Unaponunua umeme ukapewa Token na Units, ukiziingiza kwenye mita inajuaje kuwa hizo token ni unit kadhaa?

Candela

Member
Aug 12, 2021
73
150
Habari wadau.
Mi nataka kujua jambo moja silielewi kabisa. Nimejaribu kufatilia nyuzi kadhaa humu jf lakini patupu, hakuna maelezo kamili.

Ipo hivi, unaponunua umeme ukapewa Token na Units, ukiziingiza kwenye mita i ajuaje kuwa hizo token ni unit kadhaa. Maana watu wanasema hizi mita hazina mawasiliano na server za Tanesco, sasa najiuliza ukipewa token umaziingiza zinabalishwaje kuwa unit katika level ya Mita yako.

Nawasilisha.
 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,557
2,000
Habari wadau.
Mi nataka kujua jambo moja silielewi kabisa. Nimejaribu kufatilia nyuzi kadhaa humu jf lakini patupu, hakuna maelezo kamili.
Ipo hivi, unaponunua umeme ukapewa Token na Units, ukiziingiza kwenye mita i ajuaje kuwa hizo token ni unit kadhaa. Maana watu wanasema hizi mita hazina mawasiliano na server za Tanesco, sasa najiuliza ukipewa token umaziingiza zinabalishwaje kuwa unit katika level ya Mita yako.
Nawasilisha.
Hili swali la kisayansi linafuata nini chit-chat?
 

Majan

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
978
1,000
Mbona ukiangalia kwene list yako ya manunuzi ya umeme kiasi cha unit ulichopata kimeambatanishwa pamoja na hizo token
 

dronedrake

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
10,267
2,000
unaponunua umeme unaingiza vitu viwili, mita namba na pesa

zinatumwa kwenye server, pesa inabadilika kuwa units (kulingana na tariff uliyopo), then units zinaungwa na mita namba pamoja, zao linakua encrypted then linakua encoded, kwa standards za STS (algorithm) , token inatoka na kutumiwa wewe

ukiingiza token kwenye mita, mita ina micro processor inafanya reverse ya kile kilichofanyika hapo juu kwa standard ile ile ya STS

token inakua decoded,decrypted , inapatikana mita namba na units

processor inaangalia mita namba ikiyopatikana inalandana na mita namba yako ? kama ndiyo units zinaingizwa na kuongeza umeme ,
 

Candela

Member
Aug 12, 2021
73
150
Hujaelewa mkuu, ni hivi kama unanunua umeme wa 10,000 kila mwezi unapata unit 28 ila token number hazifanani kila unaponunua. Swali langu ni kuwa hii meter nayojaza umeme inajuaje kiasi cha units kutika kwenye token. Kumbuka hizi mita hazina mawasiliano na TANESCO.
Mbona ukiangalia kwene list yako ya manunuzi ya umeme kiasi cha unit ulichopata kimeambatanishwa pamoja na hizo token
 

UVIKO

JF-Expert Member
Jun 14, 2021
265
500
Mimi nakujibu Kwa uelewa wangu na siyo kisayansi..ninavyodhani Mita namba zote zipo recorded katika mfumo WA Tanesco ,ukitaka kununua umeme unaingiza vitu viwili kiasi na Mita namba ukisha maliza utaletewa message IPO full Kwa maelezo naamanisha Kias,Mita namba,idadi ya unit,token,na mengineyo Sasa tarifa hizi zimechakatwa na mfumo /system ukija kuingiza token Mita namba Kwa kuwa ni mfumo WA Moja Kwa Moja itafanya KAZI ya kujua hizi token ndizo zilichakatwa na system .vikiwa the same kitu kinakubali
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,970
2,000
Kumbuka hizi mita hazina mawasiliano na TANESCO.
Ni kweli hazina mawasiliano yale ya kwenye mtandao, ila zina uhusiano. Wewe hapo ulipo nikikupatia jina langu na akaunti namba yangu ya benki, unaweza kuniwekea hela kwenye akaunti yangu na zikaingia pasipo mimi na wewe kuwa tunafahamiana. Uhusianao huu ndiyo uliopo kati ya TANESCO na mita namba za umeme
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom