Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama
  [​IMG]
  Mke wa rais wa Marekani, Michelle ObamaTuesday, November 17, 2009 10:32 AM
  Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, ameamua kumwaga busara zake kwa kuwashauri wanawake ambao hawajaolewa na wanatafuta wachumba kuwa wasitafute mwanaume kwa kuangalia ana cheo gani au kwa kuangalia akaunti yake ya benki imejaa pesa kiasi gani.Akiongea na jarida la Glamour la Marekani, Michelle Obama alitoa ushauri bora kwa wanawake ambao hajaolewa jinsi ya kumtafuta Mr.Right.

  Katika ushauri wake Michelle Obama alisema kwamba ni vizuri kwa mwanamke anayetafuta mwanaume wa kumuoa kutumia muda mwingi kumfahamu vizuri mwanaume atakayemtongoza badala ya kuangalia zaidi pesa zake na cheo chake.

  Akiongea na jarida hilo Michelle Obama alitoa siri zake kwa wanawake zilizomfanya aweze kumnasa Barack Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

  "Kama unatafuta mapenzi ya kweli, usijali sana akaunti yake ya benki, cheo chake au umaarufu wake" alisema Michelle Obama na kuongeza "Usijali sana mali alizo nazo angalia moyo wake na utu wake".

  "Njia rahisi ya kujua kuwa umempata mwanaume sahihi ni kwa kuangalia jinsi anavyomjali mama yake na anavyowazungumzia wanawake wengine na jinsi anavyoonyesha hisia zake kwa watoto ambao hawafahamu na muhimu kuliko vyote ni jinsi gani anaonyesha kukujali".

  "Na unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za uhusiano na mwanaume, lazima uwe mwenye furaha. Usiendelee kukaa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye hakufanyi uwe mwenye furaha badala yake anakufanya uwe mwenye huzuni wakati wote".

  "Kama utakuwa kwenye uhusiano na mwanaume kama huyo, usikubali kuolewa naye kwani hautokuwa na furaha kwenye ndoa", alimalizia Michelle Obama.
   
Loading...