi lakini watu hawazipi kipaumbele.

Binafsi kazi ninazozipata ni kazi rahisi tu yeyote yule anaweza kufanya iwapo atakuwa na right mindset.

Na kuthibitisha hili jana nilimpatia mdau mmoja wa hapa JF kazi yangu ya freelancer anisaidie na nimemlipa leo.

Huyu mdau ni smart lakini pia anapenda kujifunza sana kwahiyo nikasema ngoja “nimwonjeshe” ladha ya kuwa freelancer. Nimempa kazi ameikamilisha ndani ya muda mfupi tu.

Yes, kazi ilikuwa ni kufanya transcription. Anasikiliza Audio ya maongezi na anaandika hayo maongezi.

IMG_7209.JPG


Yes hiyo ni screenshot ya WhatsApp baada ya kumaliza kazi.

Hapa niseme kitu.

Kwasababu ninapata gig kubwa nitaendelea kuwapatia baadhi ya kazi wadau wengine wa hapa JF wanisaidie na nitawalipa.

Kwa kawaida natoa kazi ndogo ndogo. Lakini ukiwa vuziri ninaweza kukupatia kubwa na nitakulipa kadiri tutakavyoelewana.

Mfano sasa hivi nipo na kazi kubwa ya ku-record Swahili conversations + transcriptions. Hapa nitahitaji watu wakunisaidia kwenye transcription kadiri nitakavyokuwa na muda mchache na kushindwa kufanya mwenyewe.

Yes man.

Lengo ni kusaidiana lakini at same time tunatengeneza pesa.

Alright. Sasa tuangalie mambo matatu unayoweza kufanya right NOW na kujiongezea nafasi yakupata kazi kama Freelancer.

1 • Jifunze Skills mpya ya muda mfupi yenye demand.

Yes.

Ukitaka upate kazi kwa urahisi kama Freelancer inabidi ubadili mtazamo.

Degree yako ya public relations haiwezi kukusaidia sana.

Dunia sasa hivi inahitaji Skills kama vile Facebook Advertising, Over the Phone Interpreter, Social Media Manager, Virtual Assistant etc.

Hizi Skills ni very easy to learn na zina demand kubwa kwasababu kwa mfano watu wanahitaji facebook kufanya matangazo ya biashara zao all day everyday. Sasa wewe ukiwa na huu ujuzi you will make so much money.

Achana na mawazo mgando degree ya university itakusaidia.

Nop it won’t.

Acha uvitu Jifunze Skill mpya leo. Na nipo hapa kukusaidia. Send me email to makingmoneyonlinetz@gmail.com

2 • Ukiwa unatuma maombi ya kazi (bid) kuwa Mindful.

Yes, baadhi ya watu hawapo vizuri kufahamu namna yakukamata attention ya client.

Sasa kwa dunia hii iliyojaa distractions usipofahamu mbinu zakuwa “sweet” katika kuwasiliana na client basi wengi wataku-ignore.

Hapa kitu cha kufanya inabidi ujitahidi sana kuwasiliana na client katika namna inayokuonyesha wewe ndiye sahihi kwa kazi husika. I have mastered this technique myself.

Pia kitu kingine ukiwa unatuma proposal kuwa mindful je ni freelancers wangapi wameshatuma maombi tayari?

Kwa sababu client mara nyingi hatojisumbua kupitia proposal 30 wakati ameshapata mtu mwenye sifa katika proposal tano za mwanzo zilizotumwa mapema.

Ukiwahi zaidi ni vuzuri sana. Siyo unatuma proposal baada ya siku 5 baada ya client ku-post kazi.

3 • Iwapo uli apply kazi lakini hukupata na client alikujibu kuwa amesha pata mtu endeleza communication ya huyu client. Chances are atakupatia kazi next time.

Ndiyo.

Kumbuka ili uwe Freelancer mzuri inabidi pia uwe unafahamu jinsi yakujenga mahusiano na clients hata kama hawajakupatia kazi.

Usiogope kuwauliza iwapo next time wanaweza kukupatia kazi.

Binafsi hii imenisaidia sana. Baadhi ya kazi zangu nimezipata kwa namna hii.

IMG_5972.JPG


Hiyo ni screenshot ya moja ya client ambaye nili apply kazi lakini alikuwa tayari ameshapata mtu.

Sasa hapo unaona akiwa na project nyingie lazima ataniuliza iwapo ninaweza kufanya. Na huo ndiyo unakuwa mwazo wa kuendelea kupiga Business kwa muda mrefu.

Natumai umenufaika na darasa hili.

Tukutane next time.
 
Back
Top Bottom