Unataka kujua yaliyotokea mpaka lowassa kusafishwa soma hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kujua yaliyotokea mpaka lowassa kusafishwa soma hapa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaone, May 10, 2011.

 1. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  “Mkutano kati ya Lowassa na rais ulikuwa mfupi sana. Lowassa alimueleza Bwana Mkubwa (rais Kikwete), jinsi asivyofurahishwa na mwenendo wa Nape hasa jinsi anavyowatuhumu ufisadi. Alimsihi Rais Kikwete kumweleza hilo katibu wake mwenezi, Nape…,” ameeleza mtoa taarifa.

  Kikwete, taarifa zinasema, alimhakikishia Lowassa kuwa “…hakuna lolote litakalotokea,” kauli ambayo imethibitishwa na Mukama katika mazungumzo yake na wahariri.

  “Yule bwana (Lowassa) alimuuliza Kikwete, mnataka kunipa barua kwa kosa lipi? Nimefanya nini? Nini ambacho wewe hukifahamu,” anasema mtoa taarifa wa MwanaHALISI.

  Gazeti hili limejulishwa na vyanzo vyake vya ndani ya serikali kuwa uamuzi wowote utakaochukuliwa na Lowassa, unaweza kuzidisha mgawanyiko ndani ya CCM.

  Mara baada ya Lowassa kukutana na Kikwete, taarifa zinasema mbunge huyo wa Monduli alikutana na kufanya mazungumzo marefu na Peter Kisumo, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya chama hicho.

  Katika mazungumzo yao, Lowassa alionya kuwa CCM kiko hatarini kupasuka kutokana na kauli za Nape na mwenzake John Chiligati juu ya ufisadi na watuhumiwa wake.

  “Huyu bwana anaua chama. Nakuhakikishia mzee Kisumo, hawa watu wakiendelea kunishutumu bila sababu, nitatoka hadharani na kujibu mapigo,” anaeleza mtoa taarifa akimnukuu Lowassa katika mazungumzo yake na Kisumo.

  Naye Kisumo anaripotiwa kumhoji Lowassa, “Mbona ninyi marafiki wawili mnataka kusambaratisha chama?” Naye Lowassa alijibu, “Kheri iwe hivyo…”

  Mwandishi wa gazeti hili alimtafuta Lowassa ili kuthibitisha walichojadili na Kikwete, lakini simu yake iliita bila kupokelewa
  SOURCE MWANAHALISI
   
 2. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  hicho chama kife mara ngapi? kilishakufa hicho katiba tu ndio bado ilikua inawabeba ngoja tuharakishe mchakato wa katiba mpya..
   
 3. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280

  bora kisambaratike ili vyama vingine vipate nafasi. wamezid kuiba rasilimali za taifa.......
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Wacha kisambaratike tu, maana kuwepo kwake ni kero na hujuma kwa kizazi chenye kiu ya maaendeleo kwenye nchi iliyogeuzwa shamba la mavuno kwa watu wachache wenye Harufu ya ubinafsi!!

  Na kife tu hata kesho tuamke tukute hizo taarifa za kifo cha chama cha Magambali!!
   
 5. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Back to my root!!
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  maoni yako mwana magamba..
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hawa mafisadi ndio wanaelekea kukiua hiki chama, maana wakitoswa ni kifo, pia wakisafishwa ni kifo..........yaani hawana pa kutokea, kifo hakikwepeki.
   
 8. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  kama ni kweli ile bendi sasa inaanza kujifia zake.
   
 9. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Ina maana Lowassa hajui makosa yake?
   
 11. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  haaayaaa kaka mamvii toboa tupo nyuma yako..............
   
 12. Ney wa Barca

  Ney wa Barca JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho,na mwisho wao umekaribia
   
 13. f

  frankkarashani Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Lowassa ni nani mpaka Jakaya amgwaye kiasi hicho?
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wavunje hicho chama kimeisha tuchosha na kututia aibu tu wezi Hazina ya serikali wao, Wizi wa maliasili wao na wawekezaji wao feki, wiziwa madini yetu wao na wanasheria wao wabovu kama akina Chenge, Mwanyika( mwanasheria mwenye akili timamu huwezi weka sahihi kwenye mkataba wa kinyonyaji wa miaka 50 kama Buzwagi hata kama unapwe vijisenti vya 1Bilion)
   
 15. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi umeniacha kidogo na hiyo heading yako ...........mpaka Lowasa kusafishwa.Naomba unifungue macho kidogo,kwani baada ya kukutana kwao amesafishwa?Na kasafishwaje?
   
 16. m

  mukwano Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Katavi hapo umelonga hawana pa kutokea pote ni noma!!!!!!!!! Kwenye Halimashauri Umeya, ufisadi noma, mawaziri baraa, maofisini hapakaliki,watu mishahara hakuna sijui ni vipi, haponi mtu hapa!!!!!!!
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kwishney
   
 18. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Akili za wengine changanya na za kwako,Jk kampoteza Nape kwa kuumjaza ujinga kuwa ukisema neno tu na mimi nipo nyuma yako ss Nape kajisahau kuchanganya na akili zake.Na hili kitawaumbua kuwafanyia wananchi mazingaumwe yao ya kujivua gamba na ss nimeamini ya wahenga kuwa "njia ya muongo ni fupi"siku 90 hazijaisha tayari wameaibika!!!
   
 19. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni dhahiri kwamba jk hana uwezo wa kuwachukulia hatua mafisadi.
   
 20. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Its now time for magamba party to be assisted to rest in peace. CDM should launch that assistance and bury it in INDIAN SEA.
   
Loading...