Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,884
Kwema Wakuu!
Kuna viongozi wakipewa dhamana wanarukwa sijui na akili, wanafoka foka, kufokeana watu wazima ni kudhalilishana tu.
Hakuna aliyekulazimisha uteua mtu, Kama mtu kaboronga fukuza kazi, sheria zingine zifuate.
Sio kupewa tuu uongozi unajifanya mkoloni ndani ya nchi, na kuwabagaza wasaidizi wako kama vile Wake zako.
Usilete mambo ya kijeshi kwenye uongozi hasa Kwa kizazi hiki.
Ukitaka ubabe na kufokeana nenda kaombe Cheo jeshini huko, ndipo kuna ubabe ubabe na kufuata amri. Tena nadhani haa jeshini kunataratibu zake.
Unakakuta kakijana kadogo tuu kanafokea watu wazima waliokazidi umri kisa kana uongozi.
Nyie Wazee wapumbavu, wajinga,
Sijui ninyi ni majizi, mafisadi, utadhani Yeye ndiye Jaji au hakimu aliyethibitisha hatia ya Msaidizi wake.
Tuheshimiane.
Huwezi mfokea mtu hadharani ili upate sifa Kwa watu, uonekane Mchapakazi na mwema.
Vijana wadogo, mnaoingia kwenye Siasa jihadharini na mambo ya kufokea watu ilhali mnatumikia Umma!
Ukitaka kufokea watu anzisha Kampuni yako, fokea Wafanyakazi wako,
OA na zaa watoto wafokee hao ndio halali yako.
Hata mke anayejielewa huwezi mfokea kipuuzi puuzo akakuvumilia.
Taratibu zipo, andika barua au sema sina kazi, Kama ni mwizi kesi ipelekwe mahakamani.
Lakini sio watu tutoe Kodi zetu ili utufanye Kama watoto wako, hiyo hapana! Umezoea kufoka kafoke huko kwenu!
Hii ni nchi, hili ni taifa! Sio jamii au kikundi Fulani cha watu! Au kitaasisi Fulani! Lazima viongozi wajue hilo.
Lazima wajue nchi hii inamakabila zaidi ya 120 na watu wa kila namna. Hivyo heshima kitu cha Bure!
Unapewa uongozi unataka kuleta mambo ya kwenu huko kwenye nchi,
Ukiongoza uwe na adabu na heshima ili uheshimiwe!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam