Unataka kujikinga dhidi ya Wachawi au unataka Kuwaona?

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Sina uhakika, maana nahisi labda mshana jr atakua ameshawaandikia hili, kama ndivyo basi iunganishwe tu maana hakutakua na namna tena.

Miaka hiyo huko vijijini kulikua na masimulizi ya kila aina kuhusiana na mambo mbalimbali. Ilikua ni aina ya elimu kupitia fasihi simulizi.

Leo napenda niongelee hili:

Wachawi ni kundi watu wasumbufu ambao hupenda kufanya mambo yasiyo ya kawaida na yenye kuogofya sana. Sababu zinazopelekea watu kujiunga na makundi ya wachawi ni visasi, udhaifu, upweke, urithi/historia na wakati mwingine kulazimishwa/mateka.

Katika simulizi hizo tulipata kusimuliwa baadhi ya mbinu za kujikinga na wachawi ukiondoa zile mbinu za kiimani/DINI.
Kuna mbinu mbili ambazo tulipata kusimuliwa.

Ya kwanza tuliambiwa ili kujikinga na wachawi, chukua mkaa wa moto ambao umekolea moto pande zote na ni mwekundu hasa na uudumbukize kwenye maji. Ukiudumbukiza kwenye maji utasikia mlio 'chaaa', yaani hapo maji yanazima ule moto na moto unajaribu kuyapasha maji lakini moto ndiyo huishia kuathirika zaidi maana huzimika kabisa.

Moto ukishazimika unatakiwa kuuchukua ule mkaa na kuuweka kichwani wakati wa kulala (chini) ya mto. Hapo mchawi akikujia usiku ataishia kuona moto tu pale kitandani na wewe utalala salama kabisa bila ya kusumbuliwa. Lakini hautafanikiwa kumuona au kumjua mchawi wako.

Mbinu hii ilitumika mpaka kwenye kuvikinga vyakula, kule vijijini ilikua ni jambo la kawaida sana kukuta mtu kaanika unga kwenye mkeka ila katika unga huo unaona donge la mkaa. Hufanya hivyo hata wanapokua wameuhifadhi unga huo kwenye vikapu.

Mbinu ya pili, hii ni rahisi sana na inatisha. Mbinu hii unatakiwa kuchukua mwiko uliosongewa ugali jioni hiyo halafu wakati wa kulala unauchukua mwiko huo bila ya kuuosha na kupanda nao kitandani na kuuweka kichwani. Utakapofika muda wa wachawi kupita 'round' utawaona wote kama walivyo ila na wao watajua kuwa umewaona, hapo ndipo ilipo hatari ya mbinu hii ya pili, maana baada ya kugundua kuwa umewaona (na ni lazima wajue) watakushambulia kichawi ili kukuzuia usitoe siri hiyo na katika mashambulizi yao huwa hawakuui, bali watakufanya u-paralise mwili/viungo au akili au mdomo na utabaki kama ndondocha.

Hiyo mbinu ya kwanza tuliweza kuijaribu ila ndiyo hivyo tena...you can't tell maana hatukuona chochote kile wala haina bifu nao wala ushahidi, kuupata ushaihidi ni kama wachawi hao waliongozana na mtoto katika shughuli zao, ndiyo utasikia mtoto akisema "Usiku tulienda kumroga yule lakini pale kitandani tukakuta moto tu".
Ila hii mbinu ya pili, kwa kweli hakuwahi kutokea 'Mkwawa ' shujaa miongoni mwetu aliyethubutu kuijaribu. Maana kila tulipouliza zaidi ili kujua ukweli tukaishia kupata jibu lile lile kuwa ni HATARI na tusijaribu.

Labda mmoja ajitolee kujaribu ili atuletee mrejesho, otherwise tutaendelea kuamini hivyo.
 
Simple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
 
!
!
kwa sababu huwa wakihisi umewaona huwa wanakuletea kidole machoni kama wanataka kukutovuga. Ili uwachanganye wewe usifumbe macho ganda tu kama hakuna kitu kujifanya umelala
 
Sasa atarudishaje mrejesho wakati kishapigwa kipapai mkuu?
 
Aisee! Kumbe ndivyo ilivyo.
Kuna jamaa alikuwa anapandisha mashetati Sasa akiona gozigozi watu wamejaa wanataka kumsikia ataongea nini,yeye alikuwa haongei ila anaomba nimwekee kaa la moto kwenye glass yenye maji halafu anayanywa faster na kuiachia glass ivunjike.

Hivi Hili kaa la moto lina maana gani kwenye mambo ya kishirikina?
Nalog off
 
Simple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
Duh...very genious.
Unaweza ukatuletea mrejesho mkuu? Maana nina hamu sana ya kupata mrejesho wa hii kitu ili niujue ukweli.
 
maneno mbofumbofu hayo, wazee walitumia hiyo mbinu 1 ili kuwatoa hofu usiku mkilala msiogope wachawi na mbinu ya 2 imewekwa vitisho na tahadhari ili watu wasijaribu kufanya hivyo msije wakastukia ni uongo
inawezekana mzee mwenzangu maana si unakumbuka ata vile vita vya MAJIMAJI ndugu zetu walidanganywa wakafa wengi ila walishinda
 
Back
Top Bottom