Unashughulika vipi na mpenzi au mwenza wako ambaye anapenda kukagua simu yako mara kwa mara?

Ndio maana nina kisimu changu cha tochi kwaajili ya kuchezea faulo huko, hakina V.A.R. Akija shemeji yenu nakificha ndani ya viatu au bafuni.

Juzi alikuja halafu nikaingia bafuni kuchat na pisi moja hivi mpya, nimeisave "Covid-19 Pro" yeye nimemsave "WUHAN-VIRUS", si nikajisahau nusu saa ikapita nipo bafuni tu, akaja kunigongea mlango kama tumevamiwa na majambazi au kama ananidai vile, kidogo anitoe roho mpaka simu nusu idondoke kwenye ndoo ya maji kwa jinsi mlango ulivyo bamizwa.

Akaniuliza kwa kufoka "Wewe mwanaume unaingia bafuni saa zima, unaosha nini huko"!!!. Nikamjibu kwa upole "VYOMBO".

Nikazuga naoga zangu, fasta nikatoka, namtafuta kumbe mtu alishasepa muda kweli, nakutana na sms "Asante kwa kuni save Wuhan-Virus". Nikajua simu yangu ya tachi imeshapigwa inspection ya kufa mtu na kibarua kishaota nyasi nshaachika, wala sikumtafuta tena mpaka leo.
😂 😂 😂 😂
 
Mi nilisikia kibao cha mgongo tu (wayaa), sijakaa vizuri ananambia "huyu anaesema amekumisi ni nani" ikabidi nikaushe zangu kimya. akashikwa na mihasira yake, mi nikawa namcheki tu
 
unaanzaje kumpa simu ?mimi juzi nimelala na wife gafla akachukua simu yangu akague nikamwambia ukimaliza kukagua uende nje ukalie huko sitaki makelele humu chumbani
 
Tafuteni hela vijana mtakuwa masikini wa kutupwa shauri yenu halafu utakutakulalama maisha magumu
Gesti 20000/
Hela ya sabuni na nauli 30000
Chakula na vinywaji 30000
Hiyo kwa siku moja sasa piga kwa wiki x2 kwa mwezi sh ngapi umetumia
 
Duuh we jamaa mbabe sana
 
Tafuteni hela vijana mtakuwa masikini wa kutupwa shauri yenu halafu utakutakulalama maisha magumu
Gesti 20000/
Hela ya sabuni na nauli 30000
Chakula na vinywaji 30000
Hiyo kwa siku moja sasa piga kwa wiki x2 kwa mwezi sh ngapi umetumia

Kwani hizo siku zote mnachakatana tu.! Si ukipiga leo labda wiki ijayo Mechi inapigwa uwanja wa Nyumbani (Kwa wasioa) lakini Waliooa wao wanakipiga ugenini na kuachana hapo hapo
 
Uhuru ni muhimu sana alfu ibaki yeye mwenyewe aamue kubaki mwaminifu au achepuke na huwezi mzuia mtu kuchepuka akiamua
Halafu kuchepuka husababishwa na mengi. kuna mtu alishawahi niambia kuwa kwa binadamu, ukimkamata leo anachepuka, unachofanya ni kumuahamisha toka kwa huyu kwenda kwa mwingine
 
Habari za wakati huu wapendwa wanaJF, poleni kwa majukumu mazito ya kuitumikia Nchi yetu na kwa wale ambao mlikuwa na ibada leo hii, Hongereni..! Niende kwenye maada moja kwa moja.!

Mimi ni kijana wa kiume 29, nina mpenzi almost mwaka na miezi mitatu tuko kwenye mahusiano. Dada huyu kipindi cha awali alikuwa na anapenda sana kuchati kuwaita watu majina kama wapenzi na hiyo ilitokana na mimi mwenyewe siku moja kumwomba simu yake na hapo iliingia text ambayo ilinishitua nikaingia inbox . Nilifuatilia zile chats na nilichogundua ni kwamba yeye alikuwa anaita majina hayo bila kujali we una mahusiano au lah...! Labda huenda jamaa alikuwa anakula ....! Sikutaka kuchimba zaidi ya kile nilichokiona..! Tulizungumza na tukaelewana na kweli aliwambia marafiki zake na yeye pia aliachakuita majina hayo. Na baada ya hapo niliamua tu kutojipa pressure isiyo ya lazima nikaacha kushika simu yake na sitashika simu ya mpenzi wangu.!
Ni muda sana hatujatofautiana kwa sababu ya ishuya simu..! Basi leo kaja Ghetto kunisalimia,, Nikawa naangalia TV nayeye yupo namimi basi akaniambia naomba simu yako. Nikampa bila kusita akaniambia toa password (Nikaweka fingerprints ikafunguka).Akaanza kusoma text nilizochati na wadada zote na na akaomba aingie na whatsapp nikamfungulia akaenda. Kasoma text namtizama tu. Katika kusom akakuta text nime toa compliments kwa mdada ambaye honestly namkubali kwa hustle zake na nikamwambia (kwenye text, kwamba siku nikipata nafasi ya kuja Mwanza nitakutafuta nikuone) kesi ikawa kwamba nina mpango wa Kwenda mwanza so niende tu nikaonane naye huyo mtu. SikuongeA na nyingine tena kadada kalikuwa kameweka video ambayo ameitoa Tiktok ambayo ni account yake ...! Nikamsifia Mguu mzuri na pia nikamwambia una shepu na Mguu pia besti na imoji ya kuonyesha napongeza.
Ishu ya kumsifia huyu mdada ikawa kesi, akakomaa kama nimependa miguu yake si nimfuate huyo nayeye nimuache na pia akawa anasema kwahiyo namsifia Mdada kisa yeye ni shapeless (Maneno yake GF wangu) na anamguu mwembamba hauna Nyama..! Kitu ambacho mimi kila mara namsikiaga nikiwa nampiga picha... utasikia “piga kuazia juu hadi magotini chini ukate miguu yangu hii mibaya sitaki ionekane.! “ Na pia ana shepu nzuri namsifiaga mnoo na hips kama zote ila sasa ishu ya kumsifia Mdada wa watu kwamba anamguu mzuri yaani imeibua kesi sana. So nimemwambia sina maana kwamba nataka nimtongoze huyo mdada ila basi tu yeye haniamini dizaini fulani.
So mimi nakuja, tupeane busara na hekima za kushughulika na mpenzi anayekagua simu kiasi cha kukufanya ushindwe kuwa huru.! Tafdhari..! Naomba mnisaidie mawazo na share uzoefu wako kulingana na ishu ya simu au text zilivyoleta ugomvi na mlitatua vipi ???
giphy.gif
Chanzo cha migogoro mingi kwenye mahusiano ni SIMU , kaa nayo mbali simu ya mwenzako ili muishi kwa amani, kuna vitu mpenzi wako anaweza akawa anaandika ila hata hamaanishi kwa kuwa kuna hile hakuna anaeona mazungumzo yangu basi nachat navyojisikia
 
Huyo ni tatizo ana kisirani, cha msingi ni kumwambia ukweli kama ulivyofanya kama hakueliwi ujue hata ukimchukua hatakuelewa na kelele na visirani havitaisha, na utakua mwanzo wa matatizo kwenye nyumba, chukua hatua mapema.
 
Chanzo cha migogoro mingi kwenye mahusiano ni SIMU , kaa nayo mbali simu ya mwenzako ili muishi kwa amani, kuna vitu mpenzi wako anaweza akawa anaandika ila hata hamaanishi kwa kuwa kuna hile hakuna anaeona mazungumzo yangu basi nachat navyojisikia

Mie sishikagi simu yake Ujue!! Niliachaga kuchungulia hiyo simu kuuponya moyo wangu na Maumivu
 
Back
Top Bottom