Unashangilia mwaka mpya unashangilia kulisogelea kaburi

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
1,002
2,000
Pole mwanadamu na hongera pia,unapoingia mwaka mpya na kaburi nalo linasogea karibu yako,watu wema wanalia na kutubia dhambi zao,mnaoipenda dunia mpo kwenye bar na kumbi xa starehe,enyi watu hakika maisha ya dunia ni mafupi na sio ya kudumu.JIANDAE NA MAISHA YA AKHERA KUMBUKA ARDHI IMEWAMEZA WAJANJA NA WAJUAJI KULIKO WEWE
 
mmash

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
432
500

Masha Allah,... Ujumbe mzuri sana,mwenye kusikia amesikia na mwenye kuelewa pia nae kaelewa.
 
KATATA

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
478
250
Majira na nyakati zimewekwa ili kuwakumbusha wanadamu kuwa hakuna jambo lidumuo. Sekunde inaisha na dakika kuanza, saa, siku, juma, mwezi na hata mwaka. Kila uanzapo mwaka kumbuka umepewa nafasi ya kuanza upya. Mwaka mpya unakuwa hauna maana kama umekusudia kuendelea kuishi vile vile ulivyokuwa ukiishi mwaka jana. Kukaribia kufa siyo sababu ya kutoshangilia. Maana wako wengi walio tamani kuendelea kuishi lakini hawakuweza kuwepo. Kushangilia ni ishara ya kushukuru kwa upendeleo uliopewa wa kuishi tena ili tuzirekebishe njia zetu za kumcha Mungu na hata za mafanikio ya kimwili. Hata usiposhangilia utakufa tu.
 
mgongo mtii

Member
Apr 8, 2016
46
125
Kila aliyezaliwa na mwanamke sharti afe, ushangilie usishangilie kufa kupo palepale, ila kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu maana wapo waliokufa punde tu baada ya kuzaliwa, na wengine wanateseka na maradhi hospitalini na hata hawajui mwaka umeisha maana hauna maana kwao kwa maumivu waliyonayo! Mshukuru Mungu kwa sadaka kwa kwa wahitaji.
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,155
2,000
Kufariki ni matokeo hauwezi kuacha kusherehekea au kufurahia kitu kisa utaja fariki...only weak people have that perception...
 
KING 360

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,999
2,000
Hata usipo shangilia utakufa tu lazima ufurahi koz wapo watu walitamani kuingia mwaka mpya but hawakuweza ni vizuri kuonyesha furaha yako kwa Mungu na kuzidi mumuomba
 
Jaby'z

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
3,815
2,000
wenzio wakisherehekea tu we hua unaharibu kama ulivyopata ziro form four
 
Nahonyo

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
3,765
2,000
Ndugu hutakiwi kukiogopa kifo, sababu kimepangwa, kumbuka kuhesabu miaka ni kama kuweka kumbukumbu tu. kwa maana hiyo basi kifo kipo pale pale kuwe na mwaka mpya au kusiwe, na furaha ya mtu huwezi ihoji wewe kila mtu ana malengo yake muhimu kuliko kifo unachofikilia wewe.
 
Kitoweo

Member
Nov 4, 2014
23
45

Malengo muhimu kuliko "kifo* yako kaburini sio hapa duniani
 
Mkono Mkavu

Member
Dec 22, 2016
70
125
Fanyakazi hapa duniani kama haufi na mtumikieni Mungu kwa sala na sadaka kama unakufa Leo. Acha ujinga mtoa mada acha watu wafurahi. Utakuwa mwisilamu wewe tena mwanamke maana ninyi ndo mafundamentalist
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom