Unataka kujikinga dhidi ya Wachawi au unataka Kuwaona?

Mimi leo nimeshindwa kulala tangu saa saba kwa mana huku kimara umeme imekatika mpaka saa kumi na moja hii haujarudi.
Mimi kuna kitu kinakuja naona kama ananizuiya kujitetea hata kwa kipiga kelele..
Nakuwa Na hisia ya kuona vitu kama vidole vya mikono ambavyo vinakuwa katika mfuno kama ushikwavyo mpira wa basketball.
Katikati ya mikono hiyo vinatokea vitu kama nyota au mngao wa vitu vingi vingi au mwanga kama wa kioo. Then ananigeukia na kuninyooshea kidole anayo weak., sasa sijui nini kinakuwa hivi., ikanibidi nirudi jamvini kuisoma hii mada vizuri kwani nilioona nikawa sina muda nayo.,
Swali langu hilo kaa la moto baada ya kulitumia leo kesho tena linatumika au kila siku jipya lina hitajika ..?
Hilo la mkaa wa moto na kwa mujibu wa simulizi unaweza ukautumia kwa wiki nzima au zaidi. Hilo la mauzauza sina utaalamu nalo sana, hilo labda mshana jr na magwiji wengine humu watatusaidia.
Ushauri wangu shikilia Imani, Mungu wako atakusaidia zaidi.
 
Mimi leo nimeshindwa kulala tangu saa saba kwa mana huku kimara umeme imekatika mpaka saa kumi na moja hii haujarudi.
Mimi kuna kitu kinakuja naona kama ananizuiya kujitetea hata kwa kipiga kelele..
Nakuwa Na hisia ya kuona vitu kama vidole vya mikono ambavyo vinakuwa katika mfuno kama ushikwavyo mpira wa basketball.
Katikati ya mikono hiyo vinatokea vitu kama nyota au mngao wa vitu vingi vingi au mwanga kama wa kioo. Then ananigeukia na kuninyooshea kidole anayo weak., sasa sijui nini kinakuwa hivi., ikanibidi nirudi jamvini kuisoma hii mada vizuri kwani nilioona nikawa sina muda nayo.,
Swali langu hilo kaa la moto baada ya kulitumia leo kesho tena linatumika au kila siku jipya lina hitajika ..?

kama kazz Mwamini Mungu wako, soma Neno la Mungu, Omba ulinzi wa Mungu maana ni zaidi ya huo mkaa au mwiko.
 
nimegundua % kubwa ya watu humu wanaogopa wachawi kitu ambacho kina dhihirisha utovu wa imani
 
madaa gani izi juzi nimexhindwa kulala kisa mapaka asa lei natia kitu makaaa ya mimawe sio kaa la moto tena af tuonee sasa....
 
Sina uhakika, maana nahisi labda mshana jr atakua ameshawaandikia hili, kama ndivyo basi iunganishwe tu maana hakutakua na namna tena.

Miaka hiyo huko vijijini kulikua na masimulizi ya kila aina kuhusiana na mambo mbalimbali. Ilikua ni aina ya elimu kupitia fasihi simulizi.

Leo napenda niongelee hili:

Wachawi ni kundi watu wasumbufu ambao hupenda kufanya mambo yasiyo ya kawaida na yenye kuogofya sana. Sababu zinazopelekea watu kujiunga na makundi ya wachawi ni visasi, udhaifu, upweke, urithi/historia na wakati mwingine kulazimishwa/mateka.

Katika simulizi hizo tulipata kusimuliwa baadhi ya mbinu za kujikinga na wachawi ukiondoa zile mbinu za kiimani/DINI.
Kuna mbinu mbili ambazo tulipata kusimuliwa.

Ya kwanza tuliambiwa ili kujikinga na wachawi, chukua mkaa wa moto ambao umekolea moto pande zote na ni mwekundu hasa na uudumbukize kwenye maji. Ukiudumbukiza kwenye maji utasikia mlio 'chaaa', yaani hapo maji yanazima ule moto na moto unajaribu kuyapasha maji lakini moto ndiyo huishia kuathirika zaidi maana huzimika kabisa.

Moto ukishazimika unatakiwa kuuchukua ule mkaa na kuuweka kichwani wakati wa kulala (chini) ya mto. Hapo mchawi akikujia usiku ataishia kuona moto tu pale kitandani na wewe utalala salama kabisa bila ya kusumbuliwa. Lakini hautafanikiwa kumuona au kumjua mchawi wako.

Mbinu hii ilitumika mpaka kwenye kuvikinga vyakula, kule vijijini ilikua ni jambo la kawaida sana kukuta mtu kaanika unga kwenye mkeka ila katika unga huo unaona donge la mkaa. Hufanya hivyo hata wanapokua wameuhifadhi unga huo kwenye vikapu.

Mbinu ya pili, hii ni rahisi sana na inatisha. Mbinu hii unatakiwa kuchukua mwiko uliosongewa ugali jioni hiyo halafu wakati wa kulala unauchukua mwiko huo bila ya kuuosha na kupanda nao kitandani na kuuweka kichwani. Utakapofika muda wa wachawi kupita 'round' utawaona wote kama walivyo ila na wao watajua kuwa umewaona, hapo ndipo ilipo hatari ya mbinu hii ya pili, maana baada ya kugundua kuwa umewaona (na ni lazima wajue) watakushambulia kichawi ili kukuzuia usitoe siri hiyo na katika mashambulizi yao huwa hawakuui, bali watakufanya u-paralise mwili/viungo au akili au mdomo na utabaki kama ndondocha.

Hiyo mbinu ya kwanza tuliweza kuijaribu ila ndiyo hivyo tena...you can't tell maana hatukuona chochote kile wala haina bifu nao wala ushahidi, kuupata ushaihidi ni kama wachawi hao waliongozana na mtoto katika shughuli zao, ndiyo utasikia mtoto akisema "Usiku tulienda kumroga yule lakini pale kitandani tukakuta moto tu".
Ila hii mbinu ya pili, kwa kweli hakuwahi kutokea 'Mkwawa ' shujaa miongoni mwetu aliyethubutu kuijaribu. Maana kila tulipouliza zaidi ili kujua ukweli tukaishia kupata jibu lile lile kuwa ni HATARI na tusijaribu.

Labda mmoja ajitolee kujaribu ili atuletee mrejesho, otherwise tutaendelea kuamini hivyo.
sasa ni hatar alafu anataka kujaribu
 
hiyo njia 1 hutumiwa na watu weng sana akiwemo mm. Ila ya pili ndio nimeisikia hapa.
Pia kuna kugeuza nguo kuanzia nguo ya ndani mpaka ya nje. Hapa mchawi hakugusi kbsa. Wale wa vijijin km unaenda sehem usiku unageuza nguo zote, mchaw hakugusi hata kidogo
 
Dahumenifumbuamacho
 
Cha msingi mtoa mada fanya uchunguz zaid we lala na mwiko alaf wakizingua tutawasiliana na mshana jr... Ila tutakua tushapata jibu
Mkuu ungejitolea tu. Sasa mnayataka mimi nifanye yote? Yaani nilete mada hapo hapo nikajaribishe? Ungejitolea kujaribisha halafu uje unisimulie ili nilete mada.
 
hiyo njia 1 hutumiwa na watu weng sana akiwemo mm. Ila ya pili ndio nimeisikia hapa.
Pia kuna kugeuza nguo kuanzia nguo ya ndani mpaka ya nje. Hapa mchawi hakugusi kbsa. Wale wa vijijin km unaenda sehem usiku unageuza nguo zote, mchaw hakugusi hata kidogo
Hii ya kugeuza nguo, shuka au godoro ilikua ni kama umeota unamgonga let's say Evelyn Salt or Madame B or Mzigua90 or Beef Lasagna unatakiwa kuamka na kugeuza shuka au godoro halafu na yeye kule alipo naye anakuota unamgonga😆😆
 
Sina uhakika, maana nahisi labda mshana jr atakua ameshawaandikia hili, kama ndivyo basi iunganishwe tu maana hakutakua na namna tena.

