Unapotoka kusaliti (kuchepuka), unapokutana na mwenza wako hivi unajisikiaje?

Mara ya kwanza kabisa nilivyotoka kufanya yangu, naingia ghetto na yeye anapiga. Moyo ulipasuka paaa, nilihisi kama amejua nimetoka kucheza mchangani.

Lakini kadri siku zilivyoenda, nilizidi ya kunogewa upande ule, nilianza kum-ignore hadi nikaona wa kawaida sana, nikapata tena mwingine nikaunganisha humo.

Ni experience moja mbaya sana, inafanya ukose furaha na amani, inafanya uwe mtu wa matumizi tu kila siku, you spend with A, tomorrow with B and the following day with C. Hukai na pesa hata kidogo, thank goodness niliacha huo upupu...
 
Binafsi nilijaribu kuchepuka ( dhambi kwa mujibu wa imani yangu, na nimetubia hii dhambi sitoirudia tena hadi nakufa).

Huwa anajua nikibanwa na majukumu sana na muda ukiwa umeenda huwa nachukua hotel napumzika na huwa nampa taarifa, ni mwanamke na mama aliyetokea kuniamini sana kama mimi ninavyomuamini.

Sasa usiku mmoja sikuridi na nikawa nimepiga mechi ya nje ( demu wa kuota huko duniani ), wakati narudi home asubuhi, nikamuona mchumba anapita njia ya juu sijui alikuwa anaenda madukani, ikabidi mie nipite njia ya chini kumkwepa, nikakosa kabisa confidence ya kukutana nae wala hata kumsalimia uso kwa uso ( sijui aliona au hakuniona )...

Nikafika home nikaoga, nikawasha laptop nikaanza kupitia mambo mawili matatu, akarudi wala hakuniuliza kitu, akaniandalia chai akaniwekea mezani nae akaja kukaa pale tukaanza kupiga story mbali mbali huku tunakula ( moyoni mwangu nikawa nasema huyu kama akijua nilichofanya usiku wa leo sijui itakuwaje hapa, na cha ajabu mapenzi yake kwangu ndio yakazidi kweli kweli, utani mwingi, cheko nyingi na furaha iliyotamalaki moyoni mwake, ndio nikawa nakosa kabisa amani nikawa nafumba fumba macho kama usingizi vile umenipitia ili nimkimbie nikalale, kabla ya kunipa ruhusu ya kwenda kulala, anapotaka kutoka huwa lazima tupige magoti kidogo tuombe kwa pamoja ndio aendelee na issue zingine.. na kwenye kuomba ukawa mtihani mkubwa zaidi...

Kwa wengine mlipokutana na mazingira haya mlikuwa katika hali gani na mliweza kumudu vipi?
Mkuu endelea kujifunza hiyo dhambi baadae utaiona ya kawaida hata mchana unaenda kukaza bila hofu yoyote
 
Akiii na mimi najiulizaga sana wanaoishi na wenzi wao huwa wanajisikiaje wakitoka kuchepuka.

Nilishawahi kuachana na bf miezi kadhaa nikapata mwingine. Yani kitendo cha kulala na yule kaka roho iliniuma namcheat mtu ninaempenda wakati hata hatuko wote.
Nililia usiku kucha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie ni wajinga kuchepuka sio kusaliti au kutompenda mwenzio ni ishu ya kubadili mvinyo kwenye chupa tofauti tofauti,sasa kuchepuka kuna shida gani
 
Simamia imani yako aisee, maana utakuwa umebaki pekebyako kwenye imani juu ya mambo hayo, maana wengi sasa wabatoka kwenye usaliti na bado anakutana na mwenza wake anaomba gemu tena huku akimtolea macho makavu kama mvuta bangi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom