Unataka kujikinga dhidi ya Wachawi au unataka Kuwaona?


Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,569
Likes
12,969
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,569 12,969 280
Sina uhakika, maana nahisi labda mshana jr atakua ameshawaandikia hili, kama ndivyo basi iunganishwe tu maana hakutakua na namna tena.

Miaka hiyo huko vijijini kulikua na masimulizi ya kila aina kuhusiana na mambo mbalimbali. Ilikua ni aina ya elimu kupitia fasihi simulizi.

Leo napenda niongelee hili:

Wachawi ni kundi watu wasumbufu ambao hupenda kufanya mambo yasiyo ya kawaida na yenye kuogofya sana. Sababu zinazopelekea watu kujiunga na makundi ya wachawi ni visasi, udhaifu, upweke, urithi/historia na wakati mwingine kulazimishwa/mateka.

Katika simulizi hizo tulipata kusimuliwa baadhi ya mbinu za kujikinga na wachawi ukiondoa zile mbinu za kiimani/DINI.
Kuna mbinu mbili ambazo tulipata kusimuliwa.

Ya kwanza tuliambiwa ili kujikinga na wachawi, chukua mkaa wa moto ambao umekolea moto pande zote na ni mwekundu hasa na uudumbukize kwenye maji. Ukiudumbukiza kwenye maji utasikia mlio 'chaaa', yaani hapo maji yanazima ule moto na moto unajaribu kuyapasha maji lakini moto ndiyo huishia kuathirika zaidi maana huzimika kabisa.

Moto ukishazimika unatakiwa kuuchukua ule mkaa na kuuweka kichwani wakati wa kulala (chini) ya mto. Hapo mchawi akikujia usiku ataishia kuona moto tu pale kitandani na wewe utalala salama kabisa bila ya kusumbuliwa. Lakini hautafanikiwa kumuona au kumjua mchawi wako.

Mbinu hii ilitumika mpaka kwenye kuvikinga vyakula, kule vijijini ilikua ni jambo la kawaida sana kukuta mtu kaanika unga kwenye mkeka ila katika unga huo unaona donge la mkaa. Hufanya hivyo hata wanapokua wameuhifadhi unga huo kwenye vikapu.

Mbinu ya pili, hii ni rahisi sana na inatisha. Mbinu hii unatakiwa kuchukua mwiko uliosongewa ugali jioni hiyo halafu wakati wa kulala unauchukua mwiko huo bila ya kuuosha na kupanda nao kitandani na kuuweka kichwani. Utakapofika muda wa wachawi kupita 'round' utawaona wote kama walivyo ila na wao watajua kuwa umewaona, hapo ndipo ilipo hatari ya mbinu hii ya pili, maana baada ya kugundua kuwa umewaona (na ni lazima wajue) watakushambulia kichawi ili kukuzuia usitoe siri hiyo na katika mashambulizi yao huwa hawakuui, bali watakufanya u-paralise mwili/viungo au akili au mdomo na utabaki kama ndondocha.

Hiyo mbinu ya kwanza tuliweza kuijaribu ila ndiyo hivyo tena...you can't tell maana hatukuona chochote kile wala haina bifu nao wala ushahidi, kuupata ushaihidi ni kama wachawi hao waliongozana na mtoto katika shughuli zao, ndiyo utasikia mtoto akisema "Usiku tulienda kumroga yule lakini pale kitandani tukakuta moto tu".
Ila hii mbinu ya pili, kwa kweli hakuwahi kutokea 'Mkwawa ' shujaa miongoni mwetu aliyethubutu kuijaribu. Maana kila tulipouliza zaidi ili kujua ukweli tukaishia kupata jibu lile lile kuwa ni HATARI na tusijaribu.

Labda mmoja ajitolee kujaribu ili atuletee mrejesho, otherwise tutaendelea kuamini hivyo.
 
PATIENCE PB

PATIENCE PB

Senior Member
Joined
Apr 3, 2014
Messages
163
Likes
27
Points
45
PATIENCE PB

PATIENCE PB

Senior Member
Joined Apr 3, 2014
163 27 45
Simple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
 
Mlatinoh king

Mlatinoh king

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2015
Messages
4,655
Likes
4,418
Points
280
Mlatinoh king

Mlatinoh king

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2015
4,655 4,418 280
unajua mim sijawahi kuona mchawi iwe kimiujiza au face to face, mpaka najiuliza wanaofatwa na wachawi wanakuwafactor zip?
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,569
Likes
12,969
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,569 12,969 280
unajua mim sijawahi kuona mchawi iwe kimiujiza au face to face, mpaka najiuliza wanaofatwa na wachawi wanakuwafactor zip?
Jaribu hiyo mbinu ya pili mkuu, huenda ikawa ndiyo nafasi ya kuwaona.
 
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
1,507
Likes
900
Points
280
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
1,507 900 280
Ngumu kumeza maana utaandamwa na wachawi kila unakoenda. Nashukuru kunielewesha kwa mkaa kuweka kwenye unga wakati umeanika maana nimeshuhudia nikiwa mdogo nilikuwa sijui kwa nini wanafanya vile.
 
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Messages
13,155
Likes
6,647
Points
280
Age
29
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2011
13,155 6,647 280
mshana jr , MziziMkavu ,Kiranga , Ishmael , jichawi tupeni ukweli hapa
 
Complicator

Complicator

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Messages
1,262
Likes
1,727
Points
280
Complicator

Complicator

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2013
1,262 1,727 280
Simple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
kumbe majiniaz bado mnaishi
 
Chichmoore

Chichmoore

Member
Joined
Jan 30, 2013
Messages
83
Likes
18
Points
15
Chichmoore

Chichmoore

Member
Joined Jan 30, 2013
83 18 15
Zipo pia mbinu za kuweza kuwaona wachawi bila a wao kugundua kama umewaona. Na majini pia ipo hivo.
 
baracuda

baracuda

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Messages
800
Likes
472
Points
80
baracuda

baracuda

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2014
800 472 80
Hizo ni imani za kusadikika..hakuna uchawi ni mbwembwe, vitisho na imani potofu..
 
amoneyazan

amoneyazan

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2013
Messages
666
Likes
338
Points
80
amoneyazan

amoneyazan

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2013
666 338 80
Simple_unalala na kaa la moto kama ulivyosema pia unalala na mwiko I,e unawaona na hata wao wanakuona ila wakitaka kuja kukudhuru ili usitoe siri wanakuta moto tu coz umelala na mkaa....hapo je mkuu...?
Umetishaa mkuu
 
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Messages
5,511
Likes
2,630
Points
280
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2014
5,511 2,630 280
Ila hio ya mwiko nimeisikia pia
 
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Messages
5,511
Likes
2,630
Points
280
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2014
5,511 2,630 280
Nasikia ukipika kuku akibaki ukiwa inahifadhi eka ndani ya maji yaani ile sufuria au bakuli enye mboga idumbikize kwenye chombo chenye maji la sivyo unahatihati ya kula bundi, wachawi wanatabia ya kubadilisha
 
kama kazz

kama kazz

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2015
Messages
1,034
Likes
472
Points
180
kama kazz

kama kazz

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2015
1,034 472 180
Mimi leo nimeshindwa kulala tangu saa saba kwa mana huku kimara umeme imekatika mpaka saa kumi na moja hii haujarudi.
Mimi kuna kitu kinakuja naona kama ananizuiya kujitetea hata kwa kipiga kelele..
Nakuwa Na hisia ya kuona vitu kama vidole vya mikono ambavyo vinakuwa katika mfuno kama ushikwavyo mpira wa basketball.
Katikati ya mikono hiyo vinatokea vitu kama nyota au mngao wa vitu vingi vingi au mwanga kama wa kioo. Then ananigeukia na kuninyooshea kidole anayo weak., sasa sijui nini kinakuwa hivi., ikanibidi nirudi jamvini kuisoma hii mada vizuri kwani nilioona nikawa sina muda nayo.,
Swali langu hilo kaa la moto baada ya kulitumia leo kesho tena linatumika au kila siku jipya lina hitajika ..?
 

Forum statistics

Threads 1,261,393
Members 485,163
Posts 30,088,818