Unasoma Chuo, una mkopo na huna malengo jua hatima inakuita

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
To be honest sipendi kuwa mnafiki huwa nasema kweli haswa juu ya suala la maisha nikizingumza kile ninachokiamini bila kutetereka wala kuogopa

Unasoma chuo kikuu na huna malengo ya maisha unatarajia tu kuajiriwa ofisi yenye kiyoyozi jua hatma inakuita

Una mkopo wa asilimia 100 na boom kama lote halaf huna cha maana unachokifanya na huna malengo unachezea tu pesa basi jua hatma inakuita mpendwa

Unasoma hujishughulishi unakula tu bata starehe sikatazi wala sipingi kula ujana sana ila uwe na malengo lakini unapata boom unakula tu starehe jua hatma inakuita!

Hatma ninini?

Hatma ni pale utakapomaliza chuo na boom limekata na ajira hakuna utapata anguko lenye kishindo cha 5g ulichezea pesa sana wewe sasa ni wakati wa kupata ulichokistahili asilimia 15% sijui na ile sijui ile 6% hapo maji utaita mma hatma itakutandika kisawa sawa

Hatma ni pale utakapomaliza utaishia huna hata mia starehe zote na bata zote kwishney hapo huna hili wala lile marafiki wamekukimbia na kukuacha njia panda ya ubungo kwenda mawasiliano

Hatma ni pale utakapomaliza chuo na kurudi kwenu huna chochote cha maana umerudi na na kiduku na cheni shingoni utadhani shule ulienda kusomea ujinga hakika ndo utaijua hatma ninini

Unarudi kwenu huna hili wala lile wazazi wako na ndugu wanaanza kukuchoka na kukuona mzigo hiyo ndo hatma mpendwa

Unarudi mtaani na degree yako hukufanya chochote boom lote la miaka 3 au minne hukufanya cha maana hapa duniani au kitu endelevu mtaa unaanza kukuchoka kikipotea kitu mtaani au tukio wanaanza kukusema huenda ni wewe "sio yule kweli?maana yeye ndo hukaa mtaa huu lazima atakua yeye ndo kaiba"hapo ndo utajua maana hatma ninini

Iogope sana hatma ,hatimaye kwani hii huamua na kuonyesha uliishia wapi, hatma ni hatari kuliko wakati wa sasa

Tengeneza msingi ukiwa chuo ili uweze kuwa na "hatimaye nzuri" badala ya "hatma mbaya"
 
Madogo mkiwa chuo bana mnajionaga nyie ndio wenye mipango mizito/maana na waliopigika huku kitaa ni wajinga wajinga tu hawakujua kupangilia maisha yao.

Hata hivyo mjinga mimi niliyeishia la 7 sijui nachangia nini kwny hii mada ya wasomi wenye maono mazito na mipango kabambe
 
Laki tano kwa miezi miwili unapata laki mbili na nusu kwa mwezi.. ulipie chumba .. ule mara tatu kwa siku... ubadilishe angalau ka t shirt... utoe stationary na vocha.... alafu uniambie unabakiwa na sh ngapi kibongo bongo.
Kwanza usifananishe laki tano ya 2014 na laki tano ya 2020.
 
Wivu tu umekujaa. Kuna mwanachuo alishakudharau au akakwambia wewe sio kitu kwa sababu ni class 7 ? Kuwa na mtazamo chanya ndugu sio kila jambo ni kama unavolichukulia kwenye nafsi yako.

Muache apange mipango afu badaye atakuja kuandika humu. Bila shaka huyo n first year na bado anakaa kwa washikaji zake
 
Wivu tu umekujaa. Kuna mwanachuo alishakudharau au akakwambia wewe sio kitu kwa sababu ni class 7 ? Kuwa na mtazamo chanya ndugu sio kila jambo ni kama unavolichukulia kwenye nafsi yako.
Na kweli mkuu nina wivu sana na nyie wasomi wa vyuo vikuu na mafanikio mliyonayo kwny maisha yenu,Mungu awabariki sana na sisi wa darasa la 7 tutabarikiwa katika shughuli zetu hizi ndogondogo za uchomaji wa mikaa na kuuza al-kasusu.

Barikiwa sana boss.
 
Boom lipi ilo la kutunza kwanza. Hela haitoshi ata kukidhi mahitaji ya kibinadamu. Imagine mtu unatumia laki tano kwa miezi miwili kuishi mjini.
Ni umaskini tu ila sio fedha inayokidhi mahitaji ya mtu.
Kama ingekua inatosha basi watu uko serikalini wangelipwa laki tano na wao.
Kutunza boom Ni uoga wa maisha
 
Na kweli mkuu nina wivu sana na nyie wasomi wa vyuo vikuu,Mungu awabariki sana na sisi wa darasa la 7 tutabarikiwa katika shughuli zetu hizi ndogondogo za uchomaji wa mikaa na kuuza al-kasusu.

Barikiwa sana boss.
Good jaribu kupunguza wivu uwe na wivu wa maendeleo utafute pesa baba.
 
Boom lipi ilo la kutunza kwanza. Hela haitoshi ata kukidhi mahitaji ya kibinadamu. Imagine mtu unatumia laki tano kwa miezi miwili kuishi mjini.
Ni umaskini tu ila sio fedha inayokidhi mahitaji ya mtu.
Kama ingekua inatosha basi watu uko serikalini wangelipwa laki tano na wao.
Kweli kabsa man, na isitoshe kuna baadhi wanasoma vyuo vya private hivyo wanahitaji kujiongezea ada kwa semester ambayo siyo chini ya 250,000 afu mtu anasema et tunanywea pombe
 
We acha tu maisha haya alafu mtu anakuambia boom linafanya hivi linafanya hivi bila kujua watu wana channel zao. Kuna mtu anasave boom na bado anapata mgao kutoka nyumbani sasa kama kwenu ni kwetu unaona ata aibu kupiga simu nyumbani maana unajua utawaonea wazazi.

Back
Top Bottom