Miaka hiyo huko vijijini kulikua na masimulizi ya kila aina kuhusiana na mambo mbalimbali. Ilikua ni aina ya elimu kupitia fasihi simulizi.

Leo napenda niongelee hili:

Wachawi ni kundi watu wasumbufu ambao hupenda kufanya mambo yasiyo ya kawaida na yenye kuogofya sana. Sababu zinazopelekea watu kujiunga na makundi ya wachawi ni visasi, udhaifu, upweke, urithi/historia na wakati mwingine kulazimishwa/mateka.

Katika simulizi hizo tulipata kusimuliwa baadhi ya mbinu za kujikinga na wachawi ukiondoa zile mbinu za kiimani/DINI.
Kuna mbinu mbili ambazo tulipata kusimuliwa.

Ya kwanza tuliambiwa ili kujikinga na wachawi, chukua mkaa wa moto ambao umekolea moto pande zote na ni mwekundu hasa na uudumbukize kwenye maji. Ukiudumbukiza kwenye maji utasikia mlio 'chaaa', yaani hapo maji yanazima ule moto na moto unajaribu kuyapasha maji lakini moto ndiyo huishia kuathirika zaidi maana huzimika kabisa.

Moto ukishazimika unatakiwa kuuchukua ule mkaa na kuuweka kichwani wakati wa kulala (chini) ya mto. Hapo mchawi akikujia usiku ataishia kuona moto tu pale kitandani na wewe utalala salama kabisa bila ya kusumbuliwa. Lakini hautafanikiwa kumuona au kumjua mchawi wako.

Mbinu hii ilitumika mpaka kwenye kuvikinga vyakula, kule vijijini ilikua ni jambo la kawaida sana kukuta mtu kaanika unga kwenye mkeka ila katika unga huo unaona donge la mkaa. Hufanya hivyo hata wanapokua wameuhifadhi unga huo kwenye vikapu.

Mbinu ya pili, hii ni rahisi sana na inatisha. Mbinu hii unatakiwa kuchukua mwiko uliosongewa ugali jioni hiyo halafu wakati wa kulala unauchukua mwiko huo bila ya kuuosha na kupanda nao kitandani na kuuweka kichwani. Utakapofika muda wa wachawi kupita 'round' utawaona wote kama walivyo ila na wao watajua kuwa umewaona, hapo ndipo ilipo hatari ya mbinu hii ya pili, maana baada ya kugundua kuwa umewaona (na ni lazima wajue) watakushambulia kichawi ili kukuzuia usitoe siri hiyo na katika mashambulizi yao huwa hawakuui, bali watakufanya u-paralise mwili/viungo au akili au mdomo na utabaki kama ndondocha.

Hiyo mbinu ya kwanza tuliweza kuijaribu ila ndiyo hivyo tena...you can't tell maana hatukuona chochote kile wala haina bifu nao wala ushahidi, kuupata ushaihidi ni kama wachawi hao waliongozana na mtoto katika shughuli zao, ndiyo utasikia mtoto akisema "Usiku tulienda kumroga yule lakini pale kitandani tukakuta moto tu".
Ila hii mbinu ya pili, kwa kweli hakuwahi kutokea 'Mkwawa ' shujaa miongoni mwetu aliyethubutu kuijaribu. Maana kila tulipouliza zaidi ili kujua ukweli tukaishia kupata jibu lile lile kuwa ni HATARI na tusijaribu.

Labda mmoja ajitolee kujaribu ili atuletee mrejesho, otherwise tutaendelea kuamini hivyo.
Njia ingine rahisi ni kuchukua tongotongo za paka mweusi, unapaka machoni mwako halafu unaenda kwenye mizunguko yako.
Hapa njiani utawaona wanga, majini, vizuka na vigagula vyoote wanaowanga mchana na hata wale wanaopaa na ungo mchana utawaona ila wewe hawatakuona.
Ila madhara ya dawa hii ni unaweza kupata mshtuko na kuzimia au kupata lolote maana kuna majini wana sura za kutisha sana au maumbile mabaya na ya kutisha.
 
Mh...don't try this at home.
 
Back
Top Bottom