Unaposafiri na Bus unapenda viti (seats) gani?

Wickama

JF-Expert Member
Mar 8, 2009
1,466
1,194
Wanaukumbi, sote tumeshawahi safiri. Hususan kwa usafiri wa mabasi. Kuna mwelekeo kila mmoja wetu ana viti (seats za kwenye Bus) ambavyo anajihisi roho kutulia sana akivipata ili kusafiri. Pia, Kila mmoja ana sababu za chaguo lake. Hebu eleza wewe unapenda seats zipi na sababu zako. Wasalaam.
 
Mi huwa napenda upande wa dereva,siti kama ya pili au ya tatu toka kwa dereva,alafu niwe dirishani,kwa iyo najifungulia dirisha nitakavyo!
 
Nakushauri ukae viti vya katikati sehemu ile ya kupitia. Ogopa sana viti vya mbele na dirishani na pia usisahau kufunga mkanda. Nawasilisha.
 
Huwa napenda seat ya kushoto dirishani....
Sababu za msingi ni site(kupishana)
Upande wa dereva si salama sana kwenye kupishana na gari.
 
Upande wa dereva siti ya katikati hili hata kama kuna kutokea ajali dereva huwa anakwepesha upande wa pili so unaweza kuwa kati ya waliotoka bila majelaa.

swissme
 
Wanaukumbi, sote tumeshawahi safiri. Hususan kwa usafiri wa mabasi. Kuna mwelekeo kila mmoja wetu ana viti (seats za kwenye Bus) ambavyo anajihisi roho kutulia sana akivipata ili kusafiri. Pia, Kila mmoja ana sababu za chaguo lake. Hebu eleza wewe unapenda seats zipi na sababu zako. Wasalaam.
Mi napenda siti zinazolala
 
Nakushauri ukae viti vya katikati sehemu ile ya kupitia. Ogopa sana viti vya mbele na dirishani na pia usisahau kufunga mkanda. Nawasilisha.

Na ndio siti ambazo huwa nakaa. Wakata ticket huwa wanashangaa sana pale ninapopewa chati na kuchagua hizo.. mbali na suala la usalama huwa zinanipa fursa ya kunyoosha miguu pale ninapokuwa nimechoka kwa style ya kukunja tu miguu kama siti za dirishani na ukikutana na basi lenye siti zilizobanana ndio utakoma.
 
Napenda siti ya katikati koridoni. Hapo najisikia vizuri sana na kufurahia safari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom