Unapoulizwa swali...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Unapoulizwa swali, Kinachotakiwa ni jibu,
Usingoje mara mbili, na kutafuta sababu,
Wewe useme ukweli, au bora uwe bubu,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!!

Wewe toa hilo jibu, usiulize maswali,
Usipekue vitabu, jibu huna ukubali,
Ujibu kwa taratibu, bila kufanya ukali,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Ee ndugu habari gani, hilo ni swali rahisi,
Jibu lake siyo geni, akilini hulikosi,
Usiulize “ kwa nini?”, wewe si Abunuwasi,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Kaka unakwenda wapi, akuuliza jirani,
Unajibu “kwani vipi”, siyo jibu ni uhuni,
Ukafanya chapichapi, mguu uko njiani,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Dada unaitwa nani, swali linataka jina,
Unauliza “kwa nini?”, hilo si jibu bayana,
Ni ujanja wa mjini, kwepa swali kiaina,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Hoja yangu nimeweka, swali halijibu swali,
Ujumbe uje kufika, zikue zenu kauli,
Na uhuni kuwatoka, mnapoulizwa swali,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Wapewape vidonge vyao, mahayawani hawa wasio makwao,
kucha kunyoosha midole yao, kutahayari wasio misimamo yao,
michosho miswali yao, ufukara wa fadhila mioyoni mwao,
kujituma mwiko kwao, kunyemelea ni ufisi wao.

Nitaifyeka mivichwa yao, nikipalilia shambani kwangu,
thubutu waje na lao, mbililimbi mbivu kitaloni kwangu,
onyo natuma kwao, kwa babu i hirizi yangu,
kujituma mwiko kwao, kimbelembele ni usifi wao.

Mwangwi wa handaki.
 
Steve D kumbe u mzima kwenye mipasho? Hii Melody wakiiona wanaweza kuicopy hakyanani!
 
Hee, kumbe humu kuna malenga! Ngoja nami nijaribu.
Dada unaitwa nani, swali linataka jina,
Unauliza “kwa nini?”, hilo si jibu bayana,
Ni ujanja wa mjini, kwepa swali kiaina,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!

Nikimjibu "Neemah", huo utakuwa wimbo,
Nitakosa pa kuhema, jibu limekuwa fimbo,
"Neemah" mtaa mzima, jambo limezua jambo!!
Ni upi huo ujanja, pliiz, nielimishe.

Na kusema la uongo, nayaogopa madhambi,
Naihami yangu shingo, kesho hakuna maombi,
Mzee nipe mpango, jina lisiwe filimbi,
Ni upi huo ujanja, pliiz, nielimishe.

Kidogo nimejaribu, makosa msiyacheke,
Nasubiri hilo jibu, wa kijiji aliweke,
Kusubiri sio taabu, wala sina makeke,
Ni upi huo ujanja, Mzee nielimishe.
 
Enhee, unacheka nini?

Mfanyie mpango Cupcake wako awe na access akiwa nyumbani; asitegemee computer za kazini tu.

Cupcake ana access na internet 24/7...iwe kazini..nyumbani..everywhere.

Salama lakini?
 
Ujanja kukwepa swali
Kwa kupindisha kauli
Ni kama yule kuwili
Mwenye vichwa pande mbili!

Linapoulizwa swali,
Kinachotakwa ukweli
Siyo jibu la kejeli
Bali jibu la dhahiri.

Neemah habari gani
Jibu wewe hali gani
Uking'aka ati "nini"?
Basi hapo magirini!

Watokea mji gani
Wajibu kwani wewe nani?
Jibu hilo ni uhuni
Swali liweke pembeni
 
hilo swali kujibu kamwe silazimishe
kama huna jawabu siseme usikike
hata masihi yesu hakuyajibu yote
kwa werevu alijibu wasema weye
 
Ujanja kukwepa swali
Kwa kupindisha kauli
Ni kama yule kuwili
Mwenye vichwa pande mbili!

Linapoulizwa swali,
Kinachotakwa ukweli
Siyo jibu la kejeli
Bali jibu la dhahiri.

Tatizo huo ukweli, nyuma angalia tena,
Sio muuliza hali, bali muuliza jina,
Ukweli nikiujali, raha nitakuwa sina,
Hata nikiwa kwa mbali, "Neemah ningoje, bwana!"

Huoni ni usumbufu, jina kuwa tangazo?
Wala si umaarafu, bali sinema ya dezo,
Tena ile ya uchafu, isiyo na hata funzo,
Yatia kichefuchefu, ukweli kuwa apizo.

Neemah habari gani
Jibu wewe hali gani
Uking'aka ati "nini"?
Basi hapo magirini!

Huyu ataka kujua, hali niliyo nayo,
Jina alitambua, si yule mfuata nyayo,
Hakuna la kusumbua, wala kuleta kilio,
Mzee kichwa sugua, uuridhishe wangu moyo.
 
Back
Top Bottom