Unaposema fulani ni rafiki yangu,huwa unamaanisha nini?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
12,105
2,000
Unaposema fulani ni rafiki yangu,huwa unamaanisha nini?
 • Anakusaidia kwenye shida
 • Anabadilishana na wewe mawazo tu
 • Anakupiga mizinga tu
 • Anakusaiia mikopo midogo midogo
 • Anakupa ushauri wa busara
 • Anakusaidia kiuchumi pale unapoanguka
 • Anakutafutia wapenzi
 • Anakupa umbea
 • Anakuwa na wewe kwenye raha
 • Anakufariji kwa maneno tu
 • Uko naye kwa sababu wenzako pia wana marafiki
 • Haujui kwa nini uko naye
 • Anakusaidia kutumia hela zako
Ipi inaweza kuwa ni sababu kuu?
 

SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,706
2,000
Equation x, Dah! Nina rafiki yangu mmoja, nikiwa fresh kiuchumi ndipo tunaungana pamoja! Ila akiona sipo vizuri mazungumzo yetu yanaishia kwenye simu tu.

Yeye akiwa fresh utamsikia mikoa jirani tu, leo nipo Mara, kesho nipo Simiyu na Geita!

Namvutia kasi, ipo siku atajigundua tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
12,105
2,000
Dah! Nina rafiki yangu mmoja, nikiwa fresh kiuchumi ndipo tunaungana pamoja! Ila akiona sipo vizuri mazungumzo yetu yanaishia kwenye simu tu.

Yeye akiwa fresh utamsikia mikoa jirani tu, leo nipo Mara, kesho nipo Simiyu na Geita!

Namvutia kasi, ipo siku atajigundua tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni wa matumizi tu
 
Top Bottom