Unasumbuliwa na tatizo la kutodumu na mpenzi mmoja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unasumbuliwa na tatizo la kutodumu na mpenzi mmoja?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Apr 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ni matumaini yangu marafiki mtakuwa mko poa na mnaendelea na majukumu ya kazi za kila siku. Kama kawaida kupitia safu hii tunapata kujifunza yahusuyo mapenzi.
  Ninapoandika makala haya, najaribu kujenga picha kwa vijana wangu wakali kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na

  Judith Wambura ‘Jide’ walipoimba; hakunaga mapenzi yale… kupendana ni zama za kale!... siku hizi kwa kudanganyana, mvulana msichana, ishakuwa poapoa tu.
  Kizazi cha zamani hakikupata shida sana katika hili. Kilisubiri muda muafaka ufike ndipo mtu athubutu kufanya maamuzi ya

  kuingia katika uhusiano ambapo ndani ya muda mfupi basi ndoa ilichukuwa nafasi.
  Kizazi cha sasa hivi, kimetawaliwa na tamaa, vijana wanaingia katika uhusiano wakipelekwa na tamaa za kimwili pasipo kutazama umri na madhara ya kukurupukia mapenzi. Matokeo yake sasa, ndiyo pale

  unapoona vijana wanateseka katika kumpata mke au mume wa maisha.
  Ukweli ni kwamba, tatizo na kutodumu na mpenzi mmoja kwa sasa ni sugu haswa kutokana na mapenzi kuzidiwa nguvu na fedha au hulka ya mmoja wenu.Ilivyo sasa, ni rahisi sana mtu kuachana na mpenzi huyu kuhamia

  kwa yule akitegemea kupata kitu fulani ambacho amekuwa akikikosa kutoka kwa mpenzi wake.
  Ni vema sasa, tukajiuliza nini faida ya huko kuhamahama kwa kila kukicha? Matokeo yake ni nini? Hapo ndipo utagundua kwamba yule unayemfuata ukidhani atakupa suluhu ya tatizo ulilokuwa nalo kwa mpenzi wako wa awali tayari na yeye ameshatendwa sana, moyo wake hauwezi kuwa kwako moja kwa moja.Cha msingi hapa ni

  kufahamu alama za nyakati na kuweza kupambanua mambo ili kuendana na mazingira uliyonayo. Vipengele vifuatavyo vitakusaidia kutambua nini cha kufanya katika ulimwengu huu ambao mapenzi yanaanza kupoteza thamani yake ili kuweza kufikia malengo.

  1. TAZAMANENI VIGEZO


  Kumtazama mpenzi wako inamaana kubwa sana katika uhusiano, haswa kwenye hatua za mwanzoni kabla hujafanya maamuzi kuwa mke au mume. Inakupasa rafiki kutazama aina ya mwanaume au mwanamke utakayemtaka atakuwa sahihi kudumu katika uhusiano kwa muda gani?
  Jiwekee malengo ya karibu kwa kutazama utayari wa mwenzako. Tumia akili yako ya kuzaliwa kuweza kupambanua mambo ambayo hayahitaji elimu ya chuo kikuu.Kabla ya kuanzisha uhusiano mpya tayari utakawa umeshaona mengi siku zilizopita kitu ambacho kitakusaidia kumpima mwenzi wako kama yupo tayari kuanzisha safari mpya ya mapenzi yenye malengo.

  2. USIHARAKIE PENZI

  Marafiki wengi kwa sasa wanapoingia katika uhusiano huwa wanafuata tendo la ndoa tu. Ni bora ukasubiri kwa muda fulani ili uweze kumfahamu mwenziyo anamsimamo gani kabla hujazama ndani ya penzi.
  Tendo la ndoa ni kitu cha mwisho katika mapenzi. Kabla hujafikia kufanya tendo hilo ni vema ukawa tayari umeshapita hatua kadhaa zitakazoweza kukusaidia mwenendo wa tabia za mwenzi wako kabla safari yenu haijaota mizizi.

  3. MUWEKE KARIBU

  Ukaribu katika uhusiano unasaidia sana, hapo itakusaidia kutambua vitu gani mwenzio anafurahi kuvipata kutoka kwako na vipi havipendi. Yawezekana kabisa ukampatia au kumfanyia kitu anachotaka ili iweze kukusaidia mbinu nyingine za kumfanya awe karibu na wewe utamfahamu zaidi.
  Ukaribu huo, utasaidia kumfahamu mpenzi wako kwa vitendo, utampima kama moyo wake ni wa kuridhika ama la! Huwezi kumfahamu mtu wakati muda mwingi unakuwa bize na mambo yako, tenga muda kila wakati uweze kuwa na mpenzi wako ili uweze kupata mambo mengi kutoka kwake.

  4. JIFUNZE TABIA ZAKE

  Unapojifunza tabia za mpenzi wako, ni rahisi udhaifu alionao katika uhusiano. Yawezekana ukabaini kitu ambacho ni rahisi kuweza kumbadilisha tabia zake pasipo hata yeye kujua kama unambadilisha.
  Tabia ya mtu huwa haijifichi hata siku moja, hata kama ataamua kuficha makucha lakini mwisho utakuja gundua. Wengi wanaingia katika mapenzi kwa ajili ya kupata masilahi fulani huwa hawapendi kucheleweshewa hivyo atajitoa mwenyewe kabla hata moyo wako haujazama katika penzi lake.
  5.

  ZUNGUMZENI UKWELI


  Ukweli huwa ndiyo silaha kubwa katika mapenzi. Mmoja wenu akiwa muongo hakika penzi haliwezi kufika mbali. Jaribu kumwambia mpenzi wako ukweli wa hali uliyonayo huku ukitazama mapokezi yake.
  Kwa mtu mwenye mapenzi ya dhati siku zote huamini katika ukweli. Epuka kuongopa, jadilini mambo yenu. Wekeni mikakati ya penzi lenu ili muweze kufikia malengo.Ni vema ‘ukamchana live’ mpenzi wako kwa kumwambia, “najua unajua kama najua sasa kwa nini tudanganyane?” Wakati huo kila mtu ataona ipo haja ya kutulia sababu kama ni ujanja basi wote mmeshapitia nyanja zote hivyo mnapoamua kutulia basi mnatulia kweli.
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  nimefanya yote hayo lakini sikai silencer kabisa
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Namba 3,nimeshindwa kui'bold ila chungu kwangu!
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu kila ukijaribu kujituliza kama kasuku unashtuka umeruka ka kunguru? Utakuwa unaumiza wanawake lakini.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mimi nilishawowa kitambooo......................
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hapa napita tu... kumbe ni kwa wale wanaopigwa vibuti kilasiku!
   
 7. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Thanx kaka, nimekupata
   
 8. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hujui kama una watoto ambao hawajaingia kwenye hiyo taasisi???
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Turuke kama senene.

   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ila heading imekaa kama tangazo la maji marefu, nina dawa ya kumtuliza mpenzi, kumvuta aliye mbali, kung'arisha nyota, kuongeza nguvu n.k.
   
 11. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  duuh mbona mawazo yapo mbali kiasi hicho kongosho?
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  ukweli wabaki kuwa wapenzi wengi ni dalili ya matatizo ya kisaikolojia kwa yule anayehangaikahangaika..........nao....ni kuwa ana mapungufu ambayo adhania atayamaliza kwa kuiburutaburuta na hao wengiwengi..................mwishowe baada ya kutumia nguvu nyingi hubakia kusononeka kuwa hana bao kokote kule...........wengi wa ni wapweke hata kama wamezungukwa na mabucha kibao...........
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  madamex........................vibuti ni shehemu ya kujifunza pia.......................we learn more from rejection than we do from total acceptance........................furahia kibuti kinapokuja, after all life is for those who are fearless of rejection and they keep on trying until they reap the intended rewards.........
   
 14. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hizi software zinaoperate vizuri pale coverage ya network inapokuwa full
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kweli aisee.... sijui kwanini sikai silensa
   
Loading...