Unataka kufika mbali? Tafuta mshauri (Mentor)

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,440
2,692
Umelelewa na wazazi/ walezi na wakakusimamia vema, wakakusomesha mpaka hapo ulipofikia hatakama ni pa dogo, ila wamekuwa ni sehemu ya wewe kupata mwanga na kutokeza katika hatua ya kwanza kimaisha.

Kwa muda huo ulikuwa na washauri na watu wa kukuonya juu ya nini ufanye na nini usifanye ili kufikia malengo yako kwa wakati huo.

Waalimu, wazazi na viongozi wa dini kwa namna moja au nyingine wamekuwa washauri wako (Mentors) na wamekusaidia mpaka wewe kufika hatua hiyo ya kuimaliza stage ya mwanzo katika maisha yako.

Unaweza usione msaada wao moja kwa moja labda kwakuwa uliona kama ni jukumu lao kukulea hivyo hukulitazamia katika jicho lingine kuona kuwa ni watu waliokuwa wanakutengenezea njia ya wewe kuimaliza stage ya kwanza vema.

Baada ya kuimaliza hatua ya kwanza sasa unaanza kujitegemea na unapambana ili kufikia malengo yako wewe.

Hii sasa ni hatua nyingine na ni kama mtoto anayeanza darasa jipya ambalo hajawahi kupitia. Hatua hii wengi huwa wanasahau kuwa peke yao hawawezi faulu mitihani ya hili darasa (kufanikiwa kimaisha), hivyo wanashindwa kuelewa kuwa lazima wapate mwalimu ambaye atatoa muongozo ili kufanikiwa katika darasa hili.

Hatua hii ni hatua ngumu iliyobeba changamoto za kila aina na wala haijali sana kuhusu kile ulichotoka nacho katika stage ya kwanza. Na kila aina ya Changamoto katika hatua hii ni WEWE ndiye wa kuwajibika kwa asilimia mia. Kiukweli ni hatua ngumu sana na yenye kuchanganya wengi mpaka kufanya wengine kufanya maamuzi ambayo yatawaumiza mpaka siku wanatoka duniani.

NINI UFANYE ILI KUIMALIZA HATUA HII YA PILI VEMA?

Kumbuka kama ilivyo katika hatua ya kwanza, vivyohivyp hatua hii ya pili lazima upate waalimu na washauri wenye uzoefu wa kutosha na wenye uwezo wa kuona zaidi ya uonavyo wewe.

Jambo la kufurahisha ni kwamba waalimu katika hatua hii ya pili unaweza ukawa umewazidi mbali sana katika hatua ya kwanza yaani kielimu, kiuchumi na mengine pia, ila utofauti wake ni uwezo halisi wa kuona na kutambua vema jinsi maisha yalivyo katika hatua hii ya pili (Hatua ya upambanaji ili kutoboa katika maisha).

Hatua hii ya pili unahitaji waalimu wengi na wenye uzoefu na waliofanya mambo yakaonekana tofauti na hatua ya kwanza.

Kwa kifupi:

1. Huwezi fanikiwa bila kuwa na mshauri au anaweza julikana kama mtoa muongozo (maana halisi ya connection).

2. Utahitaji mtu ambaye unaweza kumuelezea kila kitu kuhusu maisha yako ili kupata muongozo sahihi na mtu huyu umwamini na uwe huru naye kiasi kwamba ukiwa naye kusiwe na haja ya wewe kujifanya kuwa katika hali fulani ili kuficha uhalisia wako. (Ni ngumu kumpata ila wapo).

Mtu yeyote aliyefanikiawa katika maisha ukimuuliza kafikaje hapo ni lazima atakutajia mtu fulani mbaye ndiye aliyekuwa daraja la yeye kufika hapo alipo.

Hata kwako wewe unayesoma makala hii, tambua kuna mtu mmoja tu unamuhitaji ili wewe kufikia malengo yako, yaani kuna mmoja wa kukufungulia njia ili wewe kutoboa, na naomba kukumbusha, utapata kuendana na imani yako, wewe kama unaamini ili utoboe unahitaji nguvu za giza basi utapata mwalimu mzuri sana aliyetoboa kupitia njia hiyo na kama unaamini kutoboa kwako kimaisha ni Mungu wa kweli ndiye atakayekuwezesha basi utaletewa kulingana na imani yako.

Kila kitu katika ulimwengu huu kinafanya kazi kwa utaratibu au sheria maalum.

Tafuta wa kukutambulisha ili ufunguliwe mlango.
 
Excellent piece of advice. When people finish their exams and graduate from school, huwa wanadhani ndiyo mwisho wa hustling na kujibidiisha. Nay! Watu wakianza kuingia majukumuni maishani ndipo hasa hutambua wameanza kufanya real exam. A point to note: Most people get advice --- but they simply end up on a dead end because they get it from wrong people.
 
Excellent piece of advice. When people finish their exams and graduate from school, huwa wanadhani ndiyo mwisho wa hustling na kujibidiisha. Nay! Watu wakianza kuingia majukumuni maishani ndipo hasa hutambua wameanza kufanya real exam. A point to note: Most people get advice --- but they simply end up on a dead end because they get it from wrong people.
Ni kweli mkuu. Katika kila hatua kuna mambo mapya unakutana nayo, hivyo ni lazima kubadilika.
 
Ni kweli mkuu. Katika kila hatua kuna mambo mapya unakutana nayo, hivyo ni lazima kubadilika
Na ndiyo problem ya watu wasiopiga hatua miaka nenda rudi. They never change. Hata duara la watu wao waliowashauri 3 ama ^foo^ years ago, bado ni lilelile, halijabadilika -- bado wangali ^wapo!^ Mbinu walizotumia enzi za JK ndizo wanategemea ziwakwamue kipindi hiki cha kasi na uzalendo wa Mr No Nonsense! How in the world does that even come come!?

(Hiyo hata inakuja kujeje, ulimwenguni, kimfano!???) People must, on a daily basis, examine & prune out & trim & decimate their circle of unnecessary friends & advisors just the way we prune our flowered-fences na tunavyofanya upenuaji wa mimea shambani (plant spacing) -- to give them shape, appearance and more importantly, health.
 
--- but they simply end up on a dead end because they get it from wrong people.
Hii ni tatizo kuu. Mfano unataka kufanya biashara na unakwenda kuomba ushauri kutoka kwa mshkaji wako ambae hajawahi hata kufanya biashara ya kuuza nyanya
 
Back
Top Bottom