Unataka kumuona mkeo anajifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kumuona mkeo anajifungua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bikra, Jun 10, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni vizuri wanaume kuwaangalia wake zao wakati wa kujifungua iwapo kufanya hivyo kutawapunguzia wake zao maumivu ya kujifungua.Jambo hili litaongeza upendo na mapenzi kwa familia.

  Tendo la kujifungua ni siri kati ya mtoa huduma na anayejifungua, ambaye wakati huo hupatwa na maumivu makali, hivyo mwanaume kumwangalia mke wake kutaondoa usiri huo.

  Wakati mama anapojifungua husema maneno mengi ya uchungu… utasikia akisema sirudii tena…na mengine mengi ambayo huyatoa kutokana na maumivu anayoyapata…mara nyingine utakuta anayemzalisha ni mwanaume na iwapo atakayekuja kumtazama naye ni mwanaume, inakuwa kama kumdhalilisha kwa namna nyingine.

  Tanzania ina uhaba wa vyumba vya kuzalishia (labour rooms), hivyo katika chumba kimoja wanawake zaidi ya mmoja hujifungua kwa wakati mmoja, sasa ikiruhusiwa wanaume kuwaona wake zao wakati huo, watawaona na wake za wengine…katika mazingira hayo si rahisi kumruhusu mume kushuhudia jambo hili.

  Haya wana JF , Je hii imekaaje ?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,299
  Likes Received: 22,084
  Trophy Points: 280
  Yataka moyo.........
  Katoto kanatoka kakijerumani wakati baba ni mzaramo na mama ni mjaruo pyua
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Itapunguza manyanyaso kwa mke toka kwa mume. Its good for Tanzanian men who are always harsh to their wife. Bring it here immediately
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mume kuwepo wakati mke wake anajifungua ni jambo jema kabisa, japo huku kwetu Tz litakuwa jambo jipya. Ni jambo zurikwa sababu linamshirikisha mume maumivu ya mkewe anavyomwona anahangaika kwa utungu. Ni wakati wa kuonesha upendo na "umwili wao mmoja". Mume ataweza kumfariji mkewe. Naye mke atafarijika kumwona mumewe hapo kwenye kitanda cha labour. Halafu wote wawili watampokea mtoto kwa wakati mmoja: tunda la tendo la NDOA, tunda la upendo wao. Ni furaha iliyoje!
   
  Last edited: Jun 10, 2009
Loading...