Unapooa single mother usifikirie tu habari ya mzazi mwenzake bali fikiria hata kipindi cha uzee wako

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
4,540
2,000
Wakuu habari zenu.

Mimi ni mfuasi wa wanawake walioolewa bikra, na wanawake wenye bikra mpaka hivi leo. Nina sababu zangu nyeti za kuwapenda na kuwapigia chapuo wanawake hao, pia nawashauri vijana waodgo na wakubwa ambao mpaka sasa hamjaoa, Basi oeni wanawake wenye bikra. Usije ukajichanganya wala ukalaghaiwa na maneno ya wanawake malaya. Biblia inasema; Mwanamke malaya midomo yake yadondoza asali. Yaani wana maneno matatu ya kukurubuni, nawe kwa ujinga na ushamba unaingia mkenge. Usikubali.

Sasa nije kwenye mada yetu ya Single mothers ni sikio la kufa.

Kwanza nianze kwa kusema 95% ya single Mother ni sikio la kufa, vichomi, viungulizi, na wauaji. 5% Wapo vizuri, tena kwenye hiyo 5% 3% ni wale waliofiwa na waume zao au waliowazalisha. 2% ndio ambao ni singele mother waliotalakiana na waume zao au waliowazalisha na wakawa na tabia njema. Kwa waliosoma Hesabu za probability mtaungana na mimi kuwa hakuna uwezekano wa kumuoa single mother mzuri na kama uwezekano upo basi ni mdogo.

Usumbufu wa Single mother unaanzia hapa

1. Mtoto wake ndio kipaombele.
Single mother wote duniani 95% watoto wao waliokuletea ndio kipaombele namba moja, yeye namba mbili, wazazi wake namba tatu, kisha wewe ndio unashika namba nne. Single mother wengi 95% wanataka wewe usiye baba wa mtoto ubebe jukumu lisilokuhusu, Yaani umlee mtoto wa mwanaume mwingine, na usipofanya hivyo utaingia kwenye uhasama, migogoro, vita, na ikiwezekana kukudhuru kisaikolojia. Wao humtumia mtoto kama kinga na uthibitisho wa mapenzi yako kwao. Jambo ambalo wanaume wengi 90% hatuwezi.

Kumbuka mtoto huyu huyu baadaye anaweza kuwa kitanzi kwako.

2. MAHUSIANO NA MZAZI MWENZAKE
Kisheria na kimila huwezi vunja mahusiano ya Mke wako aliye-single mother na mzazi mwenzake, hiyo haiwezekani. Itawezekana tuu endapo Mwanaume(?huyo mzazi mwenza) hatakuwa na habari naye. Yaani kaamua kumtelekeza. Itawezakana kama mzazi mwenzake amekufa, Pia, itawezekana endapo uchumi wako ni mkubwa mara mia moja ya mzazi aliyemzalisha. Vinginevyo utaambulia maumivu. Mwanzoni ataonyesha kujificha lakini kadiri siku zinavyoenda ataanza kukujibu kuwa huyo ni mzazi mwenzake hawajadili mapenzi bali wanajadili masuala ya mtoto.

Wanaumr erngi 90% hatupo tayari kuona majadiliano yoyote yale, yawe ya mtoto, sijui ya nini baina ya wake tuliowaoa na wanaume wengine hasa waliowahi kuwa kimapenzi na wake zetu.

3. KUTIMIZA RATIBA
Single mother wengi huolewa ili kutimiza ratiba na sio mapenzi ya kweli. Wengi ni vichomi, vigagula, tena upate wale wenye umri kuanzia miaka 30 wengi 90% washanusa kwenye milango ya waganga wa kienyeji kama sio kununua uchawi kabisa, Wengi wana chale miilini mwao. Usishangae kukuta chale kwenye makalio, katikati ya maziwa, juu ya kiuno n.k.

Hawana Munkari wa ndoa, ukifika nyumbani wanakereka, wao hupenda kuishi wenyewe na watoto wao.

4. WENGI HUSUBIRI WATOTO WAKUE
Single mother wengi hujifanya wavumilivu, huvumilia uwepo wa waume zao ndani ya nyumba japo hawapendi ukiwepo nyumbani. Hufanya hivi wakisubiria watoto wakue kue mpaka miaka 20 walau, tena husubiri mtoto akimaliza chuo na kupata kazi na hapo ndipo utaonja joto ya jiwe. Ujeuri unaanza, kiburi, dharau, na umalaya unapamba moto, wanajua huwezi kuwafanya chochote, ukiwazingua wanakimbia kwa watoto wao maana tayari wanakazi, tena usiombe mtoto wa nje ndio akawa na mafanikio mbona utaisoma namba.

Wengi wakifika muda huu hudai talaka kivyovyote. Huwababaishi.

90% ya single mother wapo kimaslahi, hawana mapenzi ya kweli kwa waume zao. Wanachokifanya ni kuwarubuni ili wapate pakuishi na kusubiri mtoto wake wa nje akue. Akishakua hana wasiwasi watoto wako anajua anauwezo wa kukuachia hapo akaondoka kwani hutaweza kuwafukuza.

Unapooa single mother usifikirie tuu habari ya mzazi mwenzake bali fikiria hata kipindi cha uzee wako. Single mother wengi 90% husumbua uzeeni hasa watoto wakishakuwa na maisha fulani ya kujitegemea.

Nimalize kwa kushauri;

Usioe mwanamke asiye na bikra. Usioe mwanamke ambaye ni masikini. Hutaki acha hakuna anayekulazimisha. Single mother 95% ni sumu. na sumu haionjwi

Nawasilisha
 

Boei

Member
Oct 4, 2020
66
150
Sema nini ...kuna ukweli mchungu sana hapa wengi hatutaki kuusikia wala kuambiwa...
Anyway single mothers walikuwepo , watakuwepo na wataendelea kuwepo... Cha msingi men wabadilike ... Haikwepeki wanaume hapa lawama katika chanzo cha ma single mothers
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,497
2,000
ni ngumu kuwafanya binadamu wote wawe na mtizamo mmoja juu ya jambo lolote lile, kuna watu wanaamini katika single maza huwaambii kitu pia kuna watu wanaamini katika bikra kama mleta mada, hivo tujitahidi kuidhibiti mihemko yetu dhidi ya watu wengine maana haipendezi kuwakosea adabu coz tunamitizamo tofauti juu yao
 

privity

Member
Feb 6, 2020
93
400
Mkuu kuna jambo baya lilikupata kwa Single mother?
Kuna haja gani ya kuendesha kampeni kwa kuwalaumu hawa wadada na mama zetu.

Mbona kama hili jambo lipo "personal" sana?

Yaani unajua tabia za wanawake wote "Single mothers"?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom