Unashauri nini kiwepo kwenye majumuisho ya Taarifa za kamati za Hesabu za Bunge?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unashauri nini kiwepo kwenye majumuisho ya Taarifa za kamati za Hesabu za Bunge??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Apr 19, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Baada ya Hoja kali kutolewa na wabunge wa vyama vyote bila kuangalia itikadi zao, jioni ya leo mnamo majira ya saa kumi na moja na kuendelea, kamati tatu za mahesabu ya serikali zitafanya hitimisho ya mambo/hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge mbalimbali. Je unaishauri nini kamati zifanye kwenye majumuisho hayo kulingana na hoja zilizotolewa na wabunge????

  Binafsi, Nashauri wamshauri Spika, wabunge wapige Vote of no confidence kwa serikali yetu dokozi maana bila kumwonea mtu. Si CCM wala CDM wote wamekiri kuwa Serikali yetu imeshindwa kazi. Na kinachofanyika sasa ni viongozi wa serikali kula na kufuja kodi za wananchi bila ya kuonyesha tija chanya. Tija pekee tunazoziona ni za mawaziri na watendaji wa serikali ni kwenye kuwezesha mikataba mibovu, kushindwa kusimamia majukum yao na kusababishia serikali hasara pamoja na kusimamia kuuzwa kwa raslimali za taifa kwa wezi wale wale.

  Kama hili litaonekana haliwezekani, basi watendaji wote waliolisababishia Taifa hasara wa step down kupisha uchunguzi tukianza na Mkullo ambaye ameuza kibabe viwanja viwili kwa wahindi wezi ambao kila siku tunawatolea povu humu. Toa ushauri wako unaweza ukasaidia kuangushwa kwa serikali hii dokozi ya ccm.
   
 2. l

  lyimoc Senior Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashauri wabunge wa ccm wakitaka kurudi bungeni basi wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali ili tuendelee kuwaamini vingindvyo hatarudi hata mmoja 2015 bungeni
   
 3. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Kwanza waziri wa fedha afukuzwe kazi mara.Bodi za wakurugenzi za mashirika husika zivunjwe na wakurugenzi watendaji husika wafukuzwe kazi.Pia Mhasibu mkuu wa serikali afukuzwe kazi mara moja.

  Pia Mawaziri wa wizara za ujenzi,afya,uchukuzi,utumishi,biashara wafukuzwe kazi mara moja huku uchunguzi tight ufanyike ili kama ubadhirifu mali ya serikali irejeshwe mara moja.


  Mwanasheria wa Serikali aondelewe mara moja na asirudi kufanya kazi ya ujaji inaonekana anatafasiri sheria kinyume na sheria kwa agenda zake mfukoni.

  Waziri mkuu ni kupewa onyo kali maana ni mwepesi sana ana ubavu wa kusimamia mambo hata kama atamuudhi mteule wake(Raisi).
   
 4. a

  adviser New Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashauri waanze kuwaajibisha waziri mmoja baada ya mwingine, wezi wakubwa sisi wafanyakazi wanatuambia serikali aina ela ,kumbe ela wanazo wanashindwa kuzimeneji zinawaneemesha wajanja wachache
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii motion ni muhimu ikawepo, hata kama wabunge wa CCM watapiga kura ya kuwa na imani na serikali. Strategically ni suala zuri kwani upepo wake utawafikia viongozi serikalini na wapiga kura majimboni wataingiwa na imani kuwa serikali inaweza kuwajibishwa kwa matakwa yao pale ambapo watawachagua wabunge watakaosimamia maslahi yao ni si ya vyama vyao
   
Loading...