hitler2006
JF-Expert Member
- Sep 1, 2014
- 370
- 213
Wakuu nimekuta mzozo juzi hapa mtaani kwetu mzee mmoja akilalama kweli...
Mtoto nimemsomesha kwa shida nimeuza ardhi na asset zangu nyingi nikitegemea akimaliza masomo atakuwa mkombozi katika familia yangu cha ajabu ananiambia nimtafutie mtaji sasa degree yake inamsaidia nini si bora asingeenda chuo kikuu.
Mzee aliongea kwa hisia kali tulijaribu kumuelewesha kuhusu upungufu wa ajira na namna vijana wanakumbana na mizengwe katika upataji wa mikopo katika taasisi za kifedha lakini mzee hakuelewa aliishia kusema kijana kafeli na kama kweli amemaliza chuo lazima aajiriwe.
Jamii inahitaji kubadili mtazamo juu ya kuajiriwa na kusoma hatusomi ili tuajiriwe bali tupate maarifa yatakayotusaidia kutatua changamoto za sasa na baadae ikiwemo ukosefu wa ajira.