Unapopewa zawadi na mpenzi wako jiulize una mapungufu yapi?

green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
11,304
35,851
Wakuu habari za weekend,

Leo nakuja na ushauri au maoni yangu juu ya uhalisia wa zawadi tunazopokea toka kwa wapendwa wetu tuwe tunazitafakari kwa upande wa pili. Namaanisha unaletewa Pafyumu au body spray jua kabisa unaharufu mbaya inayomkera mwenzio ila kashindwa namna ya kukwambia na hataki mkwazane.

Pia ukipokea zawadi ya Chupi kwa Ke au Boxer kwa Me jua kabisa kabisa haupo vizuri kwenye hiyo sector au una chupi zilizokomaa au za kishamba, unaletewa miswaki sabuni mafuta viwembe anataka ung'ae na usafishe mdomo labda usafishi vizuri hunyoi unanuka kama beberu.

Kumbuka mpenzi wako awe ke au me amekutana na watu wengi kabla yako wengine wapo vizuri kuliko wewe sasa hawezi kukwambia ila atakushape unafanane na wale anaona wanafaa zaidi anakupa maujanja japo nawe uonekane mtu.

Kijana kua smart hata kama hauna mpenzi sio kijana au binti unakua na chupi 3 afu unakaa nazo mwaka sinland 2 soksi pea 2 zimetoboka chafu sidiria 2 zimechakaa tight imetoboka mapajani kwa unene huo ni uchafu.

Mimi nikiwa na demu siku ya kwanza nikimuona hayupo smart hua nampotezea mazima...
 
Tupunguze kuwa na mitazamo hasi kwenye mahusiano na wenza wetu, kwani kuna mengi ya kupendeza na kufurahia sana kwenye mahusiano ya kimapenzi badala ya kuwa na mtazamo hasi. Niwahimize tuendelee kutoa zawadi kedekede, mara kwa mara kwa wenza wetu, kwani kumpa zawadi mwenza wako ni mojawapo ya kichocheo na kikolezo bora kabisa katika kuthibitisha upendo na jinsi gani unavyomjali mwenza wako.

Tofauti na inavyosemwa hapa wenza wengi hupendelea sana kupewa zawadi. Badala ya kuhangaika kutafsiri kila aina ya zawadi tunazopewa na wenza wetu, tunapaswa kushukuru na kufurahia kila zawadi tunazopewa na wenza wetu kwani ni alama ya upendo ni si vinginevyo.

Je, ukipewa zawadi ya maua, saa, gari, nyumba, chocolate? nazo utazitafsiri vipi?
 
Inaonekana we ni mshamba wa mahusiano. Ebu tuambie wewe ni zawadi gani unampa mpenzi wako ? Kuna brand ya perfume nilikua natumia ila haikua ya kiume nikaletewa brand flani kali sana na ipo ki gentlemen, apo utasema nanuka aya nimeletewa saa mpya ya rado original na ninazo zingine 3 , apo utasema sijali muda?

Mi niliona nguo flani za kulalia kali maali zinevalishwa midoli nikasema daah hii akipiga wife itabamba sana nikamchukulia so itakua alikua analala na jeans ndo maana nikamnunulia au? Acha undezi
 
Wenzako hata tukienda kuwasalimia wazazi wetu tunawapelekea zawadi eg.kitenge kwa bi mkubwa sio kwamba hana vitenge.
Watupendao wakitupa zawadi alhamdulilah tunaona wanatupenda na kutujali pia!!
Mtu akikupa zawadi ni namna moja wapo ya kuonesha upendo
 
so itakua alikua analala na jeans ndo maana nikamnunulia au? Acha undezi.. najua wengi mlishapokea zawadi za namna nlivyosema ila kama umejirekebisha haina tatizo piga vitu vya kijanja mkuu
 
Wenzako hata tukienda kuwasalimia wazazi wetu tunawapelekea zawadi eg.kitenge kwa bi mkubwa sio kwamba hana vitenge.
Watupendao wakitupa zawadi alhamdulilah tunaona wanatupenda na kutujali pia!!
Mtu akikupa zawadi ni namna moja wapo ya kuonesha upendo
Kwa wazazi ndg sitatia neno ila kwa wapendwa wetu huko ndio kuna izo mambo
 
Dalili za roho mbaya hizo na zikiendelea unakuwa mchawi, mfano leo kuna watu wamenuna kuona Messi katupa zawadi ee ya tuzo tatu kwa mpigo.Sasa kushupaza shingo kama kivuko cha Mv Victoria ni nini?
Huo ndio uchawi wanga wazi wazi.
Washindwe na walegee
 
Back
Top Bottom