Unataka kucheka? Msikilize Lema alivyomtoa jasho wakili kesi ya Ubunge Arusha...

Ama kweli Lema umemuweza wakili, ametaka uongee kama uko kwenye mkutano na wewe ukamwonyesha kuwa huwa mnaanza na "SALAMU"
 
ha ha ha ah ha ah ha ha ha aisee kumbe huyo wakili alishindwa kule singida???ndo maana anapiga kelele kumbe ana machungu ya kukosa ubunge
 
siri ya kuelewa vema kile unachokisoma ni kukijengea picha akilini; zaidi, kama tayari unamjua Lema na haiba yake, hii inachekesha sana tu!
 
There are two kind of lawyer...those who knows the laws and those who knows the judges
 
Kwa kweli nimecheka!! hapo kwenye people's power jamaa alimaliza kazi kabisa, unaweza kuta hata Jaji alijisahau akaitikia japo kwa sauti ya chini!
 
Wakili alimwagwa kwenye kura za maoni singida?hahahahahahahahahahahaha,nimeipenda hiii
 
Wakili analeta siasa mahakamani na mbaya zaidi analeta siasa na mtu aliyemzidi experience katika siasa..
 
Amini usiamini, Wakili Alute Mughwai ni kaka yake Tundu Lissu. Baba moja mama moja. Ninamfahamu Wakili Alute
tangu tuko Ilboru Sec na Tundu Lissu, na hata siku ya Graduation yetu na Tundu, Alute alikuja.

Alute Mungwai, aligombea uteuzi wa ubunge kupitia CCM, Singida mashariki, wakati Tundu akigombea kupitia Chadema.
Mungu alinusuru mpambano wa kaka na mdogo, pale Jonathan Njau alipomshinda Alute na ndipo mechi ikawa Tundu chandema na Njau CCM, ambapo, Njau aliangukia pua.
Polikit somtaimz is very interesting
 
Lol! Kwakeli inachekesha.....Najaribu kupata picha hapo wakili aliposema "Hapana, hapana, hiyo ya peoples' power acha kwa sababu muda hautoshi.....
 
Kwa kweli nimecheka!! hapo kwenye people's power jamaa alimaliza kazi kabisa, unaweza kuta hata Jaji alijisahau akaitikia japo kwa sauti ya chini!

Possible. Lol...
 
Kilichokuchekesha nn sasa?

Well, napenda Lema/cdm washinde kesi hii pale Arusha,,lkn kwa hapa hakuna cha kuchekesha bana!

Kucheka ni hisia.......JK anapokuwa anachekacheka..........kila mara unaweza kueleza kinachomchekeshaga? Na kutoona kichekesho inawezekana hujaelewa context nzima ilivyo...........na aina ya majibu yaliyotolewa........na inawezeka hukucheka maana mmbangi uliouvuta umekukumbusha vifo vya wapendwa wako/wetu akiwemo Mwl.Nyerere....at all kucheka ni hiari.....binafsi nimecheka sana.........aliposema kuwa wakili alishindwa kwenye kura za maoni.........pia aliposema peoples....................malizia kipisi chako cha mwisho ( kwetu tunaita "cha zinde") kisha zimua na Embassy.,,, mmbangi we
 
Back
Top Bottom