Unapostawisha chuki, kero na maudhi, vitu hivyo vinaua taratibu kuliko hata sumu

ZOPPA

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
2,695
2,787
Leo nataka nikupe somo zuri la kuweza kumuua mumeo kama humpendi na ww bila kufungwa na police na bila kushtakiwa na ndugu yeyote na ukabaki kwa Amani katika maisha yako yote.Nawe mwanaume unaweza kusoma pia utaweza kumuua Mkeo kwa kutumia njia hii pia.

Binti mmoja aliyeolewa alifika kwa mama yake kumlalamikia kuhusu ndoa yake. Malalamiko yake yalikuwa kama ifuatavyo:

BINTI: Mama, mume wangu amenishinda. Ninataka kumuua lakini nakosa ujasiri wa kufanya hivyo, unaweza kunisaidia tafadhali?

MAMA: Ndiyo binti yangu, ninaweza. Lakini kuna tatizo dogo utatakiwa kulishughulikia kwanza. Itakubidi uanze kutengeneza mazingira na hali ya amani kati yako na mumeo ili kwamba watu wasikutilie shaka kwamba wewe ndiye umehusika na kifo chake. Utatakiwa kuwa mwema sana, mpole na umhudumie kwa moyo wote.
Uwe romantic kwa Mume wako maana ulimpenda Ndio maana ulikubali kuolewa nae, uwe unamshukuru sana, uwe mwenye subira, na mnyenyekevu kwake. Mchukulie kama mwanao badala ya kumchukulia kama mkubwa mwenzio au raia wako… usiwe mbinafsi, uwe mnyoofu, msikilize sana, msafishe, mnawishe, usimsumbue au kumponda.
Mwanangu, nina uhakika kwamba unaweza kuyafanya hayo, huna sababu ya kuutilia shaka uwezo wako. Kazi hiyo ianze leo jioni. Je, unaweza kufanya hivyo?

BNTI: Ndiyo mama.

MAMA: Sawa. Sasa chukua huu unga mweupe ambayo ni sumu itakayomuua. Kila siku unapomuandalia chakula weka kidogo kwenye chakula hicho, itakuwa inamuua taratibu.

Baada ya siku 30, binti akarejesha majibu kwa mama yake.

BINTI: Mama, kwa kweli sitaki tena kumuua mume wangu. Amekuwa romantic sana, amekuwa mbembezi na mwenye upendo mkubwa. Ninampenda, amebadilika na amekuwa laini tofauti na mwanzo. Sasa Nifanye nini kuzuia sumu ile isimuue? Nisaidie mama yangu kipenzi, tafadhali.

MAMA: Hahahahahahaha

BINTI: Kwa nini unacheka? Muda unakwenda, nataka kuokoa uhai wa mume wangu.

MAMA: Hapana mwanangu! Huna sababu ya kuwa na wasiwasi. Nilikupa unga wa muhogo. Hatokufa.
Ukweli ni kwamba, sumu ulikuwa nayo wewe. Unapostawisha chuki, kero na maudhi, vitu hivyo vinaua taratibu kuliko hata sumu, hivyo nililazimika kukushughulikia wewe kwanza badala ya mumeo.

BINTI: Hmmmmmm. Ahsante mama’ngu kipenzi.

DONDOO MUHIMU:
☛Itengeneze furaha yako na kuwafanya wanaokuzunguka kuwa na furaha.

☛Unapoanza kumpenda na kumthamini mumeo, mkeo, kaka yako, dada yako, mwanao, mama yako na baba yako, utayaona mambo mazuri na matamu kwao.

☛ Usisubiri mpaka mtu aumwe au afe ndo unaanza kumkubali, kumthamini na kumtukuza.

☛ Kabla hujaanza kulalamika, angalia kama tatizo halitokani na wewe.

☛Ishi kwa amani na kila mtu.
Tuna uwezo wa kuona mazuri kwa wenzetu tukiwa na MTAZAMO CHANYA na iwapo hatutajipa sumu ya MTAZAMO HASI kwa kuyaona MABAYA yao tu tukaacha kuyaona mazuri yao pia.

Imani ya penzi lenu katika mahusiano au katika ndoa yenu msiweke kwenye vitu maana vitu hivyo vikiharibika na Upendo wenu utaisha na pia usikubali uanze kuonyesha Upendo Kwa mkeo/mumeo wakati amefariki Upendo unapaswa kuonyeshwa wakati yupo hai ili ajivunie kuwa pamoja nawe.


kutoka Inbox
"Asante Sana kwa wale mnaokuja Inbox na kusema kuwa mnafurahia mafundisho yangu mpo wengi thanks so much all na ushaur zenu nafanyia kazi."

Tupo darasani tunafundisha najifunza toka kwako pia toa maoni katika Comment.

Nakutakia siku njema tuombe heri tukutane Kesho.
 
Hayo yote ya nini? Huna haja ya kumuwazia MTU kifo, MTU akutese akunyanyase, kiboko yake IPO kwa Mungu, yaani Mungu anatumia kiboko kile kile kumpiga hapa hapa duniani,

Ukishajua hayo yote lazima ukumbuke ule wimbo wa , Ombea adui yako.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom