Unataka kucheka? Msikilize Lema alivyomtoa jasho wakili kesi ya Ubunge Arusha...

Sijui kama kuna la kuchekesha hapa.
tatizo unaugonjwa mbaya sana wa kusahau...umeshasahau kwamba wewe ni kipofu na kichwa cha panzi usiyeweza kutambua na kuona yanayoendelea...huwezi ona cha kuchekesha kwa kutumia huo ubongo wako wa panzi kaka mwanaasha!!!!
 
tatizo unaugonjwa mbaya sana wa kusahau...umeshasahau kwamba wewe ni kipofu na kichwa cha panzi usiyeweza kutambua na kuona yanayoendelea...huwezi ona cha kuchekesha kwa kutumia huo ubongo wako wa panzi kaka mwanaasha!!!!

Hivi kuna wakuchekesha watu wote kweli labda Charlie Champlin.
 
Hahahaha. . .Poeples Power imenifanyia usiku wangu uwe mzuri. Hamna kesi tena hapo kwahiyo huyo wakili aangalie uwezekano wakuimaliza kabla hajaaibika zaidi.

Lizzy, habari za leo?

Huwa unavinjari na huku????
 
Siasa za Tanzania zimejaa maji taka tu...tunajaza mahakama kwenye kesi zisizo na mbele wala nyuma, badala ya kuhangaikia maendeleo.
 
Labda sipo katika good mood ndo maana sijacheka ila nimegundua jamaa alikuwa anajitetea kijanja na kumchallenge wakili katika njia nyepesi!!!big up lemma!huyu mnyamwezi namkubali gwanda za chama zinavyomkaaga!!!

tatizo huku umepotea njia rudi nyuma kaka/dada..............
 
hii kesi sio nzuri kwa lema lolote linaweza kutokea.ni vyema kuanza maandalizi mapema
 
Elimu ya Mbunge Lema utata mahakamani
Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 14th March 2012


:
ELIMU ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kama ilivyowasilishwa katika Ofisi ya Bunge na maelezo ya ushahidi wake vimeleta utata mkubwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha baada ya kutofautiana.

Utata huo ulijitokeza mahakamani hapo jana mbele ya Jaji Mfawidhi, Gabriel Rwakibarila, wakati Lema ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, akihojiwa na wakili wa wanachama watatu wa CCM, Alute Mungwai.

Katika mahojiano hayo, Lema alianza kwa kudai kuwa alisoma katika shule ya Msingi Kalangalala mkoani Mwanza na kumaliza mwaka 1983 na kwamba alijiunga na Sekondari ya Kolila mkoani Kilimanjaro kidato cha kwanza hadi cha nne na kumaliza mwaka 1993.

Lema, ambaye ubunge wake unapingwa mahakamani hapo, aliendelea kudai kuwa baada ya kumaliza elimu ya sekondari, alisoma kwa njia ya mtandao, Chuo cha Foca cha Zimbabwe na cha Cambridge cha London.

Hata hivyo Wakili Mungwai alimwonesha taarifa ya mtandao ya Chuo cha Cambridge kilichoko Cambridge na si London kama alivyodai mahakamani hapo.

Pia wakili alimwonesha taarifa ya nchi mbalimbali duniani ambazo chuo hicho kina wanafunzi wanaojisomea kwa mtandao, lakini Tanzania hakipo katika taarifa hiyo, hatua ambayo shahidi huyo alikiri.

Wakili Mungwai alimtaka Lema asome taarifa ya wasifu wake iliyopatikana katika mtandao wa Bunge ambapo aliisoma kwa sauti kwamba alisoma elimu ya msingi katika shule ya Kalanga ya Mwanza na elimu ya sekondari alisoma Geita Sekondari mwaka 1989-1991. Mungwai katika mahojiano hayo alimtaka Lema asome katika taarifa ya Bunge tena, inayoonesha elimu yake ya sekondari ya vidato vya tano na sita.

Lema alidai kuwa vidato hivyo alivisoma sekondari ya Kolila wakati katika ushahidi wa mahakamani alidai kusoma vidato vya kwanza hadi vya nne tu katika shule hiyo.

Baada ya mkanganyiko huo kujitokeza, Wakili Mungwai alidai kuwa Lema amelidanganya Bunge na Watanzania wote kwa zaidi ya mwaka kuhusu elimu yake, na kumtaka aseme anachoweza kuieleza Mahakama.

Akijibu hoja hiyo, Lema alidai kuwa Bunge ndilo lililokosea kwa kutoa taarifa za uongo kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini ambaye ni yeye. ''Niligundua juzi kuwa Bunge limenikosea kuhusu taarifa yangu na tayari nimeshaandika barua kwa Katibu wa Bunge kulalamikia hilo,'' [/TD]
[/TR]
 
Mahojiano na wakili

Sehemu ya mahojiano ya wawili hao yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Ulikuja Arusha lini?

Shahidi: Mwaka 2000, nilikuwa nakuja na kurudi.

Wakili: Kati ya mwaka 2000 na 2005 ulikuwa unafanya shughuli gani?

Shahidi: Nilikuwa namiliki daladala, supermarket (duka kubwa) lililokuwa eneo la Mianzini kata ya Kaloleni ikiitwa Bilion Supermarket.

Wakili: Baada ya Kolila ulikwenda wapi?

Shahidi: Nilisoma chuo cha Foca kilichoko Zimbabwe mwaka 2003 hadi 2006.

Wakili: Ulipata cheti? Shahidi: Ndiyo. Advanced Diploma (Stashahada ya Juu). Wakili: Ulihamia Zimbabwe?

Shahidi: Hapana nilisoma kwa mtandao. Wakili: Ulisoma chuo gani tena? Shahidi: Chuo cha Cambridge kilichoko London.

Wakili: Taarifa yangu inanionesha kuwa chuo hicho kiko Cambridge na si London ni kweli? Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Mbona awali ulisema London? Umekosea ama umepotoka?

Shahidi: Nimepotoka.

Wakili: Naomba nikuoneshe taarifa ya mitandao ya nchi mbalimbali duniani ambazo chuo hicho kina wanafunzi ambao wanasoma kwa njia ya mtandao na umwambie Jaji kama Tanzania kuna wanafunzi wake.

Shahidi: Ndiyo, Tanzania hawapo.

Wakili: Ni kweli wewe na wabunge wengine mliwasilisha taarifa zenu binafsi kwa Katibu wa Bunge kama mtawala wa Bunge?

Shahidi: Ndiyo. Wakili:Taarifa zako ni sahihi?

Shahidi: Mimi nilipeleka taarifa zangu sahihi. Wakili: Hebu angalia hii taarifa ya Bunge kuhusu taarifa yako kama Mbunge wa Arusha Mjini, je ni taarifa sahihi?

Shahidi: Ni taarifa sahihi. Wakili: Hiyo taarifa inasemaje juu ya shule ya msingi? Shahidi: Inaonesha Kalanga.

Wakili: Kuna kosa hapo? Shahidi: Ndiyo ni kosa la website (tovuti). Wakili: Soma hapo katika taarifa ya Bunge, elimu ya sekondari ulisoma wapi? Shahidi: Geita Sekondari.

Wakili: Mwaka gani? Shahidi: Mwaka 1989 mpaka 1991.

Wakili: Ni miaka mitatu uliyosoma?

Shahidi: Kwa mujibu wa taarifa hii ya Bunge ni sawa.

Wakili: Kwa mujibu wa taarifa hii ya Bunge vidato vya tano na sita ulisoma Kolila Sekondari, ni sawa?

Shahidi: Ndiyo. Wakili: Lakini kwa ushahidi hapa mahakamani umesema hukusoma Kolila vidato vya tano na sita! Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Umegundua lini kuwa taarifa hii ilikosewa na Bunge?

Shahidi: Juzi. Wakili: Ili ujipange?

Shahidi: Ndiyo na niliandika barua.

Wakili: Kwa mwaka mzima umelidanganya Bunge, umewadanganya Watanzania juu ya taarifa zako!

Shahidi: uongo ni sehem ya maisha ya mwanasiasa,naomba msamaha
 
Siajabu hata Jaji naye ilipotupwa People'ssssssssssss aliitikia Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr kuashiria kuwa na more kes. Kamanda wa vikosi vya ardhini amemvua mama wa watu na uwakili wake nguo mchana kweupe
 
Mahakama zetu zinashushiwa hadhi na majaji makada wa CCM. Kitendo cha jaji Mujuluzi kuhukumu kuwa Lema ana Kesi ya kujibu kwa shinikizo la Magamba limeishusha mahakama na kuigeuza ze-komedi. Hii yote inayoendelea sasa ni matunda ya ukereketwa katika mahakama. Mtu kateuliwa na mwenyekiti wa CCM kuwa jaji anaona payback ni kuonekana anakandamiza upinzani badala ya kufuata taaluma.

Yaani siasa ime-polute kuanzia jeshi la polisi, mahakama, na ilibaki kidogo tu Shimbo nae alipake Shombo ya CCM jeshi la wananchi wa Tanzania katika uchaguzi wa 2010 kwa kutoa kauli ya kutaka wanasiasa wakubali matokeo wakati si kazi yake kwa shinikizo la wanasiasa. Mambo kama haya yanatakiwa kuangaliwa upya katika katiba mpya kama kweli wanaoisimamia wana malengo mazuri na nchi.
 
Back
Top Bottom