Unashauri nini kifanyike kuliboresha Jiji la Dodoma?

Chakwale

JF-Expert Member
May 17, 2015
1,030
2,000
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Kama tujuavyo kuwa Dodoma sasa ndio Makao Makuu ya nchi yetu na Serikali kwa ujumla na ndiyo inayobeba taswira ya Tanzania yetu.

Kama nchi, kama wananchi na walipa kodi, tunalo jukumu la kuisadia na kuishauri serikali yetu namna gani Jiji letu liwe katika mpangilio tunaohitaji na tunaotaka.

Majiji mengi Afrika yako katika mpangilio mbovu usiozingatia mipango miji na kusababisha makazi holela,sisi kwa sasa na Dodoma yetu bado hatujachelewa kufikia huko tunayo nafasi ya kuweza kulifanya Jiji letu kuwa mfano.

Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi pia ni mwanachi, tunao wataalam wa kutosha humu ambao wanaweza kushauri namna bora ya kuyafanya makao yetu Makuu yawe katika mpangilio bora.

Kwa mfano, maeneo ya wazi, maeneo michezo, maeneo ya ibada, maeneo ya biashara, maeneo ya viwanda, nk.

Karibuni kwa maoni

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Dodoma
Mungu Ibariki Chakwale
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom