Unataka kucheka? Msikilize Lema alivyomtoa jasho wakili kesi ya Ubunge Arusha... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kucheka? Msikilize Lema alivyomtoa jasho wakili kesi ya Ubunge Arusha...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 15, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jamani mie nimecheka hadi mbavu zinaniuma. Lema amenipa Raha sana kwa majibu yake. Hebu soma nawe uongeze siku za kuishi kwa kucheka na kupanua mapafu yako.......

  Lema, wakili ‘wapigana vijembe' mahakamani

  15 March 2012

  Peter Saramba, Arusha | Mwananchi


  VIJEMBE na malumbano kati ya shahidi wa kwanza wa upande wa utete, Godbless Lema na wakili, Alute Mughwai anayewawakilisha wadai katika kesi kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, ni miongoni mwa mambo yaliyotawala ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana.

  Hali hiyo ilimlazimisha Jaji Gabriel Rwakibarila, kuingilia kati mara kwa mara na kutoa muongozo ili kuokoa muda wa mahakama.

  Malumbano hayo yalisababishwa na aina ya maswali kutoka kwa wakili Mughwai na majibu ya Lema ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini na ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu.

  Walalamikaji hao ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaoimba mahakama, kutengua ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitumia maneno ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian.

  Baadhi ya hoja zilizozua malumbano kati ya wakili na shahidi huyo ni pamoja na hatua ya Mughwai kuhoji kama shahidi anajua mila na desturi za kabila la Waarusha (Wamaasai) na Wachagga zinazowabagua wanawake katika nafasi za uongozi wa kimila na zile za kupigiwa kura

  "Mimi siyo kiongozi wa kimila, bali ni kiongozi wa kisiasa na kiserikali, hivyo sijui mila na desturi za uongozi wa kimila za jamii ya Waarusha, Wamaasai na Wachagga. Kwa nafasi yangu ya ubunge mimi ni kiongozi wa makabila yote yaliyoko katika Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo Wanyaturu na wewe (wakili Mughwai),"

  Akijibu swali kuhusu sababu za kutokuwapo kwa mwanamke aliyewahi kuchaguliwa kushika nafasi ya ubunge katika wilaya za jamii ya Waarusha, Lema alidai wengi wamejitokeza kugombea akiwamo mgombea wa Chadema aliyegombea katika Jimbo la Longido lakini hawakuchaguliwa.

  Alisema wanawake hao hakuchaguliwa katika kura za jumla au kura za maoni ndani ya vyama kama ilivyotokea kwa wakili huyo aliyeshindwa kwenye katika kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Singida Mashariki.

  "Baadhi walishindwa kwenye kura za maoni kama wewe ulivyoshindwa kule Singida Mashariki. Wengine walishinda kura za maoni lakini hawakuchaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Dk Burian hapa Arusha," alidai Leman na kufanya wasikilizaji kuangua kicheko.

  Shahidi huyo aliendelea kumrushia maneno wakili Mughwai baada ya kudai kuwa amedanganywa na wateja wake kwa kumweleza kuwa aliomba Dk Burian asichaguliwe kwa sababu siyo mkazi wa Arusha.

  Alidai kuwa kisheria, Mtanzania yeyote ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo lolote bila kujali ukazi wala asili yake ya kuzaliwa.

  "Kwamba nilisema Dk Burian asichaguliwe kwa sababu ni mkazi wa Zanzibar ni hoja ya uwongo na mufilisi, wateja wako wamekudanganya sana kuhusu hilo kwa sababu hoja hiyo isingefanya asichaguliwe ndiyo maana mimi ni mchaga wa Hai, Kilimanjaro lakini nimegombea Arusha na kushinda na leo ni mbunge wako," alidai Lema.

  Kauli ya kudanganywa na wateja wake, ilionekana kumkera wakili Mughwai na kuamua kumuonya kwa mara nyingine sahidi huyo kuacha tabia ya kumpiga misumari kwa kumrushia maneno, badala yake ajibu maswali anayomuuliza.

  "Kwa mara nyingine nakuonya usinipige misumari kwa kunirushia maneno. Wewe jibu maswali yangu," alisema wakili Mughwai.

  Wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida kuwakilisha wadai katika shauri hilo, aliingia kwenye malumbano mengine na Lema alipomzuia kumalizia kukariri maneno yake kuhusu mikopo kwa wanawake, aliyoyatamka katika mikutano yake ya kampeni kitendo kilichomfanya shahidi kukataa kujibu swali lake hadi atakapomaliza kukariri maneno yote.

  Kitendo hicho kilichomfanya Jaji Rwakibarila kuingilia kati na kumruhusu amalizie.

  Lakini alipoanza kukariri maneno hayo, kuhusu taratibu ngumu za mikopo kwa wanawake, wakili Mughwai aliingilia kati na kumtaka ajirejeshe nyuma na kuzungumza kama vile anahutubia mkutano wa hadhara mwaka 2010, kitendo kilichomfanya mbunge huyo kuanza kwa kauli mbiu na salama ya Chadema ya ‘Peoples' huku wasikilizaji wakiitikia power….

  "Hapana, hapana, hiyo ya peoples' power acha kwa sababu muda hautoshi, rudia tu maneno yako kuhusu mikopo kwa akina mama kwa kukariri maneno halisi uliyoyatamka kwenye mikutano yako ya kampeni kuhusu hoja hiyo," alisema wakili Mughwai akimkatisha Lema.

  Awali hoja kuhusu utata juu ya elimu ya mbunge huyo iliibuka baada ya wakili Mughwai kuhoji taarifa zake za elimu zilizopo katika kumbukumbu za nyaraka za bunge, hoja iliyojibiwa na shahidi huyo kuwa imetokana na makosa ya uchapaji uliosababishwa na Bunge lenyewe akidai tayari aliiandikia ofisi ya Bunge kuelezea hilo na kutaka marekebisho.
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyo wakili kumbe ni mwanasiasa mwenzake? Acha wafanye siasa
   
 3. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimependa hiyo ya kujibu pipoz! na watu mahakamani wakajibu, 'pawa'. Huyo wakili ni buege
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kilichokuchekesha nn sasa?

  Well, napenda Lema/cdm washinde kesi hii pale Arusha,,lkn kwa hapa hakuna cha kuchekesha bana!
   
 5. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  Peoplesssssss powerrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 6. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni mbaya sana pale ambapo shahidi anapomzidi maujanja wakili...ni burudani tosha. Wakili kashikwa na hasira ka-loose control ya kuuliza maswali. Kumbe huyu wakili alipigwa chini kwenye uchaguzi? Dah amemuanika vibaya.
   
 7. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hakuna kama mbunge Lema ,magamba bana!
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya pipoz pawaa ni kali.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahaha. . .Poeples Power imenifanyia usiku wangu uwe mzuri. Hamna kesi tena hapo kwahiyo huyo wakili aangalie uwezekano wakuimaliza kabla hajaaibika zaidi.
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Halafu wewe hivi mahitaji mengine ya kimwili unayafanya saa ngapi kama umegoma kulala mpaka this time!!
   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yaani nilipofika hapo jinsi alivyoanza na pipoz ....... nikaangua kicheko kwa nguvu utadhani mchana kumbe usiku wa manane hahahahahahahahaha
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Lol! Lema is a mastermind! Manake kila wakati hasiti kumkumbusha jamaa mie ndo mbunge wako...
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Karibu jukwaaa la siasa! Lol
   
 14. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hahahaaa! Wakili kapata aliyemzidi ujanja. Mawakili aina hii huwa wanatunyanyasa sana kwa maswali hasa anapomtetea mteja (jambazi) wake.
   
 15. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,970
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Nimecheka sana hapo kwenye pipoz ...... power! Yaani Lema alitaka kuanza kumwaga sera za cdm mahakamani? Lol!
   
 16. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inafika mahali mtu unajuta kwa nini ulikubali kuwa wakili wa kesi isiyo na kichwa kama hiyo.
   
 17. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ccm hamuiwezi cdm tena! Kama hamuamini, ngojea hapo arumeru. Ni 'kisu cha kisogo' kwa ccm.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Duuuuuuhhhhhhhhh Lema kaniongezea miaka 1000 mbele ya kuishi.
   
 19. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,171
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  natarajia vituko na aibu kutoka ukonga
   
 20. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hao wakaanga vitumbua sijui watapita wapi
   
Loading...