Unataka kufanikiwa katika Maisha? Acha kufanya mambo haya

Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,364
35,005
Mambo ni rahisi sana kwa uhakika kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwa kile unachokifanya. Haya ni mambo ambayo kama unataka mafanikio ni lazima uyaache mara moja.

1. Kupuuzia Mambo
Hapa tunazungumzia kupuuzia mambo ya msingi au matatizo au ishu ambazo ni za aibu unazotamani kujificha chini ya uvungu wa kitanda.

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema tabia mbaya huendelea kukua na kuongezeka kulingana na umri. Kwa bahati mbaya kuna watu hawawezi kasi ya maisha ya sasa na hivyo kushindwa kushughulikia matatizo yanayoambatana nayo kwa kuyapuuza na kufikiri kwamba yataisha yenyewe.

Kwa sasa huwezi ukapuuzia nguvu ya teknolojia na ukafikiri kwamba unaweza kufanikiwa zaidi ya hapo bila kuwekea mkazo teknolojia iliyopo sokoni. Na kama una tabia mbaya wala huishughulikii haitakufanikisha bali itakuyumbisha na kukuondolea mafanikio yako kabisa.

2. Kuwa na wivu
Watu ambao hawana mafanikio ni wenye wivu mkubwa sana na mara nyingi huwa hawafurahii wengine wakifanikiwa hivyo hushindwa kuchukua wajibu wao wa kushindwa kuweka juhudi katika wanalolifanya kwenye maisha yao. Watu wenye wivu hutafuta namna ya kuwashusha wenzao waliofanikiwa na wakati mwingine huwa sababu ya kuwekea vikwazo wenzao ili wasiweze kufanikiwa.

3. Wivu husababisha uchungu
Watu wenye wivu hutengeneza uchungu fulani dhidi ya yule aliyefanikiwa. Watu wengi ambao hawajafanikiwa kimaisha / kitaaluma na hata kibiashara huweka hasira kwa mtu mwingine badala kushughulikia maisha yake au taaluma yake mwenyewe. Kutokana na hali hiyo mtu huyo huwa hawezi kutoa ushirikiano kwa wengine, na ni moja ya watu ambao huwa wako tayari kumharibia mwenzake kazi au biashara kutokana na hali hiyo.

4. Uvivu na kutojituma
Kutokana na kuwa na wivu na uchungu kwa wengine watu ambao hawajafanikiwa huona shida kufanya kazi na wengine hivyo huwa wavivu na kuacha kujihusisha kwa juhudi kwenye kazi kama wengine ili tu asione watu wakisogea au kufanikiwa. Hufanya kazi kwa taratibu sana kiasi kwamba matokeo au muda uliotarajiwa kukamilisha kazi hushindwa kufikiwa mapema.

5. Kupenda kujificha wakati wa kazi
Watu ambao hawajafanikiwa kifikra na kwenye maisha wanakuwa na tabia ya kukimbia au kujificha ili wasipewe majukumu au kuongezewa majukumu.

Hii unaweza kuwa ulishakutana na watu ambao wanatumwa kufanya kazi sehemu fulani na kwa bahati nzuri kazi hiyo ikafanikiwa kuisha mapema, watakachokifanya ni kusema kwamba bado wanaendelea na kazi ili isijulikane kwamba kazi imekwisha ili waweze kwenda kumhudumia mteja mwingine.

8. Kutia aibu watu wengine
Kwa sababu hawa watu wanakuwa hawajiamini hivyo wanachofanya ni kujaribu kuwaaibisha watu wengine. Hupenda kuwa katikati ya watu wanaofanya sana kazi ili kuweza kuwadhalilisha wale wengine kwa kujaribu kuwachafua au kuwadhalilisha kwamba wana utendaji mbovu. Ukweli wanajaribu kupambana na ukosefu wa kujiamini ndani yao wenyewe.

9. Kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya Kijamii
Hawa watu wanaitwa walevi wa mitandao, kama uliwahi kuona watu ambao muda wote wanatumia kwenye televisheni bila kuchoka. Vile vile na watu ambao hawajafanikiwa na wala hawataweza kufanikiwa wanatumia muda mwingi mwenye mitandao bila kufanya kitu cha maana. Muda wanaotumia kwenye mitandao hawajui kwamba unaingiliana na malengo na utendaji kazi zao kwenye maisha yao binafsi.

10. Usumbufu wa chini chini na Usaliti
Tabia hii inakubidi uweke kichwani mwako wakati mwingine unapohisi kusalitiwa na mtu, je ulishawahi kupitia hali ya kwamba mlikuwa mnajaribu kufanya jambo pamoja halafu jambo limepotea juu juu au kujikuta limefanyika sehemu nyingine kabisa bila ya wewe kujua?

Ukweli watu ambao hawana furaha na hawajafanikiwa hawatapenda kuona umefanikiwa hivyo wakati mwingi watataka kusaliti mipango na miradi yako ili usifikie malengo huku wakija na sababu lukuki kwanini imetokea hivyo.

 
Ni kweli. Tatizo kubwa hasa kwa wengi wetu ni kukosa jadi ya kuweka akiba, kujifunza ujasiriamali, kuendekeza starehe na matumizi ya hovyo yasiyo na tija
 
ukiwa na wivu juu ya watu waliofanikiwa katu huwezi fika kokote, kuna wakati nilianza kidevelop hicho kitabia...ila nashukuru niliona ni upuuzi na nikaacha!!
 
umesahu...kuwahi kuamka asubuhi ni muhimu kuliko vyote...
Pia.........kuweka akiba..............kumtanguliza mny'aaz mung'u katika shughul zak'o
 
11) Kuendekeza starehe ya Pombe na Wanawake.
12) kujshughulisha sana na maswala ya Ushirkina
( kuloga wenzio)
13) Kuwa mvivu na tabia ya kuchagua kaz wakat huna hata kaz


nashukuru kwa kuviona hivi pia
 
Kuna jamaa mmoja bana ni anani hate sanaa basi tu hata sijui kwann na hatujawahi kosana or anything....in many things hata mazingira ya kazi hujitahidi na hutumia nguvu nyingi indirectly kuonyesha watu that sifai.

Cha ajabu nimetokea kukubalika mno hasa kwa madem mazingira hayo ya kazi na mambo mengi naambiwa, basi msela inamuuma kweli yan. Kuna mwanamke flan nliwahi chombeza before nikaja nikamuacha ndio dem wa huyo msela sasa hivi.

Sasa sijui jamaa anafeel bado na interest nae or sumthing kumbe nilishafunga kitabu kitambo sanaa. Na wengi pale wame note the cold war between us ila on my side walaaa hata usingizi sikosi. Tha dude feels inferior (wivu mwingi) na hata hivyo hawez nifanya chochote kwa lolote.

Mleta mada u nailed it bruv.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom