Unapotuma message

Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,523
653
kwanini tunapotuma message kwa kutumia simu za mkononi salio huwa linakatwa hata kama message yenyewe ikiwa 'not sent' au haijawa delivered? Je hii ni halali? Hapa haya makampuni ya simu yanakuwa yanatoza hela kwa huduma ipi waliyokupatia? Mtu unayemtumia anaweza akawa kazima simu au yuko out of coverage kwa muda mrefu na hivyo sms asiipate na simu inarudisha jibu kuwa 'message not sent' lakini salio linaliwa,why?

Hata ukituma msg kwenye namba ambayo haipo bado wanakuia salio,kwa nini? Lakini mbona unapopiga simu huwa salio linapunguzwa pale ambapo mtu wa upande wa pili atapokea simu! Na hata ukipiga namba ambayo haipo au haiko hewani, unajulishwa status ya namba uliyopiga bila kuliwa salio. Je huu si wizi unaofanywa na makampuni ya simu?

TCRA wanasemaje kuhusu suala hili?
 
ni kweli mku, mimi naona ni wizi tu, kwa sababu haiwezekani yule ambaye sms aliyotuma haijamfikia mlengwa atozwe fedha,huu ni wizi tu,TCRA WAINGILIE KATI.
 
Mkuu, Hili ni kweli kabisa mara ya kwanza walikuwa wanarudisha lakini siku hizi hata kama sms not sent wanakata wanakula ela ya bure.
 
kaka kwenye msg not sent hapo hata mini sielewi kwa nini wanalamba hela. lakini kwenye msg not derivered hapo sawa kwani si
kosa lao, wao wamepeleka msg ila wa upande wa pili labda hayupo hewani, hivyo wa kumlaumu ni wa upande wa pili kwa nini hakuwasha
labda simu.

Hivi wewe ukipanda gari na unaenda kumsalimia rafiki yako, bahati mbaya ukakuta hayupo, je utadai urudishiwe nauli
kwa kuwa mwenyeji wako hayupo hivyo lengo lako halikukamilika? Mi nadhani utadai nauli kama gari limeshindwa kutembea
(msg not sent) sio kwa sababu mwenyeji wako hayupo (msg not derivered)
 
kaka kwenye msg not sent hapo hata mini sielewi kwa nini wanalamba hela. lakini kwenye msg not derivered hapo sawa kwani si kosa lao, wao wamepeleka msg ila wa upande wa pili labda hayupo hewani, hivyo wa kumlaumu ni wa upande wa pili kwa nini hakuwasha
labda simu.

Hivi wewe ukipanda gari na unaenda kumsalimia rafiki yako,bahati mbaya ukakuta hayupo, je utadai urudishiwe nauli
kwa kuwa mwenyeji wako hayupo hivyo lengo lako halikukamilika? mi nadhani utadai nauli kama gari limeshindwa kutembea
(msg not sent) sio kwa sababu mwenyeji wako hayupo(msg not derivered)

Kama ni hivyo, mbona ukipiga simu na ikiwa mtu wa upande wa pili amezima simu unapata jibu 'the subscriber you are calling is not available' mbona fedha haikatwi? Kuhusu mfano wako wa kupanda basi mimi naona hauendani na somo husika kwa sababu mathalani nalipa nauli kutoka Dar kwenda Chalinze ninakuwa nimelipia gharama ya usafiri kati ya dar-chalinze na sababu za kwenda Chalinze hazimhusu msafirishaji.

Kama nilienda kununua mayai na nikayakosa si juu yao kwa sababu tiketi haioneshi 'Dar-Chalinze kununua mayai' bali 'dar-chalinze' na kuhusu kutuma msg kwenye simu lengo ni mwenye kumiliki mtandao afikishe ujumbe kwa mlengwa na kama ujumbe hakufikisha atakuwa bado hajatekeleza huduma hiyo na hivyo hastahili kulipwa.
 
kaka kwenye msg not sent hapo hata mini sielewi kwa nini wanalamba hela. lakini kwenye msg not derivered hapo sawa kwani si
kosa lao, wao wamepeleka msg ila wa upande wa pili labda hayupo hewani, hivyo wa kumlaumu ni wa upande wa pili kwa nini hakuwasha
labda simu. hivi wewe ukipanda gari na unaenda kumsalimia rafiki yako,bahati mbaya ukakuta hayupo, je utadai urudishiwe nauli
kwa kuwa mwenyeji wako hayupo hivyo lengo lako halikukamilika? mi nadhani utadai nauli kama gari limeshindwa kutembea
(msg not sent) sio kwa sababu mwenyeji wako hayupo(msg not derivered)

Umetisha mkuu tupo pamoja.
 
Nilikua silijui hili! Asante kwa taarifa. Kwenye simu huwezi kutoa thanks? Jf warekebishe hiki
 
Wizi mtupu..siku hizi wanakulazimisha ushiriki promotion za kitapeli eti etika wito namba flani, mara umechaguliwa sijui nini yani wezi Tcra mpaka ipigwe mkwara ndo inaamka
 
Nakumbuka Tigo mwaka 2004 ukituma msg hadi iwe delivered ndo unakatwa pesa. Sijui hii mambo waliipotezea lini?
 
Wizi mtupu..siku hizi wanakulazimisha ushiriki promotion za kitapeli eti etika wito namba flani, mara umechaguliwa sijui nini yani wezi Tcra mpaka ipigwe mkwara ndo inaamka

Wezi hawa jamaa,
Mi kila siku Voda wananidanganya eti "sishikiki" na kunikata Tshs 550/= kwa siku,
Nishatuma neno ondoa/toka/ cancel n.k. kwenda kwenye namba yao lakin wao wanaendelea tu na utapeli wao,
Nlichoamua sasa natuma "tusi" ili wajue sipendi wizi wao!!
 
hata ukituma matusi mia hakuna anayesoma hizo message hizo ni programs tu ni kati yako wewe na system ambayo imesetiwa kukujibu kadri unavyotuma message

zile message wanazokutumia ni za kukushawishi ujiunge ama ucheze usipocheza huwezi katwa fedha kila fedha utakayokatwa yaan 550,itakatwa tu kama ulituma...me nakushauri cheza kama una fedha za kuchezea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom