Unashauri njia gani sahihi kupita kati ya hizi tatu zenye kero?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
Mwendo ni mrefu na inatakiwa upite kila siku njia hiyo hiyo: kutoka Mji (A ) kwenda kula JIJI (B).
Zingatia; (Hairuhusiwi kwenda kwa miguu, pikipiki wala bajaji)

(Njia ya kwanza ni Lami yenye Foleni):
Kutoka sehemu (A) kwenda (B) kuna barabara ya lami, lakini imejaa magari mengi na inafoleni kubwa sana, gari zinasogea taratibu sana kwasababu wenye mamlaka wanatanua na ving'ola kwenda kuchomekea mbele hivyo (Traffic jam) ni kubwa sana!

Njia ya pili ni barabara yenye mashimo na mchanga mwingi lakini haina foleni kabisa ;

Njia hii ya vumbi inapitika lakini inamashimo hatari, madimbwi pia baadhi ya eneo kuna mchanga mwingi sana kiasi kuhitaji gari imara na dereva makini, lakini haina foleni hata kidogo! Inatembea.

Njia ya Anga lakini uwanja wa kupaa na kutua kuna milipuko inayowashwa kwa mitetemo au mawimbi ya ndege (Helkopita)

Njia hii ya anga wanaofanikiwa kuitumia ni wale wenye roho ngumu, wanaoweza kupanda kwenye helicopter kwa kamba na kushuka kwa kamba ndefu umbali 100m!
Kwani Kiwango cha mwisho cha mabomu kujilipua (ignition) ni db inayosikika umbali wa 80M juu ya ardhi!.

Je, njia ipi sahihi kutumia kati ya hizi tatu zinazoelekea sehemu moja?

Itapendeza ukieleza ni kwanini umechagua njia hiyo ili uwasaidie na wenzako kufanya maamuzi?

MJADALA UPO WAZI KARIBUNI
 
Nitahakikisha naboresha kipando changu na kutafuta dereva hodari ili nipite njia ya pili
 
Asubuhi njia ninayotumia huwa inafoleni eneo fulani. Wengi wakifika hapo wanaingia kinjia fulani kifupi kina mashimo balaa ila hakina foleni.
Matokeo yake wakitokea kule mbele tunakutana na Sisi tulioamua kwenda kwa foleni.
Mimi nitatumia njia ya kwanza,naweza kuchelewa ila nitafika salama.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom