Unataka kununua nyumba au kiwanja? Hakikisha haya kisheria usitapeliwe

Asante kwa maelezo mazuri mwanasheria, umedadavua vyema.umesahau kama ni kiwanja kina miti au msingi ambao haujaisha vyote vyapaswa kuainishwa ikiwa ni pamoja na aina na idadi ya miti hiyo.
 
Shukrani sana kwa elimu hii.. wengi wetu huwa hatuzingatii haya mambo.. tuanaishi kwa kuaminiana..
 
IJUE SHERIA,
Mnamo mwaka 2007 mama yangu alinunua kiwanja toka kwa mtu ambaye na yeye alikuwa ameuziwa na mmiliki wa mwanzo. Ilipofika mwaka 2008 yule mmiliki wa mwanzo alirudi na kudai kuwa aliuza eneo lake kimakosa kwani alikuwa amechanganyikiwa hivyo akafungua kesi kudai eneo lake na mama alikuwa amemtumia ndugu yake kununua eneo lile.

Kesi imeendeshwa kwa miaka 10, mwezi uliopita ndio kesi imehitimishwa na mmiliki wa mwanzo ameshinda kesi na mama inabid alirudishe neo lile. Wakati analinunua thamani yake haikufika hata laki 2.5 tshs, ila hv sasa thamani yake ni zaidi ya 5m.

Tunashukuru sana kwa uzi huu mkuu, naaminI wengi tumeelimika na tutakuwa makini ktk masuala ya ununuzi na uuzaji viwanja au nyumba
 
Je, mtu ukipimiwa na kuwekewa bicon si inamaanisha ndio.vipimo sahihi vya eneo lako? na je ukitokea ramani wizarani imekuja tofauti eneo kumega nakumpa mtu barabara apa nani wa kulaumiwa au wakudili naye.
 
Kumbe wanashereria nao ni wajanja. kuna wakili nilimpelekea issue ya kuniamdikia mkataba wa bajaji. mwishoni kabisa akaniandikia ukitokea mgogoro watakaohusika kutatua ni sisi tuliopeana bajaji. Mimi nilifikir ukitokea mgogoro mfano tukaenda mahakamani na yule wakili atakuja kunisaidia
 
ila wasisahauu kuwa kiwanja/shamba au nyumba utakayouziwa bila muhuri au shahidi Mwenyekiti au bila kwenda kwa mtendaji wa mtaa au kata uwezekano wa kutapeliwa Upo juu Sana
Kisheria Mwenyekiti)serikali ya mtaa hana nafasi kwenye mauziano
 
79 Reactions
Reply
Back
Top Bottom