taamu
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 10,158
- 8,044
Ninachofurahia kwenye kauli yako ni kwamba kuna wachawi.hivyo na watenda uchawi wapo hivyo uchawi upo."Waganga" wote wa kienyeji wachawi.
Ninachofurahia kwenye kauli yako ni kwamba kuna wachawi.hivyo na watenda uchawi wapo hivyo uchawi upo."Waganga" wote wa kienyeji wachawi.
Kwahiyo paka anatuzidi stamina ee!?Njia ingine rahisi ni kuchukua tongotongo za paka mweusi, unapaka machoni mwako halafu unaenda kwenye mizunguko yako.
Hapa njiani utawaona wanga, majini, vizuka na vigagula vyoote wanaowanga mchana na hata wale wanaopaa na ungo mchana utawaona ila wewe hawatakuona.
Ila madhara ya dawa hii ni unaweza kupata mshtuko na kuzimia au kupata lolote maana kuna majini wana sura za kutisha sana au maumbile mabaya na ya kutisha.
Thread haijakamilika no research no right to speak unazungumziaje Habari Za kuweka mwiko hali ya kuwa hujawahi kujaribu Nend kaweke mwiko Kisha njoo na mrejeshoSina uhakika, maana nahisi labda mshana jr atakua ameshawaandikia hili, kama ndivyo basi iunganishwe tu maana hakutakua na namna tena.
Miaka hiyo huko vijijini kulikua na masimulizi ya kila aina kuhusiana na mambo mbalimbali. Ilikua ni aina ya elimu kupitia fasihi simulizi.
Leo napenda niongelee hili:
Wachawi ni kundi watu wasumbufu ambao hupenda kufanya mambo yasiyo ya kawaida na yenye kuogofya sana. Sababu zinazopelekea watu kujiunga na makundi ya wachawi ni visasi, udhaifu, upweke, urithi/historia na wakati mwingine kulazimishwa/mateka.
Katika simulizi hizo tulipata kusimuliwa baadhi ya mbinu za kujikinga na wachawi ukiondoa zile mbinu za kiimani/DINI.
Kuna mbinu mbili ambazo tulipata kusimuliwa.
Ya kwanza tuliambiwa ili kujikinga na wachawi, chukua mkaa wa moto ambao umekolea moto pande zote na ni mwekundu hasa na uudumbukize kwenye maji. Ukiudumbukiza kwenye maji utasikia mlio 'chaaa', yaani hapo maji yanazima ule moto na moto unajaribu kuyapasha maji lakini moto ndiyo huishia kuathirika zaidi maana huzimika kabisa.
Moto ukishazimika unatakiwa kuuchukua ule mkaa na kuuweka kichwani wakati wa kulala (chini) ya mto. Hapo mchawi akikujia usiku ataishia kuona moto tu pale kitandani na wewe utalala salama kabisa bila ya kusumbuliwa. Lakini hautafanikiwa kumuona au kumjua mchawi wako.
Mbinu hii ilitumika mpaka kwenye kuvikinga vyakula, kule vijijini ilikua ni jambo la kawaida sana kukuta mtu kaanika unga kwenye mkeka ila katika unga huo unaona donge la mkaa. Hufanya hivyo hata wanapokua wameuhifadhi unga huo kwenye vikapu.
Mbinu ya pili, hii ni rahisi sana na inatisha. Mbinu hii unatakiwa kuchukua mwiko uliosongewa ugali jioni hiyo halafu wakati wa kulala unauchukua mwiko huo bila ya kuuosha na kupanda nao kitandani na kuuweka kichwani. Utakapofika muda wa wachawi kupita 'round' utawaona wote kama walivyo ila na wao watajua kuwa umewaona, hapo ndipo ilipo hatari ya mbinu hii ya pili, maana baada ya kugundua kuwa umewaona (na ni lazima wajue) watakushambulia kichawi ili kukuzuia usitoe siri hiyo na katika mashambulizi yao huwa hawakuui, bali watakufanya u-paralise mwili/viungo au akili au mdomo na utabaki kama ndondocha.
