Unaponunua maji basi unachouziwa ni chupa tu, maji ni bure

Hata Mimi ningekuuliza hivyo hivyo, inawezekanaje muuzaji akuulizie chupa na wala sio maji?

Hebu tafakari ulichokiandika na ikiwezekana ukifute kabisa. Ina maana maji hayana cost production?
Imagine !??
 
Nashangaa sana mnaosema nakwepa swali.. Sasa iko hivi yale maji yanakuwa ni reference ya mauzo yaani kwa maana nyingine wakikupa maji tupu watashindwa kupata ya kuwekea kwenye chupa ambayo inawapa hela wao..sijui umeelewa hii scenario
Watashindwaje kuweka sasa wakati umesema maji ni bure na ni haya haya ya dawasco?
 
Sasa kaka unashindwa hata kujiongeza hapo wewe unafikiri dawasco maji wanayatoa wapi, wao wanayanunua? maji wao hawayanunui unacholipia hapo kwenye hio bili yako ni gharama za mitambo na production kwa kuconvert kwenye units..maji ni bure kaka
In that case maji sio bure sasa
 
Maji yana ingredients gani, amka mlamu!
MAJI YAPO MENGI MLAMU
Dasani-strawberry-water.jpg
 
Hii si excuse aliyoitumia yule mzalisha maji mashuhuri?

Akaulizwa kama wewe ni muislam kweli mbona unawauzia watu maji? Ndiyo akajibu hivi kua yeye anauza chupa hauzi maji.

Kwani wapi uliambiwa ukiwa "muislamu kweli" ni haramu kuuza maji?
 
Hii si excuse aliyoitumia yule mzalisha maji mashuhuri?

Akaulizwa kama wewe ni muislam kweli mbona unawauzia watu maji? Ndiyo akajibu hivi kua yeye anauza chupa hauzi maji.

Soma fatwa hii namna uislamu ulivyofafanua jambo la kuuza maji

*HUKUMU YA KUUZA MAJI! ๐Ÿšฐ*

fawaidusalafiyatz online


ุงู„ุณุคุงู„ - (ูกูฃูจ):

Swali - (138):


ู‡ู„ ูŠุฌูˆุฒ ุจูŠุน ุงู„ู…ุงุก ูˆู…ุชู‰โ€ุŸ

Je, inaruhusiwa kuuza maji na muda gani (inaruhusiwa)?


ุงู„ุฌูˆุงุจ:

Jawabu:

โ€
ููŠ ุฐู„ูƒ ุชูุตูŠู„ ุฅุฐุง ูƒุงู† ุญุงุฒ ุงู„ู…ุงุก ููŠ ูˆุนุงุฆู‡ ุฃูˆ ุจุฑูƒุชู‡,

Katika hilo kuna ufafanuzi pindi (mtu) akiwa ameyakusanya maji katika chombo chake au birika yake,


ูุฅู†ู‡ ูŠู…ู„ูƒู‡ ูˆูŠุฌูˆุฒ ู„ู‡ ุฃู† ูŠุจูŠุนู‡ ู„ุฃู†ู‡ ุญุงุฒู‡ ูˆุงุณุชูˆู„ู‰ ุนู„ูŠู‡,

Basi (muda huo atakuwa) anayamiliki na anaruhusiwa kuyauza, kwa sababu yeye ameyakusanya na ameyatawala,


ูˆุชุนุจ ููŠ ุชุญุตูŠู„ู‡ ูุตุงุฑ ู…ู„ูƒู‹ุง ู„ู‡ุŒ

Na akapata tabu katika kuyapata (kwa hali hii) yamekuwa ni miliki yake,


ุฃู…ุง ุฅุฐุง ูƒุงู† ุงู„ู…ุงุก ุจุงู‚ูŠู‹ุง ููŠ ุงู„ุจุฆุฑ ุฃูˆ ููŠ ุงู„ู†ู‡ุฑ ุฃูˆ ููŠ ุงู„ู…ุฌุฑู‰ ุงู„ุฐูŠ ูŠุฌุฑูŠ ููŠ ู…ู„ูƒู‡,

Ama yakiwa maji yamebakia katika kisima au katika mto au (yakawa) katika mapito ya miliki yake,


