Unasikia kuchoka kazi yako? Mambo manne ya kufanya

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
38
61
Kutokuridhika na kazi ni hali ya kujisikia hufikii matarajio yako kikazi. Matarajio yanaweza kuwa kiwango cha mshahara, kujisikia unafanya kazi ndogo kuliko uwezo ulionao, kazi kutokuendana na vipaji ulivyonavyo au hata kutokupata heshima uliyoitarajia.


Kila mtu kwa wakati fulani hujisikia kutokuridhika. Kuna sababu kadhaa. Moja, ni kuwa na matarajio makubwa kuliko uhalisia wa kazi. Lakini la pili, kujilinganisha na watu wasiolingana na kazi unayoifanya. Unapoona wenzako wanafanya kitu tofauti na kile unachokifanya wewe inawezekana ukajisikia kuachwa nyuma hata kama kimsingi pengine unafanya vizuri.

Vyovyote iwavyo, zipo nyakati unaweza kujikuta huridhiki na kazi unayoifanya. Makala haya yanaangazia vichocheo vinne vya kuchoka kazi na hatua za kuchukua unapojikuta katika hali kama hiyo.

Huridhiki na mshahara

Ulipokuwa mwanafunzi uliota ndoto za kufanya kazi yenye mshahara mnono. Uliamini maisha yako yangebadilika ndani ya muda mfupi. Baada ya kupata kazi, unashangaa mambo ni kinyume. Unacholipwa hakilingani na matarajio yako.

Hapa sababu inaweza kuwa kukosa subira. Hakuna mafanikio yanayokuja kwa njia ya mkato kama vijana wa siku hizi wanavyoamini. Mafanikio katika mazingira ya kazi yanafuata hatua fulani. Unahitaji kuwa mvumilivu.

Lakini vile vile huenda kuna maslahi usiyoyaoona. Hata kama mshahara ni mdogo, pengine mwajiri wako anakupa usafiri kwenda na kurudi kazini; amekulipia nyumba; amekuweka mpango wa bima ya afya; anahakikisha unapata chakula cha mchana ukiwa kazini.

Mbali na mshahara huo mdogo, labda mwajiri anakupa fursa ya kwenda masomoni na pia unapata muda wa ziada kufanya mambo mengine. Haya yote unaweza kuona ni madogo lakini ukiyabadilisha kuwa fedha yanaweza kuwa nusu ya mshahara unaoutamani.

Bonyeza hapa kuendelea zaidi.
 
Back
Top Bottom