Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Nov 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama Tuesday, November 17, 2009 10:32 AM
  Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, ameamua kumwaga busara zake kwa kuwashauri wanawake ambao hawajaolewa na wanatafuta wachumba kuwa wasitafute mwanaume kwa kuangalia ana cheo gani au kwa kuangalia akaunti yake ya benki imejaa pesa kiasi gani. Akiongea na jarida la Glamour la Marekani, Michelle Obama alitoa ushauri bora kwa wanawake ambao hajaolewa jinsi ya kumtafuta Mr.Right.

  Katika ushauri wake Michelle Obama alisema kwamba ni vizuri kwa mwanamke anayetafuta mwanaume wa kumuoa kutumia muda mwingi kumfahamu vizuri mwanaume atakayemtongoza badala ya kuangalia zaidi pesa zake na cheo chake.

  Akiongea na jarida hilo Michelle Obama alitoa siri zake kwa wanawake zilizomfanya aweze kumnasa Barack Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

  "Kama unatafuta mapenzi ya kweli, usijali sana akaunti yake ya benki, cheo chake au umaarufu wake" alisema Michelle Obama na kuongeza "Usijali sana mali alizo nazo angalia moyo wake na utu wake".

  "Njia rahisi ya kujua kuwa umempata mwanaume sahihi ni kwa kuangalia jinsi anavyomjali mama yake na anavyowazungumzia wanawake wengine na jinsi anavyoonyesha hisia zake kwa watoto ambao hawafahamu na muhimu kuliko vyote ni jinsi gani anaonyesha kukujali".

  "Na unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za uhusiano na mwanaume, lazima uwe mwenye furaha. Usiendelee kukaa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye hakufanyi uwe mwenye furaha badala yake anakufanya uwe mwenye huzuni wakati wote".

  "Kama utakuwa kwenye uhusiano na mwanaume kama huyo, usikubali kuolewa naye kwani hautokuwa na furaha kwenye ndoa", alimalizia Michelle Obama.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3561018&&Cat=7
   
 2. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hizo sifa za mwanaume bora zote ninazo kama kuna mtu yupo single na anahitaji kuwa na bwana ani Pm tafadhali..
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  acha kudanganya watu wewe
   
 4. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ha! ha! we umefikaje huku tena?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280

  SIO UWONGO, mi mwenyewe ninazo,
  ila wanawake nikiwafuata wananiambia sina mvuto,
  ushamba wangu wa malezi ya kijima nipeleke kijijini kwetu,
  KAZI KWELIKWELI
   
 6. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanawake wa dar hawataki sifa zozote, wanacheki unene wa wallet na uzito wa gari lako
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Duh pole sna kwa nini usitafute anae endana na malezi yako my kaka!! ila utapewa mwema na Mungu achana na hao!!!
   
 8. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haina mbaya hata hii pia ninayo nadhani sina mengi sana ya kusema ngoja nikasome Pm kwanza...
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hehhe hhehe unajipa moyo haha hahha mama we jitahidi lakini huwezi jua!!!
   
 10. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  We sinili kwambia ukalale huku nini sasa hivi kama si kuharibiana shamra shamra za thanksgiving bila sababu!
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Good advice, lakini je inatekelezeka? nakumbuka kuskia kwamba hata yeye amepitia makashkash makubwa na hata huko mwanzo sigara ilimnyima raha, sasa ina maana hakukosa furaha??

  I believe in marriage zilizoandaliwa na mungu kwahiyo kila moja ina majaribu yake, mengine yooote ni majaaliwa yake muumba na si binadamu

  Ndoa haina dummy run!!!
   
Loading...