ูู‡ุฐุง ููŠู‡ ุฎู„ุงู ุจูŠู† ุฃู‡ู„ ุงู„ุนู„ู…,

(Hukumu ya) hili kuna tofauti baina ya wanachuoni,


ูˆุงู„ุตุญูŠุญ ุฃู†ู‡ ู„ุง ูŠุฌูˆุฒ ู„ู‡ ุจูŠุนู‡,

Na (kauli) sahihi kuwa haruhusiwi kuyauza,


ุจู„ ูŠูƒูˆู† ู‡ูˆ ุฃูˆู„ู‰ ุจุงู„ุงู†ุชูุงุน ุจู‡ ู…ู† ุบูŠุฑู‡,

Bali yeye anastahiki zaidi kunufaika nayo kuliko mwingine,


ูˆู„ูŠุณ ู„ู‡ ุฃู† ูŠู…ู†ุน ุงู„ุขุฎุฑูŠู† ู…ู† ุงู„ุงู†ุชูุงุน ุจู‡,

Na haruhusiwi kuwazuia wengine,


ุงู†ุชูุงุนู‹ุง ู„ุง ูŠุถุฑู‡ ู‡ูˆ ูˆู„ุง ูŠุถุฑ ููŠ ู…ู„ูƒู‡,

Unafaikaji usio mdhuru huyo (mwenye eneo) na wala hauleti madhara katika miliki yake,


ู„ุฃู† ุงู„ู†ุจูŠ ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู… ู†ู‡ู‰ ุนู† ุจูŠุน ูุถู„ ุงู„ู…ุงุก, โ€

Kwa sababu Mtume amekataza kuuza ziada ya maji.


๐Ÿ“ ุงู„ู…ู†ุชู‚ู‰ ู…ู† ูุชุงูˆู‰ ุงู„ุดูŠุฎ ุงู„ููˆุฒุงู†.

[ Al-muntaqaa min fatawaa Sheikh Al-fauzan ]


Maelezo ya Mfasiri;

Hadith aliyoitaja Sheikh - Allah amuhifadhi - ameitaja Muslim namba (1565), na Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie - ameeleza hivi yaani amekataza kuuza ziada ya maji, kwa kawaida mara nyingi mtu huuza kile ambacho ni cha ziada kwa maana kimezidi katika haja na mahitaji yake,

Je, haifai kuuza maji moja kwa moja?

1 - Inaruhusiwa kuuza maji ikiwa mtu ameyamiliki kwa kuyaweka katika birika au tank n.k, ataruhusiwa kuyauza kwa sababu yamekuwa ni miliki yake kwa kuyakusanya au kuyazoa.

2 - Maji ya kisima au mto, au chemchem haya hayafai kuuzwa yaani yale maji ambayo kupatikana kwake hakutokani na tendo lake kwa maana hakuyahangaikia kama hayo ambayo Sheikh ameyataja.

Tanbihi:

Ikiwa hayo maji ambayo hauruhusiwi kuuza yanakutosha mwenyewe tu kiasi ambacho akitumia mwingine wewe unapata madhara basi wakati huo utaruhusiwa kunufaika nayo peke yako kwa sababu wewe ndiye mwenye haki zaidi,

Pia ikiwa watu wanapokuja kuchuka hayo maji yaliyopo katika miliki yako wanakuletea madhara kama vile kukanyaga mazao yako au wakawa wanaiba mazao yako au wakawa wanachukua maji yote kwa namna ambayo inakuletea madhara au wanakupunguzia mahitaji yako, au wakawa wanapokuja huleta maudhi kama vile kuchungulia utupu wako au wake zako, basi katika hali hii unaruhusiwa kuzuia,

Je, ni wajibu kuomba idhini kwa yule ambaye maji yapo katika miliki yake?

Ikiwa unajua kuwa mwenyewe anaruhusu basi hakuna uwajibu wa kuomba, ama ikiwa kama ataingia bila ya kuomba kutatokea fitna kama kupigana basi muda huu ataambiwa ni lazima aombe idhini kwa mwenyewe.


Tarjama na maelezo:
Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde - Allah amuhifadhi
๐Ÿ—“๏ธ Tarehe ya kuandaliwa:
3/Dhuสปl-Qiสปdah /1441H โ‰ˆ 24/June/2020M.

Dar es salaam, Tanzania
Kiunganishi: fawaidusalafiyatz
Jiunge nasi upate faida mbalimbali.

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu

Kupata faida nyingi zaidi jiunge nasi Telegram, bonyeza hapa: ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

๐Ÿ”— fawaidusalafiyatz

Jiunge nasi katika Instagram, Twitter, facebook na you tube:
@fawaidusalafiyatz

โ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ขโ€ขโœฆโœฟโœฆโ€ขโ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ข
 
Back
Top Bottom