Hiyo mbinu ya kwanza tuliweza kuijaribu ila ndiyo hivyo tena...you can't tell maana hatukuona chochote kile wala haina bifu nao wala ushahidi, kuupata ushaihidi ni kama wachawi hao waliongozana na mtoto katika shughuli zao, ndiyo utasikia mtoto akisema "Usiku tulienda kumroga yule lakini pale kitandani tukakuta moto tu".
Ila hii mbinu ya pili, kwa kweli hakuwahi kutokea 'Mkwawa ' shujaa miongoni mwetu aliyethubutu kuijaribu. Maana kila tulipouliza zaidi ili kujua ukweli tukaishia kupata jibu lile lile kuwa ni HATARI na tusijaribu.
Labda mmoja ajitolee kujaribu ili atuletee mrejesho, otherwise tutaendelea kuamini hivyo.
Mkisikia misemo kazi yenu ni kuirukia na kuanza kuiimba tu bila ha ya kuielewa.Thread haijakamilika no research no right to speak unazungumziaje Habari Za kuweka mwiko hali ya kuwa hujawahi kujaribu Nend kaweke mwiko Kisha njoo na mrejesho
Sio unatuletea vitu nusunusu
Sent using Jamii Forums mobile app
Wazungu wanatushinda vitu vichache tu wanapoona kitu ambacho hawakielewi wanakifanyia research wakiisikia Story wanaifanyia uchunguzi wanakuja na conclusion ya kila jambo dogo na kubwa ki ukweli Kuna chunguzi nyingine zimegharimu maisha ya watu watu wamekua vilema waliopoteza mali na sifa zao lakini mwishowe hawa watu tunawasoma katika vitabu kama malegendary heroes philosophers na majina mengi mazuri sasa mkuu umeleta swala zuuuuuuri kabisa nimelipenda watu wamelipenda lakini halijakamilika kukuambia ufanye uchunguzi nimekosea ?Mkisikia misemo kazi yenu ni kuirukia na kuanza kuiimba tu bila ha ya kuielewa.
unaposema "Nyo nyichechi nyo raiti chu chipiki" hivi unaelewa hata maana ya huo msemo???
Mimi nimeandika kiuwazi kabisa kuwa ni MASIMULIZI, wewe unakuja na mambo ya "nyo richechi" wapi na wapi!!!
Mkuu, hii issue kama utafuatilia vizuri huu mjadala hata mimi nimeomba watu kama wataweza basi wakajaribu halafu watuletee mrejesho. Mimi nimelileta kama Simulizi, maana yake hata mimi limenishinda kulijaribu na kuja na majibu ya kina.Wazungu wanatushinda vitu vichache tu wanapoona kitu ambacho hawakielewi wanakifanyia research wakiisikia Story wanaifanyia uchunguzi wanakuja na conclusion ya kila jambo dogo na kubwa ki ukweli Kuna chunguzi nyingine zimegharimu maisha ya watu watu wamekua vilema waliopoteza mali na sifa zao lakini mwishowe hawa watu tunawasoma katika vitabu kama malegendary heroes philosophers na majina mengi mazuri sasa mkuu umeleta swala zuuuuuuri kabisa nimelipenda watu wamelipenda lakini halijakamilika kukuambia ufanye uchunguzi nimekosea ?
Hapana lazima uwe shujaa mkuu consigliere.
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari ndo hiyoooooKwahiyo paka anatuzidi stamina ee!?
usisahau kuweka na mfupa wa nguruwe chini ya mto nao ni kinga na uvute bangi kabla ya kulalaSimple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
Nimeipenda sana hoja yakoSimple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
umemuwezaUnaona ajabu kutatuliwa marinda?
Mie kama mpemba tu, deki inakula kanda
Hahahahumemuweza
Eeehe ngoja tufukue kaburi, tueleze mwenzetu umeonana nini au wenge tu?😃Nyie jamani acheni... nimejaribu moja kati ya hayo.. kilichonipataaa... sirudii milele!! Kuanzia kesho naanza kwenda kanisani na maombi. THIS IS VERY DANGEROUS!! Jamaa hadanganyi
Sent using Jamii Forums mobile app